Umewahi kutapeliwa? Njoo tuelezane mbinu za matapeli

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Baada ya ile njia ya tuma pesa kwa namba hii jina litakuja fulani kushindwa ,ikaibuka kuna fedha imetumwa kwako kimakosa ,pamoja na zile za miamala ya mawakala kulizwa na miamala ya bank

Sasa hii naona ndo mbaya zaidi

Ukirudishiwa chenji usichanganye na hela zingine ambazo unazo,ukizichanganya baada ya muda utajikuta huna pesa yako

Ukiokota pesa barabarani,njiani au sehemu yoyote usichanganye na hela zako ,aisee hii imempata mshikaji wangu kabisa wa karibu

Asubuhi ya leo alikuwa anawahi kwenye biashara zake,alikuwa anaenda kufuata mzigo (dagaa huko ziwani)

Wakati anawahi gari ili aweze kuelekea ziwani njiani akakutana na hela elfu 20 noti mbili za elfu 10 ,akaziokota akaziweka pamoja na milioni mbili alizokuwa nazo .

Akapanda gari ,na kwenye gari walikuwa watatu tu,abiria wawili na dreva tu ,wakati safari inaendelea akawa anataka kulipa nauli ili dreva aongeze mafuta ,kutoa pesa akajikuta anatoa majani ya mime,hela hana bali ana majani mabichi ya mimea

Akahisi kuchanganyikiwa ,ulizia wenzake hamna,check kila sehemu hamna

Pia nasikia ukiwa unataka kusafiri nchi za nje kupitia mpakani ,kuna wale wabadilisha fedha,sasa na wale huwa wanawaliza watu sana,anakuhesabia hela vizuri na wew unahakikisha kwa kuhesabu mara mbili mbili na baada ya kujiridhisha,ukiwa safari unajikuta huna hela,kumbe wanatumia viini macho kukuhesabia hela,wanapendekeza kama unataka kubadilisha hela uende kwenye maduka makubwa kuliko wale watu wa vichochoroni

Unakaribishwa kuweka aina za utapeli ili kuwaokoa wengi
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,077
2,000
Mimi pamoja na uzoefu wangu wote kwenye biashara ishu ya CHUMA ULETE sijawahi kuiamini

Yaaani swala la hela kupotea kwa mazingaombwe/kiini macho sijawahi kuliamini. Najua kuibiwa na huwa naamini watu huwa wanaibiwa tu kwa nguvu,kwa madawa(sio ya kienyeji), kwa kutapeliwa au kudondosha hela ila sio hela kutembea yenyewe itoke mfukoni au kwenye droo ipotee
 

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Mimi pamoja na uzoefu wangu wote kwenye biashara ishu ya CHUMA ULETE sijawahi kuiamini

Yaaani swala la hela kupotea kwa mazingaombwe/kiini macho sijawahi kuliamini. Najua kuibiwa na huwa naamini watu huwa wanaibiwa tu kwa nguvu,kwa madawa(sio ya kienyeji), kwa kutapeliwa au kudondosha hela ila sio hela kutembea yenyewe itoke mfukoni au kwenye droo ipotee
Mkuu watu wanalizwa kwa viini macho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom