GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,281
- 6,696
Binafsi nimewahi kwenda mara kadhaa nikiwa na timu fulani ya Mpira wa Miguu, Siku moja nikiwa na hiyo timu nilipewa kitu ambacho nilifunga katika maeneo nyeti 'sehemu za siri' HAKI YA MUNGU siwezi kusahau, wakati nafunga ilikuwa kawaida lakini baada ya mechi kuanza ilikuwa kana kwamba nimefunga Mzigo wa kilo kumi, Ilifika wakati nikahisi Nanihii inataka kukatika..... kukaanza kufukuta si mchezo kana kwamba limewekwa Jiko la mkaa, ilifikia wakati nilianza kulia kimyakimya uwanjani
Nikaomba kutoka, viongozi wa BENCHI LA UFUNDI WAKAKATAA wakasema mimi nisitoke, mpaka nikajisingizia kuumia nilipotolewa nje ukawa ni muda wa mapumziko nikatafuta namna ya kwenda chooni, nilipofika huko nikafungua na kutupa kila kitu, Siku hiyo nilitafuta upenyo nikatoroka uwanjani na ndio mechi yangu ya mwisho katika maisha ya soka, mpaka leo sijawahi kucheza mpira wa kimashindano hata hivyo umri nao hauruhusu.
Pia wakati huohuo niliwahi kumpeleka mtu ambaye alikuwa na kesi ya wizi wa fedha za Umma, akafanyiwa mambo na mtaalamu huyo ili aweze kushinda kesi, Alishinda kesi lakini kwa kiasi kikubwa naona RUSHWA ndio ilimuokoa bado sikuweza kuiona nafasi ya mganga.
Ni miaka mingi sasa sijawahi kwenda kwa Mganga na haitatokea kabisa, nimekuwa mtu wa tofauti sana kwa sasa.
JE UMEWAHI KWENDA HUKO? NI YAPI ULIKUTANA NAYO? Hebu tupe uzoefu wako.