Umeweka bajeti kiasi gani katika sikukuu za mwisho wa mwaka?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
28,811
39,019
Maisha ya mwanadamu huwa ni ya kuangaika/kutafuta na baadaye aweze kuburudika.Wengine uweka bajeti kwa kudunduliza kidogo kidogo na hatimaye wanakamilisha furaha yao katika kusherehekea kile walichokipanga.Kila mwisho wa mwaka huwa kuna sherehe nyingi na huwa zinawapa faraja na matumaini karibia binadamu wote katika hii dunia.Wenzetu wa mataifa mengine wana ule utaratibu wa kuweka akiba ili mwisho wa siku mambo yaende sawa.Kwangu binafsi bado napambana angalau niweze hata kununua soda siku hizo zikifika.Je wewe umebajeti kutumia kiasi gani?
 
Nimetengeneza Kibubu tangu ilipoisha sikukuu ya Pasaka na ninaweka kila siku kuanzia buku mbili, nikikosa sana buku.Nitakifungua kwenye Xmas na sherehe hizo zikiisha natengeneza kingine kwa ajili ya Pasaka
 
Unataka kuwachinjia watoto ng'ombe ama?
 
Nimetengeneza Kibubu tangu ilipoisha sikukuu ya Pasaka na ninaweka kila siku kuanzia buku mbili, nikikosa sana buku.Nitakifungua kwenye Xmas na sherehe hizo zikiisha natengeneza kingine kwa ajili ya Pasaka
Hongera mkuu,wengi huwa tunapanga hivyo ikifikia hatua ya utekelezaji inakuwa ni tatizo
 
Baada ya Xmas na mwaka mpya ndiyo nafungua kibubu changu.
Watu huwa wamepigika sana. Kwangu ndipo nafanya starehe za kuchagua kama nyama kwenye bucha.
ha ha ha na wengi ikishafika january-February huwa ni matatizo,mahitaji ya fedha yanakuwa makubwa kuliko mapato.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom