Umewahi kumwona Mungu?? Usihangaike kwenda mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kumwona Mungu?? Usihangaike kwenda mbali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Nov 28, 2008.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimepewa hadithi hii na jamaa yangu anayefanya kazi ya kuwahudumia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi (orphaned and vulnerable children, OVC) katika mji mmoja hapa Tz. Watu wengi wanaowahudumia ni wahanga wa VVU/UKIMWI (victims of HIV/AIDS). Siku moja walimtembelea bibi mmoja mzee mwenye umri wa karibia miaka 70. Anaishi na binti yake mmoja mwenye VVU/UKIMWI na wajukuu karibia 10. Watoto wake wengine 5 walishakufa kutokana na VVU/UKIMWI. Huyo mgonjwa alikuwa anaumwa sana na anatoa harufu kali. Waliamua kumpeleka zahanati ambapo iligundulika kuwa sehemu zake nyeti zimeoza. Alipewa huduma kwa gharama za shirikia (la huyo jamaa yangu) na kuanzishiwa dawa za kurefusha maisha. Kwa sasa hali yake ni nzuri kiasi.

  Tatizo jingine ni kuwa hii familia haikuwa na nyumba. Nyumba yao ya mbavu za mbwa ilianguka na walikuwa wanalala nchini ya mti karibu na ilipokuwa nyumba yao. Hawakuwa na uhakika wa chakula, walitegemea wajukuu wawili wa huyo bibi (ambao walikuwa darasa la 7) wafanye vibarua na kupata pesa ya unga na dagaa. Maisha yalikuwa magumu kweli kweli.

  Shirikia liliamua kuwajengea nyumba ndogo ya bati na kuta za udongo. Pia walianza kuwapatia chakula kila wiki. Na yule bibi alipewa godoro. Wakati anakabidhiwa vitu hivyo, bibi alilia sana. Akawambiwa wanfayakazi wa lile shirika kuwa, ameishi umri wake wote, hakuwahi kula chakula kizuri na mbali ya hayo hakujua kuwa siku moja anaweza kulalia godoro. Yule rafiki yangu naye alitokwa na machozi na kupata hisia za ajabu. Anasema kuwa kwa muda mfupi tu alijihisi kama alimwona Mungu amezungukwa na malaika.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mauza uza tu hayo ,hivi wamewahi kuenda kanisani hao,kwenye nyumba yake
   
 3. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wapi imeandikwa kuwa kanisani ndiyo nyumba yake?
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hakuna ilipoandikwa nadhani ni mawazo yake tu ambayo kayatoa katika ufahamu wake binafsi
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nyumba yake nani ? Wacheni kuhukumu yaani mawazo yenu yanajua kusoma tu hayawezi kufikiri na kupima na kuona ,yaani hayana uwezo wa mawazo ya kuhoji ,nyie naona mkikamatwa basi hakimu hana tabu atawafunga tu. ,Yaani mnashindwa hata kuifahamu senteso ipo kwenye tungo gani ,dah hii hasala ndio maana mabenki yanaibiwa kwa mamilioni kutokana na watu dizaini zenu .
   
 6. S

  Scorpion Member

  #6
  Nov 29, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dark City,

  Whatever direction this discussion takes, the story is very inspiring and worth sharing. Tujifunze kuishi hivyo, kama watoto wa Mungu.

  Thanks.
   
 7. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwiba, hiyo senteso (Sentesi) hapo juu ni tata!!!!!!!! Weka sawa tuendelee, kulalama hakutusaidii!!!!!

  Ukiacha hayo, Dark City hiyo story inachoma sana!!!!! Yafanana na yule mama wa kisomali aliyeshuhudia mtotoe akiliwa na tai huku yeye akiwa hana nguvu kutokana na njaa kwa kutokuwa amekula mwezi usheee!!!
   
 8. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu yuko kila mahali, sio lazima atutokee kama kichaka cha moto as was the case with moses. Anaonekana kwenye mambo mengi tu sema saa nyingine tuko too busy to notice. That unexpected smile from a little child, those encouraging words from a stranger. Nilikua uchi ukanivisha, nilikua na njaa, nilikua na kiu, nilikua kifungoni ukaja kunitembelea....
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  These are the words I just wished I could hear from thinkers in JF. Ni ajabu sana watu bado wanamtafuta Mungu kwenye nyumba za ibada. Amini usiamini huko hayupo hata ukienda mara 1000 kwa siku. But just touching broken hearts makes you feel the real God. Thanks to those who can dare.
   
 10. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tafsiri ya kanisa uanijua? Tafuta tafsiri ya kanisa kwanza ndo uulize hivi!
   
