Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

innocentkirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,752
2,000
Napata wapi hiki kitabu
Kwangu boss vipo
timizamalengo_bookshop_20210419_115956_0.jpg
 

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
748
1,000
"Katika maisha yote ya urafiki wetu sijawahi ona ukiongea kama hivi Bansir" alishangaa Kobbi.
"Miaka yote hiyo sijawahi pata mawazo kama haya". Akajibu Bansir "Toka asubuhi hadi giza linapoingia nimekuwa nikitengeneza magari bora sana. Nilitegemea siku moja Miungu itaona kazi yangu nzuri na kunitunuku mafanikio.

Hawajawahi fanya hivyo na mwishowe nimegundua hawatakuja kufanya hivyo. Natamani kumiliki ardhi na ng'ombe. Kuwa na nguo nzuri na pesa mfukoni.

Niko tayari kufanya kazi kwa nguvu na akili zangu zote ili kupata vitu hivyo. Natamani kazi yangu inilipe ninavyostahili. Kwani tuna mkosi gani? Nikuulize tena! Kwanini hatuna vitu vizuri?"

"Unafikiri najua jibu?" Alijibu Kobbi. "Mimi ni kama wewe tu. Mapato kutokana na kinubi changu yanaisha haraka sana. Muda wote inanibidi niumize akili ili familia yangu isijepatwa na njaa. Pia moyoni mwangu natamani kupata kinubi kikubwa zaidi ili niweze kupiga muziki hasa. Kinubi kama hicho kinaweza kutoa muziki bora ambao hata mfalme hajawahi kuusikia. Na si mfalme tu, hata Miungu watashangazwa na muziki wake mzuri.

"Lakini nawezaje kupata kinubi bora ikiwa sote ni maskini kama watumwa wa mfalme tu? "Sikiliza kengele! Hao wanakuja," akaonyesha kwenye msafara mrefu wa watumwa waliotoka mtoni. Waliokuwa wamebeba maji huku wakiwa nusu uchi, jasho huku wakitembea kwa taabu kutoka mtoni. Walitembea watano watano huku wamebeba mifuko mizito ya ngozi ya mbuzi ikiwa imejaa maji."

"Anayewaongoza ana afya nzuri" akasema Kobbi huku akionyeshea kwa mtu aliyevaa kengele akiongoza mbele ya msafara aliyekuwa hana mzigo wowote. "Bila shaka ni mtu wa maana huko kwao, si unamuona?!" Akaendelea Kobbi.

"Watu wengi tu kwenye huo msafara wamejengeka vizuri" alisema Bansir. "Wako kama sisi tu. Warefu, weupe kutoka kaskazini, weusi kutoka kusini na wa kahawia kutoka nchi za jirani. Wote wanatembea kutoka mtoni hadi bustanini, kwenda na kurudi. Hawategemei furaha yoyote. Usiku kitanda cha nyasi kinawasubiri na chakula chao ni makande. Waonee huruma Kobbi!"

"Unawahurumia lakini mimi sioni tofauti yao na yetu japo tunajiita watu huru," akasema Kobbi.

"Hilo ni kweli Kobbi, ukweli mchungu. Hatujapenda kuishi kama watumwa miaka na miaka. Kufanya kazi kwa bidii bila kufika popote"akasema Bansir kwa unyonge. "Unaonaje na sisi tujue jinsi wenzetu wanavyopata mafanikio? Unaonaje na sisi tuwaige?" Akauliza Kobbi.

"Pengine kuna siri tunaweza kujifunza tukiuliza wale waliofanikiwa," akajibu Bansir kwa matumani.

"Huwezi amini, leo hii hii nimekutana na rafiki yetu wa zamani Arkad" akasema Kobbi. Alikuwa amepanda gari lake la dhahabu. Nilipomuona nikajisemea moyoni, hawezi kuniangalia mtu wa chini hivi, hana tofauti na matajiri wengine. Nikashangaa ananipungia mkono. Watu wote waliona tajiri mkubwa akimsalimia Kobbi mpiga kinubi kwa uchangamfu"
"Inasemekana ndiye tajiri kuliko wote hapa Babiloni" akasema Bansir kwa kustaajabu.

"Ni tajiri hadi inasemekana mfalme huomba msaada wa kifedha kwake" akasema Kobbi. "Tajiri sana" Bansir akamkatiza" ninaogopa siku nikikutana naye kwenye giza naweza kumpora".

"Acha ujinga" akamzodoa Kobbi. "Mtu hatembei na utajiri wake mfukoni. Mifuko huwa mitupu iwapo hakuna namna ya kuijaza tena. Arkad ana kipato ambacho kinafanya mifuko yake itune muda wote, haijalishi ana matumizi ya kiasi gani."

"Kipato, hicho ndiyo muhimu" akasema Bansir kwa furaha. "Natamani kuwa na kipato ambacho kitakuwa kinaingia hata nikisafiri nchi za mbali au nikikaa juu ukutani kama sanamu. Arkad atakuwa anajua jinsi ya kuwa tajiri. Unafikiri anaweza kunielewesha mtu mwenye akili nzito kama mimi?"

"Nafikiri inawezekana, mbona aliweza kumfundisha mtoto wake Nomasir" akajibu Kobbi "nilisika watu wakisema kuwa kijana wake alienda Ninawi, na bila msaada wa baba yake, amekuwa mmoja wa watu matajiri huko Ninawi"

"Kobbi umenipa wazo" akasema Bansir akasema Bansir huku macho yake yaking'aa kama mtu aliyegundua jambo. "Haitupunguzii kitu kupata ushauri kwa rafiki, na Arkad ni rafiki mzuri. Tusijali kuwa mifuko yetu ni mitupu kama kiota cha mwaka jana cha kipanga.

Twende tusiogope. Tumechoka kuwa maskini katikati ya utajiri mwingi. Kama tumedhamiria kuwa watu wa maana na twende kwa Arkad tumuulize cha kufanya ili na sisi tuwe na kipato cha kueleweka."
 

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
748
1,000
Mikono mingi ilinyooshwa, na wa yule mfanyabiashara mzee ukiwemo. Arkad akamuonyeshea ishara kuwa aongee. "Kwa sababu wewe ndiye umetoa wazo, tungependa kusikia kutoka kwako."

"Nitafurahi kuwasimulia hilo," akasema Arkad.
"Nitawasimulia hadithi inayoonyesha ni jinsi gani bahati inaweza mkimbia mtu na jinsi anavyoweza kuiacha iondoke bila kujua na kuishia kupata hasara au majuto."

"Miaka mingi iliyopita nilipokuwa kijana. Nilipokuwa nimetoka tu kuanza kazi na kuoa, baba yangu alinifuata na kunisihi sana kuhusu kuanza kuwekeza. Mtoto wa mmoja wa rafiki zake alikuwa ameona eneo moja kame nje ya kuta za mji. Lilikuwa lipo sehemu ya muinuko kutoka kwenye mfereji wa umwagiliaji hivyo maji hayakuweza kufika.

"Kijana yule aliandaa mpango wa kununua lile eneo na alitarajia kujenga mashine ya kupandisha maji iliyoendeshwa kwa ng'ombe. Akikamilisha hilo, alipanga kuligawa kwenye vishamba vidogovidogo na kuwauzia wakazi wa jiji kwaajili ya kulima bustani.

"Lakini kijana yule hakuwa na pesa za kutosha kufanya yote haya. Kama mimi tu, alikuwa ni kijana mwenye kipato cha kawaida. Baba yake alikuwa na familia kubwa na kipato cha kawaida kama baba yangu tu. Kwa hiyo aliamua kutafuta watu ambao wako tayari kushirikiana naye kwenye huo mradi. Walitakiwa watu kumi na mbili wenye kipato. Kila mmoja alitakiwa kuchangia moja ya kumi ya kipato chake mpaka pale eneo litakapokuwa tayari kwa kuuzwa. Baada ya kuuza kila mmoja atapata faida kulingana na alichowekeza.

'kijana wangu,' aliniambia baba yangu. 'ningependa uanze kuwekeza ungali bado kijana ili hapo baadaye uje kuwa mtu wa maana. Napenda kuona ukifaidika kwa kujifunza kutokana na makosa ya baba yako.'

'''Natamani sana kufanya hivyo baba yangu,' nikajibu.
'''Vema, nashauri ufanye kile nilichopaswa kufanya nilipokuwa na umri kama wako. Kwenye pato lako hakikisha moja ya kumi unawekeza kwenye mradi. Kwa kipato utakachopata kutokana na uwekezaji huo, utakuwa tajiri mkubwa kabla hata ya kufika umri kama wangu.

