Umewahi kutapeliwa baadaye ukaishia kujicheka ulivyo Mjinga ukawapa gwala Matapeli?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,461
23,736
Kutapeliwa ni kubaya lakini asilimia 90 ya waliotapeliwa walikaribisha mazingira ya kutapeliwa wakiongozwa na tamaa na kutotaka fikiri. Lakini wapo kadhaa ambao waliibiwa Kitapeli kwa kufuata utu au kujali.

Kuna dogo mmoja aliibiwa pikipiki kipindi flani huko nyuma.aliponiambia jambo hili ikabidi nicheke sana hadi machozi kutoka badala ya kukasirika au kumwonea huruma.Ilikua hivi;

Katika mizunguko yake kuna abiria mlemavu wa mguu(alikua kashikilia gongo la kumsaidia kutembea) alimsimamisha, aliposimama jamaa akaomba apelekwe sehemu fulani hivi, dogo hakusita akamsaidia kumpandisha kwenye piki piki haooo safari ikaanza, katikati ya safari yule abiria akadondosha lile gongo na kumwambia dogo limeanguka bahati mbaya.

Dogo akapaki chombo akamsaidia jamaa kushuka na kumuweka chini (maana jamaa alijidai anasikia maumivu sana ya mguu hawezi hata kusimama) kisha dogo akaanza kutembea fasta kurud nyuma kwenda kuliokota lile gongo, ile anainama kuokota kule mlemavu bandia akawasha pikipiki na kuondoka kwa spidi, basi ndugu yangu chombo kikawa kimeenda kwa staili hiyo dogo akabaki na gongo la jamaa kama kifuta machozi anarudi nalo maskani kinyonge.

Kwa hisani ya Mnyenz
 
Siku moja nipo kariakoo nalishangaa mshikaji mmoja akaniita kwa jina langu na kuanza kunichangamkia sijui nimepotea sana mbona hatuoanani e.t.c niliianza kushangaa kuja kushtuka kuwa mshikaji alisoma tatoo ya jina langu kwenye mkono tulianza kucheka na akawa jamaa yangu wa kuniuzia simu za mishe Kariakoo (Miaka hii nimeachana nazo)
 
hakika hii iliwahi kujikumba na mm kwa kutaka milioni 2 kwa sh 500 sio kamari ila dah ww acha tu. Kutaka kutajirika kwa haraka ni hatari sana
 
Hahaha tuma kwenye hii number jina ni Wajinga Ndio Waliwao afu linamalizia habari za huko vipi mnaendeleaje, jinga kabisa haya majamaa!
 
Uliwatapeli vipi mpaka wakaomba mshirikiane.

Kuna mmoja amenitumia sms kuwa nikitaka kujiunga na Freemanson nimpigie, nampigia apokei nataka nitampeli yeye

Niliwahi fanikiwa mmoja alipostuka akaomba nifanye nae kazi
 
Mdada mmoja nimemuona analia huku akidai pesa zake kuchukuliwa na wenye 'kamali', basi bhana ikabidi nipite pale kwa wale jamaa nimsaidie. Si nikacheza na mie, basi nikaliwa pesa hadi simu yangu, ikabidi niwaombe 'laini' yangu ya simu kisha nikaondoka huku nikiwa nimetapeliwa. Huruma yangu ikaniponza, hadi leo moyo wangu ulishakuwa mgumu kumsaidia nisiyemfahamu.

T
 
Jamaa Kaja anataka Kuku wa kisasa Broilers

Akaja Na Gari kabisa kuwabeba Kama kuku 500

Order yake ipo New Africa Hotel


Baada ya kuchinja Na kutengeneza Kuku 250 akasema acha niwatangulize Hawa kwanza

Akaenda Na Kijana anaehusika Na kufuga kuku ili Utapeli usifanyike

Wengine 250 wakabaki wanatengenezwa

Kufika Kule New Africa kuku walishushwa wote

Jamaa akaagiza wale Vijana wakaleta waliobaki

Dereva akaona Haina Shida kwa Kuwa anarudi Na Kijana wa Mwenye Kuku hivyo hawezi kutapeliwa

