Umewahi kuwekeza nini kwa ajili ya mapenzi (mahusiano) na mkaja kuachana?

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,573
Swali langu ni umewahi kuwekeza kitu gani au shilingi ngapi kwa kukadilia katika mapenzi ili kudumisha mahusihano yako na mwanamke au mwanaume?

Ngoja niongelee kwa upande wangu,
Mimi nimekua ni mtu mgumu sana kutoa kitu changu au pesa yangu kwa ajili ya kumpata mwanamke, siamini katika hilo hata kidogo.
Nitampa pesa yangu mwanamke ambaye tayari ni mpenzi wangu.

Mbali na gharama za kulipia mahitaji siku ya kwenda kupimana pumnzi (kunyanduana) umegharamika vipi kum keep mpenzi wako katika himaya yako???

Wakati nina kama 21 age hivi kitambo kidogo, nilikua naringa sana na kujikubali, yani nilikua natongoza mademu wa kali tu, hadi nikutane na beuty hasa ndio natongoza, mbali na hapo mamanzi wa kawaidi hata wakinishobokea nilikua nawakwepa kabisa sina time nao.

Kama unavyojua kukutana na mwanamke mkali na anae jielewa wa age hiyo ya kwangu ilikua ni nadra sana, kwanza wengi ni wanafunzi na mimi muda huo nipo kitaa napiga kazi.

Basi bhana siku moja nikakutana na binti kamaliza kidato cha nne. Ni mzuri for sure tena sana. Siku hiyo nilikua maeneo ya kazi na binti huyo alikua kamsindikiza dada yake clinic ambae ni mjamzito, so nilimkuta kakaa kwenye kiti peke yake akimsubili atoke (alikua karbu na maabara)

Nikaona niingie kwanza maabara na mimi, nikafika nikamuuliza mwana hapo maabara huyo manzi mzuri kakaa hapo nje ameingia humu kwako? Akanijibu ndio.

Daaa nikamwambia mwana leo zamu yangu lazima niombe jimbo kwa huyu dada, ila hujamtongoza kweli wewe maana ninavyokujua wewe, jamaa akanipoteza akasema ni mjamzito huyo kaja kupima arudishe mjibu clinic

Daaaa niliishiwa pozi kabisa lakini nilipofikiri kidogo na kutoka nje kumuangalia vizur nikaona binti hafananii kabisa kuwa ni mjamzito, nikahisi jamaa kanidanganya.

Mwisho nikamfata huyo binti, na alivyokua mzuri nilimpa namba yangu ili kama asiponitafuta basi nitajua hakuvutiwa na mimi hata kidogo.

Basi bhana huyo binti alinitafuta siku hiyo hiyo jioni, ukaribu ukaanza.
Hakutaka kukubali mahusiano ya kimapenz moja kwa moja alitaka nimpe muda tuendelee tu kuwa karbu kwanza.

Nilikua nampenda sana ila ujinga niliofanya ni mmoja, sikuwahi kumpa gift yoyote kabisa mbali na kutembea nae sehemu mbalimbali, kwenda stadium kuangalia mpira, na kula nae sehemu za outing, n.k ice cream tulikua tunalishana yani kama wapenzi.

Na baada ya mimi kuona manzi hafikirii ngono na mimi nikawa na jealous kwa mbali.

Na kumbuka tulipanga out siku moja ilikua boxing day, nilivo fala niliacha simu charge ikiwa silent nikawa naangalia match za England.
Siku hiyo nilimkera najua ila hakuongea kitu alisema basi siku nyingine.

Basi zilipita siku kadhaa binti akaniaga anaenda shule. Akiwa mbali mahusiano yakaenda yanapungua hadi tukaacha kuwasiliana.

Nilikuja kumtafuta baada ya miaka miwili akadai anamtu wake na hawezi kumuacha.
Asee niliumia sana.
Hapo ndipo nikaanza kukumbuka ufala wangu, kwanini sikuwekeza kwa huyu binti????

Ila kuna muda huwa najitia moyo nasema, kama yeye alikua ananipenda kweli, kwanini hakutaka kuniweka kuwa mwanaume wake wa kwanza, kwamba siku akiwa tayari kuanza mahusiano ya kimapenzi anitafute na kuniambia nipo tayari kufanya mapenzi na wewe.

Au kwa nini toka tuache kuwasiliana hakufikiria kunitafuta tena?

Najifariji nasema itakua na yeye ni wale mabinti ambao anaweka pesa mbele kwenye mahusiano ndio hisia za mapenz zinafata nyuma, japo alikua akinisifia mie mzuri.

Nilienda chuo tena nilipo rudi.

MWANAMKE wa pili ambae nilimpenda na kutamani kua awe mwanamke wa ndoto zangu huyu alikua mbali na mimi, so nilipokua vizuri kipesa nilimtafuta, ilikua mwaka jana tu hapa.
Nikasema huyu nitaweza kwake.