 11. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The topic of the thread is so enticing!
  Its a good work they are doing and God will reward them abundantly!
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli Nkamangi hapo mwisho hapo pamenikuna. L. Masha kaenda kuwatembelea kina BPM na Yona, atakuwa rewarded ama! Basi anmi naenda Keko kesho kuwatembelea BPM na mwenzie
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Bado tu mnaharibu lugha.
   
 14. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Eeka Mangi unajua Bwana Yesu alisema hakuja duniani kwa ajili ya wenye haki bali kwa ajili ya waliopotea.... Kuhusu Masha na Mramba et al, hapo pagumu lakini,huwezi jua ndio maana ni Mungu, we can't figure him all out. Nndumi naarafumwe!!
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu Dark city, hiyo si hadithi,ila ni kweli hiyo familia ipo kijiji fulani ndani ya Tanzania yetu na kama unataka nikutajie kijiji hicho kipo wapi na familia hiyo inaitwaje nitafanya hivyo. Ila ni-pm. Ukifika kwenye hiyo familia utamwona Mungu. This is a true living thing, I have seen it.
   
 16. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  I don't think to be a thinker one has to think as you do. Kama Mungu yuko mahali pote si hata humo kwenye nyumba za ibada yumo au mahali pote 'excludes' nyumba za ibada?

  Maana ya kwenda kanisani, sinagogi au msikiti ni hasa kukutana as a believing community. Nyumba hizo hazina maana kama hakuna community inayoamini. Na ni katika and through the community that we can share, be open to one another and get in touch with ourselves and people around us.

  Unacho'propose' wewe ni individualism au anti-God mentality. Kwa hiyo, hizo nyumba zinatukutanisha na kama hakuna watu wanaoenda humo hazitakuwa nyumba za sala bali majengo au maghala fulani.

  Suppose kila mtu angeamua kusali nyumbani kwake na kivyake si hata ingekuwa shida kujua nani ana shida na asaidiweje? Na maana ya kusali pamoja ni pamoja na kusaidiana kwa ushauri au kwa vitu?

  Tunapotaka kushirikiana ni lazima tupate njia inayotuwezesha kuonana na kushauriana. Na kama kila mmoja angeamua afanye mambo kivyake hata tusingekuwa tunaoa au kuolewa.

  Ungemwoa au kuolewa na nani bila kujenga 'familiality' fulani. Na once binadamu wanaanza kuwa pamoja wana'form' institutions zinazowasaidia ku'operate' mambo yao vizuri kwa kuwa na 'rules of exclusion and inclusion'. i.e. Nani awe na nani asiwe.

  Hizi rules ni 'natural'. Mfano, nyumbani kwako una 'rules of inclusion na exclusion'. Una namba fulani ya vitanda, meza, viti, vyumba, budget ya chakula, malazi, mavazi etc. kulingana na size ya familia yako.

  Hali kadhalika mnapokutanika kama jumuiya kubwa 'rules' hizi zinaongezeka kutokana na majukumu mnayokuwa nayo. Hivyo, ni muhimu kutafakari vizuri maana ya kusali pamoja hata kama Mungu yupo kila mahali.

  Yesu alisema: "Mnapokusanyika wawili, watatu... kwa jina langu Mungu yupo kati yenu." Yaani, wale wanaotenda na kuishi jinsi Mungu anavyowataka waishi, basi hao wana Mungu ndani mwao na haiwezekani kufanya hivyo kwa'kuji exclude' au kujitenga na wengine.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Nov 30, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Malaika ni viumbe imaginary na wala hakuna ajuaye waina sura gani. Yeye alijuaje kama hao alioona kweli walikuwa malaika?
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Inategemea unaamini nini. Kwa sababu hata Mungu ambaye karibia kila mtu duniani anamwongelea na wengine kumwamini kuwa ndiye aliyewaumba hakuna mtu ambaye aliwahi kumwona.
   
 19. S

  Stone Town Senior Member

  #19
  Dec 1, 2008
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa ufupi kwa mujibu nilivyofahamu mimi hiyo story ni kuwa mambo kama hayo yanakufanya uweze kumuona Mungu ila sio kumuona kwa jicho lako lakini ile hali halisi ya mazingira aliokutwa nayo huyo bibi na mjukuu wake kwa kweli inatia huzuni sana na bila ya shaka watu wa aina hiyo wapo wengi na hili linatokana na kuwa kukosekana ujirani mwema na kukosekana imani miongoni mwetu maana kama tuna imani thabiti bila ya shaka hatuwezi kumuacha mtu afikie hatua kama hiyo bila ya kusaidiwa kwani wapo watu wengi wenye kumudu kumsaidia lakini ukosefu wa imani na roho mbaya tuanfikia hapa tulipo na kuwaacha wazee wakiahngaika na maisha.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu, you just hit a nail on its head! Great views.
   
Loading...