UMEYA: Madiwani wa wawili wa CUF wajiunga na wenzao 8 wa CHADEMA Musoma Mjini

Shapecha

Member
Oct 21, 2010
45
1
Madiwani wawili wa CUF wameamua kuiunga mkono CDM musoma mjini katika mchakato wa kumpata meya. Musoma Mjini CDM ina madiwani 8, CCM 3 na CUF 2. Jimbo zima lina madiwani 13. Mwanzo mzuri wapinzani wanaungana bila vikwazo HR upo?
 
Yupo sana na udini wake. Nimeongea na diwani wa CUF amesema atamia chadema muda wowote maana anaona RH amegundua CUF ya mapalala haipo tena
 
Viongozi wa CUF mikoani wanafikiri mbele ya viongozi wa ngazi za juu. Hongera madiwani wa CUF huko Musoma, na kama kuna sehemu nyingine CUF wameshinda kwa kuwa na madiwani wengi, nashauri madiwani wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wawaunge mkono. Mwacheni Hamad aendelee kuiunga mkono CCM ila sisi wananchi tuunge mkono mabadiliko.

Nina imani kubwa CUF bara, ni kama ilivyo kwa CHADEMA na watanzania bara wote, hatujapata tunachokitaka ambacho ni haki yetu ya msingi - demokrasia ya kweli, haki kwa watu wote na uongozi kwa maslahi ya watanzania wote. CUF Zanzibar wasitulazimishe watanzania wote tuone kuwa mabadiliko tunayoyataka tayari yamekwishapatikana.

Hongereni sana madiwani wa CUF mjini Musoma.
 
Mijitu yenye upeo mdogo wa kufikiria ina taabu sana! Maana hata 1 + 1 wanaitafutia scientific calculator! Mweeee....
 
Big Up to your selves CUF Musoma.
Na yule diwani wa CUF Mwanza afanye hivyo tafadhali na Mungu wa Watanzania atambariki!
 
Viongozi wa CUF mikoani wanafikiri mbele ya viongozi wa ngazi za juu. Hongera madiwani wa CUF huko Musoma, na kama kuna sehemu nyingine CUF wameshinda kwa kuwa na madiwani wengi, nashauri madiwani wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wawaunge mkono. Mwacheni Hamad aendelee kuiunga mkono CCM ila sisi wananchi tuunge mkono mabadiliko.

Nina imani kubwa CUF bara, ni kama ilivyo kwa CHADEMA na watanzania bara wote, hatujapata tunachokitaka ambacho ni haki yetu ya msingi - demokrasia ya kweli, haki kwa watu wote na uongozi kwa maslahi ya watanzania wote. CUF Zanzibar wasitulazimishe watanzania wote tuone kuwa mabadiliko tunayoyataka tayari yamekwishapatikana.

Hongereni sana madiwani wa CUF mjini Musoma.

hapa hawana choice, kwani mahesabu na ccm hayaivi? yaani kura hazitotosha.
 
If you cant fight them join them i agree nawapa heko hao madiwani walioiunga mkono chadema kazi yetu ni moja tusonge mbele
 
sasa kwa hayo mahesabu hata wasingejiunga bado CDM ilikuwa na majority. Hiyo ni COMEDY too
 
Back
Top Bottom