Viongozi wa CUF mikoani wanafikiri mbele ya viongozi wa ngazi za juu. Hongera madiwani wa CUF huko Musoma, na kama kuna sehemu nyingine CUF wameshinda kwa kuwa na madiwani wengi, nashauri madiwani wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wawaunge mkono. Mwacheni Hamad aendelee kuiunga mkono CCM ila sisi wananchi tuunge mkono mabadiliko.
Nina imani kubwa CUF bara, ni kama ilivyo kwa CHADEMA na watanzania bara wote, hatujapata tunachokitaka ambacho ni haki yetu ya msingi - demokrasia ya kweli, haki kwa watu wote na uongozi kwa maslahi ya watanzania wote. CUF Zanzibar wasitulazimishe watanzania wote tuone kuwa mabadiliko tunayoyataka tayari yamekwishapatikana.
Hongereni sana madiwani wa CUF mjini Musoma.