Mwenye Kuku akihisi anarudi Na Dereva wa Mteja alieagiza Kuku hivyo sio rahisi kutapeliwa

Kumbe New Africa walihitaji kuku 250 tu

Jamaa alivyo ona Gari imeondoka akaenda kwa Mhasibu wa Hotel akachukua pesa akaPotea

Wale kuleta Kuku wengine 250 Manager wa Hotel akashangaa akasema niliagiza 250 nimemaliza Na nimeshalipia kwa alieniletea


Dereva Kamkunja dogo aliekuwa nae akidhan anajuana Na Mtu aliemkodi akitaka apewe pesa yake ya kusafirisha Kuku Mara mbili kutoka Kawe kwenda New Africa Hotel Mkabala Na Headquatre ya NBC

Yule Dogo mfuga Kuku kamkunja Dereva akidhan anajuana Na Jamaa aliekuja kununua Kuku ili alipwe pesa ya wale Kuku wa awali


Wote wanarejea Na wale Kuku 250 waliojinjwa awamu ya pili lakin bila ya pesa ya wale Kuku wa awamu ya kwanza

Mtaji unakata Na Biashara inaisha Baada ya Muda Yale mabanda ya Kuku yanaoza Na Miti yake inakua kuni Za kupikia

Duniani kuna watu Wana dhambi Sana kutapeli Wanyonge wenzao
 
Natoka posta kwenda Mbezi baada ya mihangaiko ya mjini mida ya saa mbili usiku enzi hizo hakuna Mwendo kasi,mbonge la foleni ubungo mataa mnyama nikaamua kushuka nikojoe nikijua usiku hakuna walinzi nikaenda kwenye ukuta wa TANESCO nikakojoa then akaja jamaa akasema kwanini umekojoa nikambishia mkojo uko wapi akaniambia nitii sheria bila shuruti.

nikakataaa nataka kumtoroka akatoa pingu na kunikamata daah nikajua kwisha habari yangu twende kituoni kufika mbele kidogo akaniuliza una sh ngapi nikuachie nilikuwa na 12500, akachukua 12000 na simu ya tochi akaniacha na jero ili niendelee na safari ya Mbezi aisee mjini shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah nilitapeliwa baada ya kununua simu kariakoo. nilikuwa makini kutouziwa sabuni hivyo baada ya kunipa tu, nikaiweka mfukoni ili asipate muda wa kubadilisha, kumbe ile simu(blackberry) ilikuwa imelockiwa na mtandao wa huko ulaya na haiflashiki mpaka uweke code, jamaa akasepa, mi kila nikiweka line haisomi, kujaribu kuflash kila sehemu nayoenda inakataa ikabidi nitumie kama mp3 player tu. Na ujanja wangu nikabaki nimebung'aa tu kweli mjini shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miaka ya nyuma kuna muuza juice mmoja alinisimamisha kariakoo, akaanza kupiga stori na mim, na mie hua ni mtu wa watu so nilijua jamaa tumewai kukutana mahala, tulipiga stori huku kila saa ananipa glass ya juice ninywe, namie nikajua huyu mwana wa kweli, tulipiga sanaa storii, nilikunywa sanaa juisi siku hio, baadae nikasema mwana ngoja niondoke kama vp tutaonana, huku akinitabasamia mjomba haujanilipa hela ya juisi,

nilipigwa na butwaa, jamaa anadai nimekunywa juisi za elf 7, nikabisha akaita wenzake, wakajaa wakasema sasa wewe si tumekuona hapa umekunywa sana juisi mbona unakua mkorofi, mlipe mwenzio yupo kwenye biashara,,, watu kibao wakanizinguka lipa hela acha ubabe wa kijinga,,, daaah nikampa elf 7 yule fala, alaf siku hio nilikua nna elf 9 mfukoni hela nimeshaipigia hesabu nyingi tu, na wakati ule elf 10 ilikua sawa na laki sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom