Umewahi kutapeliwa kwa njia gani?

Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
2,112
5,208
1. Kuuziwa dhahabu feki

2. Tuma pesa katika namba hii

3. Mwanao anaumwa shuleni (boarding) tuma hela

4. Kudanganywa unaunganishiwa vifurushi vya chuo, unawapa password ya MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, HALOPESA. Baada ya hapo unaona meseji tu za imethibitishwa umetoa hela.

5. Kubadilishiwa simu yenye "line" ya uwakala. (Hii watoa huduma za kifedha kwa simu wanaifahamu)

6. Kupewa lift na watu kwenye gari wakijidai kuulizia sehemu kwamba hawajui ilipo, unawalekeza wanakuambia kama hutojali tunaomba tukupe lift utuoneshe, ukipanda kwenye gari yao huna hela mfukoni na hujui zimetokaje.

7. Bonanza kumulikwa "tochi" na hela zinadondoka zotee yaani. (hii kama kuna mtu anaijua nadhani ni nzuri maana wachina wanapigwa hadi wanachanganyikiwa)

8. Mtu kujifanya amekosea kutuma hela kwenye akaunti yako hasa MPESA n.k. Ukisema hujatumiwa hapo hapo inaingia meseji!

9. Mtu anakupigia simu na kusema anakufahamu, anakupa mchongo kua anafanya kazi UN, kuna madili anataka kupiga huko mshirikiane. Ila anaomba umtumie hela kwanza. Mazao, madawa ya kilimo n.k(UNAPIGWA).

10. Mtu anakuomba hela akuunganishie kazi (migodini kama GGM, watu wanapigwa sana afu dada zetu wanachezea "cassava" sana na kazi hapati)

11. Mtu anakuja anapiga picha nyumba yako anaenda kwenye taaisisi inayotoa mikopo, anabeba hela kisha anatokomea (msala utabeba wewe)

12. Mawakala huduma za kifedha (MPESA n.) kubadilishiwa jina la "boss" (mwajiri wako) kwenye simu. Yaani mtu anawinda simu yako unayotumia anaisaka namba ya boss wako kisha anaandika yake, akitoka hapo anaanza kukuomba umtumie hela kwenye namba flani (anakutumia hiyo namba) kisha unapigwa hela zote

13. Kumtumia mdada hela ya nauli na humfahamu, kisa kakumbia anataka aje umnyandue, unatuma hela na unapigwa block.

14. Mawakala wa benki, matela (Tellors). Hawa watu nao ni hodari kwa kudondosha misimbazi na buku tano tano. Umehasabu zako laki 1 unaambia mbona hela ipo elfu tisini

15. Kwenda kukopa hela benki au kutoa akiba yako yote na unawapelekea QNET, GLOBAL ALLIANCE, LONG RICH na takataka kama hizo huku ukiahidiwa utakua bilionea baada ya miezi kadhaa. hapa walimu wengi wamelizwa sana, sjui hua wanakwama wapi walimu?

NB: Katika heka heka za mishe mishe mjini, kama hujawahi kutapeliwa ni jambo la kumshukuru Mungu. Hebu tupeane uzoefu namna gani ulitapeliwa au mtu alitapeliwa
 
Back
Top Bottom