'''Hayo ni maneno ya hekima sana baba yangu. Natamani sana kuwa tajiri lakini kipato changu kina matumizi mengi. Sitaweza kufanya kama ulivyoshauri ila mimi bado ni kijana, muda bado upo.
'''Hata mimi nilipokuwa na umri kama wako nilifikiri hivyo lakini sasa miaka mingi imepita na sijafanya chochote.'

'''Nyakati zimebadilika mzee wangu, nitajitahidi kuepuka makosa yako.'
''' Mwanangu, fursa ipo mbele yako. Inakupa nafasi ya kuweza kuwa tajiri. Nakuomba usikawie kuitumia. Kesho nenda kamuone kijana wa rafiki yangu na kubaliana naye kuwekeza asilimia kumi ya pato lako kwenye mradi. Nenda kesho bila kuchelewa. Fursa haimsubiri mtu yeyote. Siku zinasonga haraka, usichelewe.

"Pamoja na ushauri mzuri wa baba yangu lakini sikuweza kuufuata. Kulikuwa na mavazi mazuri yaliyoletwa na wafanyabiashara kutoka mashariki. Zilikuwa nguo nzuri sana kwa hiyo nikanunua yangu na ya mke wangu.

"Ningetumia asilimia kumi ya pato langu kuwekeza kwenye ule mradi ningekosa vitu hivi vizuri na vingine vingi. Nilichelewa kufanya maamuzi hadi muda ukapita. Najutia sana jambo hili.

"Mradi ule ulikuja kuleta faida kuliko tulivyofikiria. Hiyo ni hadithi yangu ya jinsi nilivyoacha bahati ipite."

"Kwenye simulizi hii tumeona jinsi bahati inavyomfuata mtu ambaye anatumia fursa," alisema mtu mmoja mweusimweusi kutoka maeneo ya jangwani.
"Ili kujenga utajiri lazima kuwe na mwanzo. Mwanzo unaweza kuwa vipande vichache tu vya dhahabu au fedha ambavyo mtu anatoa toka kwenye pato lake na kuwekeza. Mimi mwenyewe ninamiliki mifugo mingi. Nilianza ufugaji nikiwa mvulana tu. Nilinunua ndama mmoja kwa kipande kimoja cha fedha. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utajiri wangu na ninauthamini sana.

"Kuanza hatua za kwanza za kujenga utajiri ndiyo bahati yenyewe. Hatua hiyo ndiyo huwabadili watu kutoka wale wanaotegemea kipato kutokana na kazi zao kuwa wale wanaopata kipato kutokana na uwekezaji wao.
Wengine kwa bahati nzuri huwekeza wangali bado vijana. Hawa huwaacha mbali wale wanaowekeza umri ukiwa umeenda au wale wasiowekeza kabisa kama baba wa huyu mfanyabiashara.

" Kama rafiki yetu mfanyabiashara angeanza kuwekeza angali kijana pale alipopata fursa leo angebarikiwa kwa utajiri mkubwa sana. Kama rafiki yetu mshona nguo naye akichukua hatua muda huu, utakuwa mwanzo wa mafaniko makubwa sana."

"Asanteni! Nami ningependa kusema." Akasema mtu mmoja kutoka nchi ya mbali. " Mimi ni msiria. Siongei vizuri lugha yenu. Napenda kumbatiza huyu mfanyabiashara jina. Pengine mtaona si vema lakini ningependa nimpe jina.
Sijui kwa lugha yenu mnamuitaje huyu mtu, nikimuita kwa kisiria hamtaelewa. Naomba mniambie, mnamuitaje mtu ambaye kila mara anachelewa na kusita kufanya mambo ambayo yanaweza kuwa na faida kwake?"
"Mhairishaji," ilijibu sauti moja.

"Huyo huyo," alisema muashuru kwa furaha.

"Akiona fursa haitumii, anasema, sasa nina mambo mengi, kwaheri tutaongea baadaye. Fursa hawezi kusubiri mtu goigoi hivyo. Anajua kuwa mtu anayetafuta bahati lazima atachangamkia fursa. Mtu yeyote ambaye hatumii fursa haraka mhairishaji mkubwa kama huyu rafiki yetu mfanyabiashara.

Yule mfanyabishara alisimama na kutoa ishara ya kuinamisha kichwa baada ya watu kulipuka kwa kicheko." Heshima yangu kwa mgeni wetu msiria ambaye hajasita kuongea ukweli'

"Sasa hebu tusikilize simulizi nyingine juu ta fursa iliyopotea. Nani ana simulizi nyingine?" Akauliza Arkad.
 

mkaamweusi

JF-Expert Member
Feb 19, 2013
546
1,000
Watu kama nyinyi Red Giant mnabarikiwa sana. Hiki kitabu nilikipakua huku mwaka jana nikapitia tu list of content nikaacha leo nimekisoma kupitia kwako.

Nasema mnabarikiwa kwasababu kama mimi nashindwa tu kujisomea, je kweli ningeweza kusoma na kutafsiri niandike kwa ajili ya watu?

Shukrani. Big up
Kama mimi tu, Mungu ambariki Huyu Jamaa Red Giant.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
kwa sasa unaweza kukisoma hiki kitabu kikiwa na sura zote ndani ya maktaba App(by pictuss), app ipo playstore. ni bure kusoma vitabu humo.
 

emunenen

Member
Feb 25, 2015
8
95
View attachment 1756326

Muandishi: George S. Clason's, 1926.
Mtafsiri: Pictuss.

Email: pictuspublishers@gmail.com.

©Pictuss2021.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.


UTANGULIZI

YALIYOMO

Mtu aliyetamani dhahabu
Tajiri wa Babiloni
Tiba saba za pochi tupu
Kutana na Mungu wa bahati
Sheria tano za pesa
Mkopesha pesa wa Babiloni
Kuta za Babiloni
Mfanyabiashara ya ngamia wa Babiloni
Mabamba ya vigae
Mtu mwenye bahati zaidi katika Babiloni

Sasa unaweza kukisoma kitabu hiki bure ndani ya maktaba app(by pictuss). Install toka playstore.

MTU ALIYETAMANI DHAHABU
Bansir alikuwa ni mtengenezaji wa magari ya kukokotwa na farasi huko Babiloni. Alikuwa ni mtu ambaye hakuridhika na hali ya maisha yake. Siku hii alikuwa amekaa juu ya ukuta mfupi unaozunguka nyumba yake. Aliangalia kwa huzuni kajumba kake na eneo analofanyia kazi ambapo kulikuwa na gari la farasi ambalo halijaisha kutengenezwa.

Mara kwa mara mke wake alionekana mlangoni. Kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia ilimkumbusha kuwa unga ulikuwa unakaribia kuisha hivyo anatakiwa kufanya kazi gari lile liishe. Agongelee, akate, apige msasa, apige rangi aweke matairi na kupamba kisha alipeleke kwa mteja wake ili apate pesa.

Hata hivyo mwili wake mnene na uliojengeka uliendelea kukaa kizembe juu ya ukuta. Akili yake nzito ilikuwa inahangaika kutatua tatizo ambalo hakuweza kupata jibu lake.

Joto na jua kali la kwenye bonde la mto Efrati lilikuwa likimpiga bila huruma. Matone ya jasho kama shanga yalimtoka kwenye paji la uso. Yalimtiririka mpaka kwenye kifua chake chenye vinyweleo vingi bila yeye mwenyewe kujua wala kutilia maanani.

Mbali na nyumba yake kulikuwa na jumba kubwa la mfalme lililokuwa limezungukwa na ukuta. Pembeni yake kulikuwa na jengo refu lililopakwa rangi, hekalu la Bel(bwana, Marduki). Katikati ya majengo makubwa na ya kifahari namna hiyo, kulikuwa na kajumba kake na tujumba tungine tuchafu zaidi.

Babiloni ulikuwa ni mji wa namna hiyo, mchanganyiko wa ufahari na uchafu. Utajiri mkubwa na umaskini wa kutupwa. Vilichanganyika na kujazana pamoja bila mpango ndani ya ukuta wa jiji.

Nyuma yake, japo hakuangalia kulikuwa na kelele za magari ya kukokotwa na farasi ya watu matajiri yakipita sambamba na wafanyabiashara waliovaa makubazi na ombaomba waliokuwa peku.

Matajiri walilazimika kupaki pembeni kupisha msafara mrefu wa watumwa waliobeba maji kwaajili ya kazi za mfalme. Kila mmoja wao alibeba mfuko mzito wa maji uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya mbuzi. Walikuwa wanayapeleka kwenye bustani zinazoelea za Babiloni.

Bansir alikuwa amezama kwenye mawazo kuhusu shida zake wala hakukazia akili vurugu za mji. Alishtushwa na mlio wa kinubi ambao haukuwa mgeni kwake. Aligeuka na kukutana na uso unaotabasamu wa rafiki yake kipenzi, Kobbi, mwanamuziki.

"Baraka za Miungu ziwe nawe rafiki yangu" alisalimia Kobbi

"Inaonekana Miungu ni wema sana kwako hadi huna haja ya kufanya kazi! Nafurahia bahati yako maana na mimi naweza kufaidika nayo. Bila shaka mifuko yako imetuna, vinginevyo ungekuwa unapiga kazi saa hizi. Nikopeshe shekeli mbili, nitakulipa jioni baada ya karamu ya matajiri"

"Yaani ningekuwa na shekeli mbili nisingekukopesha" akajibu Bansir kwa unyonge. "Nisingekopesha mtu yeyote, hata wewe nisingekukopesha. Hizo ndizo zingekuwa kila kitu kwangu na mtu hawezi kukopesha kila kitu alichonacho, hata kwa rafiki yake kipenzi"
"Unasema!" Akashangaa Kobbi. "Inamaana hauna hata shekeli moja mfukoni lakini umekaa juu ya ukuta kama sanamu. Kwanini usimalizie hilo gari? Sasa utapataje mahitaji yako? Siyo kwa mtindo huo rafiki yangu. Nguvu zako za siku zote ziko wapi? Kuna kitu kimekukwaza, Miungu imekuletea matatizo?"

"Itakuwa ni mateso toka kwa Miungu" alikubali Bansir. "Ilianza kama ndoto, ndoto isiyo na maana. Ndani ya ndoto nilikuwa ni mtu wa maana. Kwenye mkanda wangu wa kiunoni ilining'inia pochi nzuri iliyojaa pesa. Kulikuwa na pesa nyingi kiasi kwamba ningeweza kugawia ombaomba bila kujali kuishiwa; nilikuwa na dhahabu zilizonifanya nijihisi salama hata kwa siku za usoni na wala sikuogopa kutumia pesa. Nilikuwa ni mtu niliyeridhika sana. Usingenijua kama ni mtu mwenye bidii ya kazi wala mke wangu usingemtambua. Uso wake haukuwa na makunyanzi na uling'ara kwa furaha, alikuwa mwanamwali tena, kama alivyokuwa mwanzo nilipomuoa."

"Ndoto tamu kweli" akasema Kobbi. "Lakini kwanini ndoto tamu hivyo ikufanye ukae juu ya ukuta kama sanamu?"

"Hilo ndilo swali! Nilipoamka na kukumbuka jinsi mifuko yangu ilivyo mitupu, hisia za uasi na kutojali zikaniingia. Ngoja tuongelee hilo suala pamoja. Kama mabaharia wasemavyo, mimi na wewe tupo ndani ya mtumbwi mmoja. Wakati tukiwa wavulana tulijifunza pamoja kwa kuhani. Tulipokuwa vijana tulifurahia maisha pamoja. Na katika utu uzima tumekuwa marafiki wa karibu.

Tumekuwa watu wa kuridhika. Tumeridhika kufanya kazi kwa masaa mengi na tunatumia mapato yetu kwa uhuru. Tumepata pesa nyingi kwa miaka yote tuliyofanya kazi lakini furaha ya utajiri tunaipata ndotoni tu. Bah! Tunatofauti gani na kondoo wasioelewa kitu? Tunaishi kwenye mji tajiri zaidi duniani. Wasafiri wanasema hakuna mji unaofanana nao kwa utajiri lakini sisi hatuna kitu. Baada ya kufanya kazi ngumu kwa nusu ya maisha yangu, mimi, wewe na rafiki zetu wengine, hatuna kitu,'

"Naweza kuazima shekeli mbili na nitakulipa jioni? Nilijibuje? Nilisema kuwa hii hapa? Hapana, nilikubali kuwa mifuko yangu haina kitu kama yako tu."

"Shida yetu nini? Kwanini hatuwezi kuwa na fedha na dhahabu zaidi ya zinazotosha nguo na chakula tu?"

"Fikiria kuhusu wana wetu" aliendelea Bansir. "Je, hawafuati hatua zetu? Si kwamba wao, familia zao, na familia za watoto wao wataishi katikati ya dhahabu na utajiri kama sisi lakini wataridhika na kunywa maziwa mgando ya mbuzi na uji tu
Very simple and practical lessons about saving money and growing wealth There is a copy here
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom