Umewahi kuwa mtalii ndani ya Tz na kujionea maajabu haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kuwa mtalii ndani ya Tz na kujionea maajabu haya?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by J.K.Rayhope, Oct 27, 2011.

 1. J

  J.K.Rayhope JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nabaki na maswali mengi sana kichwani,hivi kweli serikali yetu ina mpango gani wa kizalendo wa kukuza utalii wa ndani?Mlima Kilimanjaro uko tz,hivi kweli mjerman anatumia mamilioni ya maili kuja kuuona,halafu mimi mtz nasaga ndala na sina muda wa kufanya utali wa ndani,kwanza mimi kama mtz sijahamasishwa hata na wenye mamlaka,au hata kwa motisha.Kwa ujumla niseme wote tumelala.Kisiwa cha Saa 8 (mfano)akilichopo ndani ya Ziwa Victoria nililazimika kukitembelea baada ya mwl wangu wa somo la history nikiwa Kibasila sec,(Dar) kuzungumzia juu ya kisiwa hicho,nilipotembelea mwanza baadae niliamua kuupata ukweli wa maneno ya mwalimu wangu,niliridhika sana tu,utalii wa ndani kwa tz upo chini sana.Sehemu zote zenye vivutio tuzitembelee tujifunze,au ndio wageni kwanza wenyeji b'dae?Tuwe na desturi ya kujifunza NATUREWORK YA MUNGU.Uone fahari ya kuwa MTANZANIA
   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Bosi ungejua kwa hali ya kimaisha ilivo ngumu, sina hamu na ufahari wa Tanzania. Wenzetu wanachapa kazi ,wanalipwa vizuri then anachukua likizo kupumzika na ana akiba ya kutosha. Sisi hapa hatuna National Insurance, Ada za shule juu, sembe juu, umeme juu, maharage juu, bati juu..halafu mtu apate wapi hela ya kwenda Kilimanjaro? Mimi siwalaumu watu. Siku maisha yakiwa bora utashangaa watu watakavyojaa huku. Siyo kuwa hatupendi bali huwezi kuacha kulipa kodi ya meza kwa kuangalia wanyama ati!
   
 3. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono Mkuu. Umesema kweli kabisa. Umetuwakilisha vema sisi wakesha-hoi. Mi natamani sana lakini kipato changu kimezidiwa na majukumu, hatimaye kuzima ndoto zangu.
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Mbona haujatuhamasisha sasa? Hicho kisiwa kina vivutio gani na sisi tutamani kwenda kukiona? Mimi nimetalia kiasi TZ, Kili nimepanda, Ngorongoro, Serengeti etc.
   
 5. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Utakuwa mmoja wa waliofaidi kauli mbiu ya CCM, 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania....mwenye uwezo wa kuchonga dili halali au haramu" teh teh teh
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Wabongo wengi wakikata bajeti ya Bia,Kitimoto na za kuhonga wanawake mwezi mmoja tu wanapata pesa ya kupanda Kili, ni priorities tu.
   
 7. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa ni sanctuary ya wanyama tu na ndege. Sijui kama bado wapo.
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  nakumbuka nilikwenda kishule kutembelea mikumi lakini baada ya hapo sijabahatika kutembelea sehemu nyingine tena.
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Yep inapendeza; ni experience ya kufa mtu!
   
 10. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NCAA mwezi wa 12 huwa wanatoa gari kwa ajilia ya wazawa kwenda Ngorongoro kwa bei nafuu kama vikundi.
  Nauli huwa around buku 10 na kiingilio ni kama Tsh 1500.
  Msosi unajitegemea lakini ni day trip.
  Pamoja na kwamba wanapigaga promo, lakini response bado inakuaga ndogo kinoma.
  Huwezi niambia kwa mwaka mzima unashindwa kijipanga ukakosa buku 15 kuvisit mahali bomba kama Ngorongoro.
   
 11. k

  kauzu pipo Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hzo nzo ni starehe kama kwenda kuangalia mlm kilimanjaro. Kwa hali ya umaskini tanzania na kwenye familia zetu c dhani kama tunachoice. Hizo hela za starehe ni bora kusomesha watoto wa ndugu na na marafiki. Tusiige kila kitu wanachofanya wazungu kwaani hali yao inawaruhusu.
   
Loading...