MNFUMAKOLE
JF-Expert Member
- Nov 14, 2014
- 1,400
- 1,704
Mkuu! Kuna roho nyingi sana unaziponya kwa kupitia kazi yako njema!! Hakika Mungu atakulipa mara dufu!! maana hakuna aliyemtumikia Mungu akabaki mikono mitupu!! hakuna aliyemtumikia Mungu akapata aibu! Mungu aukumbuke na uzao wako!!"Siku moja nilitoka nje ya jiji tena, nilishangaa nilipokuta umati mkubwa wa watu umekusanyika. Nilipomuuliza mtu mmoja kuna nini alinijibu, 'hujasikia? Kuna mtumwa amemuua mlinzi hivyo amekamatwa na atachapwa hadi afe kwa uhalifu wake. Hata mfalme mwenyewe atakuwepo hapa leo!'
"Watu walikuwa wengi sana wakiwa wamezunguka nguzo ya kumfunga mtuhumiwa anayechapwa. Niliogopa kusogea karibu nisije mwaga sinia langu la keki. Nilipanda juu ya ukuta uliokuwa unajengwa na kuangalia kutoka juu. Siku hiyo ndiyo nilipata bahati ya kumuona Nebkadneza akiwa amepanda gari la kuendeshwa kwa farasi, gari la dhahabu. Sijawahi ona mtu aliyekuwa kapambwa ghali kiasi kile. Kwenye nguo zake kulikuwa dhahabu ikining'inia na nguo za hariri.
"Sikuweza kuona anayechapwa lakini niliweza kusikia kilio chake. Niliwaza inakuwaje mfalme wetu mwema anaruhusu ukatili kama ule na cha kushangaza alikuwa anacheka na kutaniana na watu wengine mashuhuri. Hapo nilifahamu kuwa alikuwa ni katili sana na pia nikaelewa ni kwanini wale watu hufanyishwa kazi ya kujenga ukuta kama wanyama.
"Baada ya mfungwa yule kufa, mwili wake ulitundikwa kwenye nguzo kichwa chini miguu juu ili kila mtu aone. Watu walipopungua nilisogea kuona mwili ule. Kwenye kifua chake niliona tatuu ya nyoka aliyejikunja. Alikuwa ni Haramia!
"Siku niliyokutana tena na Arad Gula alikuwa amebadilika sana. Alikuwa mchangamfu na alinisalimia. 'Tazama mtumwa aliyekuwa unamjua sasa ni mtu huru. Tayari biashara yangu inakua na mke wangu ana furaha. Yeye ni mtu huru pia, mpwa wa bwana wangu. Amenishauri tuhamie mji ambao hakuna mtu anayejua kuwa nimewahi kuwa mtumwa. Anataka watoto wetu wasikue na aibu kuwa baba yao alikuwa mtumwa. Kazi imekuwa msaidizi wangu mkubwa, imenirudishia kujiamini na kuongeza uwezo wangu wa kufanya biashara.'
Nilifurahi kuwa ushauri wangu ulikuwa umemsaidia.
"Siku moja jioni Swasti alinifuata akiwa mwenye wasiwasi sana: 'Bwana wetu ana tatizo, nina wasiwasi juu yake. Miezi kadhaa iliyopita alipoteza pesa nyingi kwenye mchezo wa kamari. Mkulima ambaye humletea nafaka na asali hajamlipa. Pia alikopa pesa sehemu na hajalipa. Watu hao wana hasira juu yake na wameanza kumtishia.'''
"Kwa nini tunajihangaisha na matatizo yake. Sisi si walezi wake,' nilisema bila kufikiri.
'''Kijana mpumbavu! Huelewi chochote. Amekuweka wewe kama dhamana kwa mkopesha pesa. Chini ya sheria, mkopeshaji anaweza kukuchukua na kukuuza. Mimi sielewi cha kufanya, Nana-Naid ni bwana mzuri, hata sielewi kwanini amejiingiza kwenye matata haya?'
"Swasti alikuwa sahihi kabisa kuwa na wasiwasi. Asubuhi moja nilipokuwa naoka mikate mkopesha pesa alifika akiwa na mtu mwingine aliyeitwa Sasi. Yule mtu aliniangalia na kusema kuwa nitafaa.
"Yule mkopesha pesa hakusubiri bwana wangu arudi bali alimwambia Swasti amjulishe kuwa amenichukua. Nilichukuliwa nikiwa na nguo nilizovaa tu na pochi yangu ya pesa kwenye mkanda.
"Nilichukuliwa kama vile mti unaong'olewa toka msituni na kimbunga na kutupwa baharini. Matumaini yangu yalipotea. Kwa mara nyingine kamari na bia ziliniletea matatizo.
"Sasi alikuwa ni mkatili na mtu asiye na mzaha. Alipokuwa ananiongoza kupita jijini nilimueleza kuhusu kazi nzuri niliizomfanyia Nana-Naid na nikamwambia kuwa natumaini kumfanyia kazi nzuri pia. Majibu yake yalikuwa ya kukatisha tamaa kabisa. Alijibu:
"'Sipendi hii kazi na bosi wangu haipendi kata kidogo. Mfalme amemuagiza anitume nikajenge sehemu ya mfereji. Ameniambia ninunue watumwa wengi na wafanye kazi kwa bidii ili iishe haraka. Boh! Mtu anawezaje kumaliza haraka kazi kubwa namna ile?"
"Piga picha ya jangwa lisilo na miti bali vichaka vidogovidogo vya hapa na pale. Jua linawaka hadi maji kwenye mapipa yanakuwa ya moto na hayanyweki. Tena piga picha msururu wa watu wakishuka chini unakochimbwa mfereji na kutoka wamebeba vikapu vizito vya udongo toka asubuhi hadi usiku unapoingia. Vuta picha chakula kimewekwa ndani ya karai refu na tumejipanga tukila kama nguruwe. Kulikuwa hakuna hema wala kitanda cha nyasi. Hayo ndiyo maisha niliyoishi. Pochi yangu ya fedha niliichimbia sehemu nilipoweka alama lakini sikuwa na matumaini iwapo nitakuja kuichimbua.
"Mwanzoni nilifanya kazi kwa bidii lakini kadri miezi ilivyozidi kwenda nilianza kukata tamaa.
Nilipatwa na homa kutokana na joto kali na nikapoteza hamu ya kula. Usiku nilikuwa nikijigeuza geuza tu kwa kukosa usingizi.
"Katika taabu ile nilikumbuka maneno ya Zabado, 'kutojivunja mgongo kwa kutegea kazi'. Hapo nikakumbuka hali niliyomuona nayo kwa mara ya mwisho. Nikaona kuwa mbinu yake haisaidii kitu.
"Nikamkumbuka Haramia na ujeuri wake. Nikawaza iwapo nipambane na kuua. Lakini kumbukumbu ya mwili wake uliojaa damu ikaniambia kuwa mbinu yake haisaidii kitu.
"Mwishowe nikakumbuka mara ya mwisho niliyoonana na Megiddo. Mikono yake ilikuwa imekomaa kwa kufanya kazi kwa bidii lakini uso wake ulikuwa ni wenye furaha sana. Mbinu yake ndiyo ilikuwa bora zaidi.