Umeya kinondoni" vyama vya upinzani fungueni kesi

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,251
Hakika chama tawala CCM kinazidi kujionyesha uchovu wake katika Siasa za Tanzania.Kitendo cha kukodi madiwani walioapa kuwa in wa Manispaa ya Ilala Mama Ndalichako Na Mahiga Kuja kupiga kura Manispaa ya Kinondoni in umbumbumbu wa Sheria,Kitendo cha kufanya Uchaguzi bila Akidi kutimia huo nao in umbumbumbu wa Sheria.Nadhani in wakati muafaka Kwa Vyama vya Upinzani kwenda Mahakamani ili Mahakama iwafundishesheria CCM maana hawaelewi.Hizi siasa za ujanja ujanja mpaka lini CCM?
 
Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo
 
Hakika chama tawala CCM kinazidi kujionyesha uchovu wake katika Siasa za Tanzania.Kitendo cha kukodi madiwani walioapa kuwa in wa Manispaa ya Ilala Mama Ndalichako Na Mahiga Kuja kupiga kura Manispaa ya Kinondoni in umbumbumbu wa Sheria,Kitendo cha kufanya Uchaguzi bila Akidi kutimia huo nao in umbumbumbu wa Sheria.Nadhani in wakati muafaka Kwa Vyama vya Upinzani kwenda Mahakamani ili Mahakama iwafundishesheria CCM maana hawaelewi.Hizi siasa za ujanja ujanja mpaka lini CCM?

Karibu sana ofisi ya CCM Mwinjuma Kinondoni kuanzia Muda huu mpaka majogoo kuna Ka Tafrija Ka kujipongeza kwa kuaminiwa na Madiwani na kukabidhiwa kuongoza tena Manispaa !
 
Hivi mh. Rais Magufuri mimi kusema kweli ni CCM, ila napata shida sana kama ni wewe (mwenyekiti) wetu ccm unabariki haya mambo ya kihunihuni..

Mh. Rais nikwambie kabisa kama mtu mwenye hofu ya Mungu na mwanachama wa CHAMA CHW MAPINDUNZI kama kweli unataka kujenga nidhanamu ndani ya CCM na Tanzania kwa ujumla ebu achana na upuuzi wa watu wachache kufanya fitina za kijinga, simamia ukweli na fuata misingi ya democracy ili tusonge mbele.

Kama unaweza kuruhusu haya yanayoendelea kinondoni yakatokea ukweli unafundisha uhuni na utapeli kwa watanzania kuishi kihuni tu. Ebu simamia haki na usawa vitawale nchini mwetu.
 
*KWANINI CCM MNATUMIA NGUVU NYINGI ZA KUHARIBU UCHAGUZI WA MEYA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI!!?*



_*Martin Maranja Masese,*_

.., hiki ni kitu kingine ambacho kinanifanya niichukie CCM milele..., ni pale ambapo wanapotumia kila mbinu, kila jitihada kushinda kwenye maeneo ambayo hata wananchi wamewagomea na kuwakataa..., CCm mnajinasibu kama watu wa demokrasia usoni.., kumbe ni uzandiki na uongo kabisa..

Oktoba 2015 kila chama kilitumia nguvu na akili nyingi na muda wao kutafuta kura za uingwaji mkono, UKAWA (CCM, CUF, NCCR, NLD) wakapata uungwaji mkono jijini Dar es Salaam kwa kupewa madiwani na wabunge wengi.. Kwanini CCM hamtaki kuridhia jambo hilo!?

Awali katika uchaguzi wa kumtafuta meya wa jiji la Dar es Salaam ilitokea timbwili kama hii.., hadi kufikia mkurugenzi fulani kughushi nyaraka za mahakama ili uchaguzi uhairishwe.., (hatua hazikiwahi kuchukuliwa dhidi yake)


Tuendelee;

Uchaguzi wa kumtafuta meya na naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Kinondoni uliokuwa ufanyike katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika..

Sababu za kuvurugika kwa uchaguzi huo zimetokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza haswaa kwa upande wa CCM na mkurugenzi (msimamizi wa uchaguzi huo)..

.., uchaguzi wa kumtafuta meya wa manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa ambazo kimsingi zinaletwa na makada hawa wa CCM kwa kushirikiana na wakurugenzi (ambao wameacha weledi katika utendaji kazi sasa wameamua kuwa makada wa CCM)

.., tumewahi awali kulalamika kuhusu jambo hilo (wakurugenzi ni watendaji, hawapaswi kuwa makada wa vyama vya siasa)..

.., hawa CCM baada ya kugundua kwamba wanazidiwa idadi ya madiwani katika manispaa hiyo wakaamua kuwatumia wabunge walioteuliwa na Rais ili kuokoa jahazi.., (Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.) idadi yao inazidi wabunge 4 wa kuteuliwa na Rais (wanapaswa kushiriki uchaguzi wabunge wasiozidi 3 pekee katika halmashauri moja)

.., Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja..., kwamba mkurugenzi haifahamu hiyo sheria!!? Hawa wasomi wakubwa waliopelekwa kupiga kura tena maprofesa na madaktari hawafahamu mambo haya!?

..., Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga awali walikwisha kuapa kuhudumu kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje watake kupiga kura halmashauri ya manispaa ya Kinondoni wakati waliapia halmashauri ya manispaa ya Ilala?

..., zipi ni sababu za kumtoa Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo na kumtaka akashiriki kuwa diwani wa Ubungo wakati awali aliapa kuhudumu kama diwani wa halmashauri ya manispaa ya Kinondoni!!?

.., kuna nyakati nafikiria sana na kujiona ni mtu wa ajabu kuzaliwa Tanzania.., hivi mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi huu hafahamu taratibu za kuitisha vikao vya halmashauri!!? sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla ya mkutano.., mkutano huu wa leo umeitishwa jana tarehe 22-10-2016 (chini ya saa 24)

Uchaguzi hauwezi kufanyika tena kwa siku ya leo kwa sababu madiwani na wabunge wa UKAWA wametoka ukumbini.., madiwani na wabunge wa CCM (ukiweka na wale walioteuliwa na Rais) hawafikishi akidi.., yaani akidi haijatimia..

Kanuni za uendeshaji vikao vya maamuzi vya halmashauri zinataka walau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kipate uhalali..., 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. CCM ukiweka na wale wabunge 4 unapata jumla madiwani 18...

NB: _Taarifa nilizozipata hivi punde ni kwamba, pamoja na Augustine Mahiga na Joyce Ndalichako katika viapo vyao vya awali kuhudumu kama madiwani wa Ilala, leo wamepiga kura na kuchagua meya na naibu meya wa CCM, bila ile 2/3 kupatikana..._ _*Maajabu makubwa*_

Mapropesa na madaktari.., mnatuangusha sana watanzania.., yaani mnafanya usomi uonekane usanii...



Martin Maranja Masese
 
wewe
Hakika chama tawala CCM kinazidi kujionyesha uchovu wake katika Siasa za Tanzania.Kitendo cha kukodi madiwani walioapa kuwa in wa Manispaa ya Ilala Mama Ndalichako Na Mahiga Kuja kupiga kura Manispaa ya Kinondoni in umbumbumbu wa Sheria,Kitendo cha kufanya Uchaguzi bila Akidi kutimia huo nao in umbumbumbu wa Sheria.Nadhani in wakati muafaka Kwa Vyama vya Upinzani kwenda Mahakamani ili Mahakama iwafundishesheria CCM maana hawaelewi.Hizi siasa za ujanja ujanja mpaka lini CCM?
ulikuwepo eneo la tukio au mihemko tu
 
Mbona tunaambiwa CCM wamefanya uchaguzi na wamemuweka Benjamini Siita kuwa meya.?!
Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu niaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?
 
Elimu ya Tanzania ni kituko hasa hawa
Professor
Doctors
PHD


Yaani ni bure kabisa
 
<<<Ndo Ushapita huoo HATA ukienda Wap hupati kitu ''demokrasia sasa ni Mtihani Wa somo La kichina >>>
 
Nawashauri muende UN mkitoka huko mpitie ICC, nendeni kwa maalimu Seif atawapa muongozo
 
Back
Top Bottom