Umewahi kutembelea familia yenye toto lililodekezwa?!

si mna wa kwenu? waleeni kikamanda. au zaeni wa kwenu mlee mtakavyo
kumbukeni watoto hawafanani, na kuna umri hata uchape vipi mtoto hasikii. mnaweza kuwalaumu wazazi ila wengine watundu mnoo
 
  • Thanks
Reactions: D23
si mna wa kwenu? waleeni kikamanda. au zaeni wa kwenu mlee mtakavyo
kumbukeni watoto hawafanani, na kuna umri hata uchape vipi mtoto hasikii. mnaweza kuwalaumu wazazi ila wengine watundu mnoo
Hakuna lolote, mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo, sisi tulilelewa kikamavu nashangaa kizazi hikihiki watoto wetu tunataka kuwalea kama mayai, toto limemaliza kula hata kuosha sahani yake tabu mnataka kila kitu afanye dada upuuzi mtupu.

Wanawake ndio wanaowaharibu watoto wa kizazi cha leo kwa upendo wa kipuuzi kumbe unampoison mtoto bila kujijuwa.
 
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Luninga, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Luninga, mwenyewe anakaita junia sijui junia ndio hivyo hivyo, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja, basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote.

Nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, "No Junia no...! is bad!” Na kucheka cheka huku akisifu, "Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, "Junia no!", anapanda meza mara kabati, jamaa yangu na mke wake utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, "No Junia no" Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, 'Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, 'No Junia no'.

Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Junia akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi...! "Leo umekuja kula kwetu?" "Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?" Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, "Junia yu a veri bed". Sasa chenyewe si kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zereu.

Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichin... "We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio kabisa".

Eeh bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza "Junia umefanya nini tena baba?" kimya "Junia what has happened?" kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake, "Huyu kafanya nini?" Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa... "Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko".

Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, "Junia a yu sik? Unaumwa?" Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio.

Wengine hatuangaliagi Luninga ohooo!!

WAZAZI WA ZAMA HIZI HII INATUHUSU ASILIMIA 100!

TUWE MAKINI NA ST FRANCIS SCHOOLS! ZINAFUNDISHA INGLISHI TU SO MALEZI!
SHAURI YETU!
Hahahaaa nimecheka sana ila we ni kauzu mkuu
 
Aisee,hako "kajunyia" kapo hapa kwa jirani yangu.Kina tabia hizo hizo ulizotaja.Ila wao hawakaiti junyia,wanakaita "plinsi".Picha linaanza shikamoo kwake mwiko(kwa baadhi,ya watu shikamoo ina-mata).Af,baba ake kila siku anahadithia leo prince kavunja hiki,mara jana kavunja hiki,huku akiwa anacheka😁😁😁😁.
 
Hii ndo sababu kubwa ya kuwepo wanaume wa Darisalama,
Kitu kidogo janaume linalia,
Kujikwaa kidogo tu janaume zima linatuma kwenye group sijui lisaidiwe nini bure kabisa!

Na hiyo ndo sababu nyingine ya kuzalisha jitu zima liko kwenye 50's lakini linajipakaa caroline ili liwe jeupe pambaf sana.
 
Back
Top Bottom