Umeya Dar es Salaam, Rais Magufuli ameonesha ukomavu kisiasa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
HIVI Karibuni Rais John Magufuli alizua gumzo nchini kutokana na kauli yake ya kukihimiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho anatazamiwa kuwa Mwenyekiti wake ifikao Juni kukubali matokeo ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Rais John Magufuli akizungumza kwenye tukio la kuhakiki silaha yake jijini Dar es Salaam, alitoa ushauri kwa viongozi wa CCM kujiandaa kisaikolojia kuyakubali matokeo ambayo yangetangazwa kwenye uchaguzi huo wa umeya. Katika kauli yake hiyo, Rais alisema upande wowote, uwe wa CCM au wa upinzani, yafaa uwe tayari kuyapokea matokeo ili meya apatikane na Jiji la Dar es Salaam liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi.

Rais Magufuli alisema: “Mahali tunapostahili kushinda (CCM) kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.” Kwa maneno hayo, Rais Magufuli ameonesha ni jinsi gani alivyo mtetezi wa demokrasia ya kweli. Licha ya kuwa muda mfupi madarakani, Rais Magufuli amesoma alama za nyakati na kuwathibitishia Watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa yeye katika utawala wake hatokuwa mkiukaji wa misingi ya demokrasia.

Rais akiwa ni kiongozi anayetokana na CCM anawaambia viongozi na wanachama wenzake wa chama hicho kuwa mahali ambapo CCM inastahili kushinda, sio ishinde tu, bali ishinde kwa ukweli, lakini mahali inaposhindwa napo ikubali kushindwa kweli na kusisitiza kuwa hiyo ndiyo demokrasia. Iko mifano katika bara hili la Afrika ya baadhi ya viongozi wastaafu wamewahi kukiuka na kuvunja misingi ya demokrasia ama kwa kuwatangaza hadharani watu au ndugu zao wa karibu wanaowataka kurithi nafasi za uongozi wa juu wa nchi na ule wa majimbo.

Katika hatua hii aliyoichukua Rais John Magufuli ni jambo la kupigiwa mfano kwa viongozi wengine, hususan wa Tanzania, walio katika chama chake au vingine kutambua kwamba Rais Magufuli hana uroho wa aina hiyo. Nimegusia vyama vingine, hususan vya upinzani ambavyo vimekuwa vikilalamikia chama tawala katika mazingira kama yaliyotaka kujitokeza katika umeya wa Dar es Salaam wakati ndani ya vyama hivyo hakuna demokrasia.

Kwamba baadhi ya hivyo wenyeviti wao hawataki kusikia kunajitokeza upinzani dhidi yao. Kauli hiyo Magufuli aliyoitoa hadharani ni yenye kuleta faraja kwa wale waliokata tamaa, kwani inaonesha kwamba anachohitaji kutoka kwetu ni sote kumuunga mkono bila kujali itikadi zetu za vyama vya siasa, maana sote tunajenga nyumba moja ya maendeleo, hivyo tusiwe na mihemuko ya kugombania fito.

Uchaguzi huo wa umeya wa jiji la Dar es Salaam, ulipitia vikwazo na michakato mingi kutoka kwa viongozi wa kisiasa wa vyama vya CCM na Chadema, kutuhumiana kuweka wapiga kura mamluki. Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kati ya kambi ya CCM na ile ya upinzani uligubikwa na kupigana vikumbo na vijembe vya maneno ili mradi kila upande ulikuwa ukivutia upande wake ili kunyakua kiti hicho cha Umeya.

Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa inachukua jukumu la kisheria la kuahirisha uchaguzi huo ili kujiridhisha kuwa taratibu zote zinafuatwa ili kutimiza matakwa ya kidemokrasia katika kuwapata viongozi wanaotokana na uchaguzi huru na haki. Kinyang’anyiro kwenye uchaguzi huo kilikuwa ni kati ya Isaya Mwita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Yenga Omari (CCM).

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sara Yohana, alihitimisha kelele na mihemuko ya kisiasa kwa kumtangaza hadharani Isaya Mwita ambaye ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema) akitokea Wilaya ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi kwa kupata jumla ya kura 84 na kumshinda aliyekuwa mpinzani wake, Yenga Omary (CCM) ambaye ni Diwani wa Kinondoni aliyepata kura 67.

Baada ya Ushindi huo, Yohana aliwashukuru wapiga kura kwa kuhitimisha zoezi hilo la kihistoria kwa jiji la Dar es Salaam kwa kumalizika kwa amani na utulivu hadi mshindi akawa amepatikana. Ni tukio la kihistoria kutokana na ukweli kwamba ni mara ya kwanza katika jiji hilo kuongozwa na meya anayetokea upinzani. Uchaguzi huo umekuwa ni wa kihistoria baada ya kuiweka nchi yetu katika ramani ya kisiasa hususani kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ukizingatia pia jiji la Dar es Salaam ni kitovu cha kibiashara kwa nchi hizo, hali iliyosababisha msukumo wa watu kutoka ndani na nje ya nchi kujua hatima ya uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora jijini Mwanza, Jimmy Luhende, anasema Rais Magufuli ameonesha ukomavu wa kisiasa kwa kuhimiza uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ufanyike kwa haki na kwa kuzingatia demokrasia bila kujali mshindi anatoka chama gani.

Anasema ni nadra kusikia kiongozi wa Kiafrika na hasa Rais wa nchi akikemea chama chake kutokulazimisha mambo na badala yake wakubali matokeo na kuweka mikakati mpya ya kushinda katika chaguzi zijazo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo anaunga mkono kauli ya Rais John Magufuli akisema dalili za CCM kushindwa katika uchaguzi wa kiti cha umeya jijini Dar es Salaam zilikuwa za wazi na kulikuwa hakuna namna nyingine.

“Mimi naiunga mkono kauli ya Rais Magufuli, amefanya jambo la kidemokrasia, maana hata kama meya wa Dar es Salaam angeshinda kutokea CCM alikuwa hana madiwani wa kutosha wa kufanya nao kazi,” anasema. Anaongeza: “Kwa kauli ya Rais, kuwa tukishinda tushinde kweli, umeona mwenyewe katika uchaguzi wa marudio ya urais Zanzibar tumeshinda na watu wamefurahi.”
 
Vipi Zanzibar napo kaonesha ukomavu wa kisiasa?
 
Back
Top Bottom