Alikua mpenzi wangu wa utotoni nikiwa kidato cha kwanza, sasa mwaka jana tulianza mapenz ya utu uzima.
Tulidumu mwezi mmoja tu tukaachana.
Sababu za kuachana ni..
Alikua ni mwanamke anaependa hela kupita maelezo, kila ndoto yake ya maisha anafikiria mwanaume ndie atamtimizia ndoto yake..
Alitaka ndoa haraka sana, yani mipango ambayo mimi nilikua naipa mwaka mzima yeye anataka itimie ndani ya miezi mitatu.
Ghafla uchumi wangu uliyumba, mie nikaona hakuna haja ya kuendelea kua nae. Ananipa stress tu.
Kuna siku tunajibizana nikamwambia acha usenge kua muelewa, basi ikawa kosa kila mtu akapita njia yake.
Alikuja kuomba msamaha na mimi nikamjarbu na kumwambia sina kazi kwa sasa na ninasoma, mtihani huo ulimshinda ndani ya wiki tu, akanipotezea na kuona mimi sio riziki.

So, sikuweza kuweza chochote cha maana kwa huyu mwanamke kwani ilitokea tukaachana haraka.
Yani nakumbuka hela ya kusuka nilitoaga mala moja tu, and no gift ila yeye nina gift yake moja hadi leo.

Mahusiano yangu ya chuo yalikua ya kisela sana, na sikuwahi kuwa na mahusiano mazito chuoni.
Chuoni nilikua mgumu tu sina hela, nikipata ni pombe na masela, bangi kidogo na kwenda kuruka basi.
Mademu partial sana kwa ubahiri wangu.

HUKU KUWEKEZA KUMEKAAJE?

kupata mke ni kazi sana bila kumshirikisha Mungu.

Wewe una lipi la kusema? usiwe msiri ni kujifunza tu.

Leo nimeandika Uzi mrefu kazi kwenu manaopenda kusoma.
 
Ur clever man wala usijilaumu kwa loloteh. Wapo wanao wekeza na bado mahusiano yanakuja kuvunjika after few month,days or years. Kama mwabamke abapenda sana hela basi ahakikishe kwabla ya yy kuolewa aje na zake ili isije leta tabu badae maan somerimes wanataka mambow mazuri na makubwa bila kujali kwamba hata sis we have our own plans and goals in life
 
It's true kupata mke mwema ni kazi sana bila ya kumshirikisha Mungu,siku hizi wanawake wengi focus yao ni pesa,kama hauko vizuri utaishia kuchanganywa na wanaume wengine,dunia imebadilika sana,na wale wanaoanza mapenzi katika umri mdogo wameishia kutendwa kwani wanaume wengi kiuhalisia hela ni ngumu,na akishakujua wewe ni mpenda hela/mizinga isiyo na akili hamfiki mbali lazima aingine mitini...
 
Mimi wa kwangu alikuwa ananipenda mpaka anatoroka kwao usiku anakuja kwangu ananiletea chakula naona tu anazingua masikini. Anapanda boda boda mtoto wa watu yule usiku anahangaika, mimi vituko vyote nilivyokuwa namfanyia lakini alivumilia. Kuja kushtuka ashaolewa na Mchungaji Mkubwa huko Kenya ndipo nilijua kuwa "you never miss a good thing till it's gone" I was busy collecting stones to realiaze that I had lost a diamond.
 
wanza, kwamba siku akiwa tayari kuanza mahusiano ya kimapenzi anitafute na kuniambia nipo tayari kufanya mapenzi na wewe.
Sahau hii
 
Mimi yupo mmoja huyo ilikuwa

Kila siku natuma 5000 ya kula
Mwisho wa mwezi 10000 ya umeme
Kila weekend natuma 10000 ya saloon
Kila week namuunga Brando la 3000 la week kifurushi .

Lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua yote haya ninayomfanyia moyoni mwake Simo hapo ndipo nilipogundua kumpenda mtu asiyekupenda ni sawa na kazi bure hata umfanyie nini ,,,

Ilinichukua muda mrefu kujitoa katika hayo mahusiano maana binti nilikuwa nina mpenda sana kuachana na Yule binti mpka nakuja kukaa sawa ilinichukua almost miezi 6 kukubali uhalisia sipendwi nahitaji kuanza upya

Ila nashukuru baada ya kuanza upya niko vizuli na Yule binti mpka leo hii bado ananitafuta tusahau ya zamani tufungue ukurasa mpya
 
Mimi yupo mmoja huyo ilikuwa

Kila siku natuma 5000 ya kula
Mwisho wa mwezi 10000 ya umeme
Kila weekend natuma 10000 ya saloon
Kila week namuunga Brando la 3000 la week kifurushi .

Lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua yote haya ninayomfanyia moyoni mwake Simo hapo ndipo nilipogundua kumpenda mtu asiyekupenda ni sawa na kazi bure hata umfanyie nini ,,,

Ilinichukua muda mrefu kujitoa katika hayo mahusiano maana binti nilikuwa nina mpenda sana kuachana na Yule binti mpka nakuja kukaa sawa ilinichukua almost miezi 6 kukubali uhalisia sipendwi nahitaji kuanza upya

Ila nashukuru baada ya kuanza upya niko vizuli na Yule binti mpka leo hii bado ananitafuta tusahau ya zamani tufungue ukurasa mpya
Mimi nanavyo fikiri ni heri kukaa bila mke hadi ukafika hata miaka 35, kuliko kulazimisha kuishi na mtu ambae sio sahihi.
 
wanza, kwamba siku akiwa tayari kuanza mahusiano ya kimapenzi anitafute na kuniambia nipo tayari kufanya mapenzi na wewe.
Sahau hii
Mtu kama anakupenda anaweza kufanya hivo, japo ni ngumu.
 
juma balo aliimba pendo la zaman lilinikondesha walitajiani kunikumbusha ujuemoyon wanisikitisha.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom