Umewahi ziona hybrid cars hapa bongo? Je, zinastahimili changamoto mbalimbali? Wataalamu karibuni!

Kudasai

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
204
231
Habari za week end Wakuu?
Niende kwenye mada moja kwa moja. Ni hivi, huku Japan (Niko kwa Sasa) gari zinazoonekana kwa wingi barabarani ni:

1. Gari ndogo zenye ukubwa wa 650cc engine size.

2. Hybrid cars ambapo Toyota Prius na Toyota Aqua Ndio zinazoongoza.

Hizi gari ndogo zinapendwa kwasababu matumizi yake kwa ujumla ni nafuu mf. Matengenezo, kodi, nk.

Sasa Basi, Lengo la kuanzisha uzi huu ni kuhusu hybrid cars.

Kwa mfano 4th generation Toyota Prius tolea la 2016 inatumia 1L kutembea about 40km. Hili ndilo tolea la mwisho kwa Sasa lakini kuna 1st, 2nd, na 3rd generations. They are Very economic in fuel utilization kwa sababu ina battery system kuhifadhi na inatumia umeme. Sio Toyota peke Yao Wana hybrid cars; Mitsubishi, Nissan, Honda, nk pia wanazo.

Sasa Basi hoja yangu ni kwamba hizi gari zinaweza stahimili mazingira yetu? Ninamaanisha uchakachuaji wa mafuta ni rahisi sana kuziua hizi gari.

Karibu tujadili kwa wenye uzoefu au wamiliki wa hizi gari.

Picha hizi hapa:
 
ca0618729bb3c723ef9d755b8e035826.jpg
86c32a2f88f2810c57a283a69a8e4b24.jpg
cbf022d546e3e2c813fdf17ccb3716f3.jpg
 
hizi gari ni nzuri kwa fuel consumption baadhi 1L inaenda mpaka 56km, inategemea na jinsi unavyoliendesha kwasababu kama unaendelesha below 60 or 40km/h (sina uhakika) linatumia umeme hivyo una save fuel lakini sijajua gharama ya maintanance ya huo mfumo especially durability and cost of repalacing new battery.
 
MKUU SIKUSHAURI kabisa ununue hizo gari sababu kubwa ni spea mm nishakutana nazo kama 7 hivi na zote mpaka kufikia kuharibika ni kisa kimoja 2.ile gari huwa ina kuwa na betri 2 ya kawaida mbele na nyuma kunakuwa na betri kubwaa ya hybrid .

tatizo huwalinakuwa betri ya haybrid ikiisha charge hapo ndio kwisha kazi.maana huwa inachajiwa na mashine maalum kwa wenzetu ukiingia kwenye vituo vya kujazia mafuta huwa kunakuwa na cable kwaajili ya kucharge betri kuna soket unachomeka kama unajaza mafuta vile.

mm nilitegemea TOYOTA tanzania labda wangekuwa na hizo mashine lkn hakuna betri ya hybrid ikiisha basi gari haiwezi kuwaka tena.kuna gari tulihangaika nayo sana kujaribu kucharge hizo betri kwa njia ya kucharge cell moja moja tukafika kwenye gari tukaweka ikazunguka mara moja tuu na zikaenda down.

na hata hivyo wataalam wakutengeneza hizo gari nao ni shidaa.
mm nashangaa sijui kwa nn toyota wasingekuwa wanaendesha mafunzo kwa mafundi wanao taka kujiendeleza ili iwe rahisi mafundi kurekebisha gari zao??

mfano now gari za D4 zinaonekana kama kimeo sana wakati sio kweli kbs badala ya kufundisha watu jinsi ya kuzirekebisha wao wapo kimyaa tuu.

kwanza tanzania hakuna chuo cha kufundisha ufundi huko VETA ukienda wanafundisha magari ya mwaka 70 huko unafundishwa starter ya 109 rand rover?? hahahahahha
 
MKUU SIKUSHAURI kabisa ununue hizo gari sababu kubwa ni spea mm nishakutana nazo kama 7 hivi na zote mpaka kufikia kuharibika ni kisa kimoja 2.ile gari huwa ina kuwa na betri 2 ya kawaida mbele na nyuma kunakuwa na betri kubwaa ya hybrid .

tatizo huwalinakuwa betri ya haybrid ikiisha charge hapo ndio kwisha kazi.maana huwa inachajiwa na mashine maalum kwa wenzetu ukiingia kwenye vituo vya kujazia mafuta huwa kunakuwa na cable kwaajili ya kucharge betri kuna soket unachomeka kama unajaza mafuta vile...
Mkuu LEGE, Umejitahidi kueleza vzr sana! Big up kwa ushauri murua
 
Back
Top Bottom