Umewahi kukutana na wababe wa familia/ukoo na manyanyaso yao?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,697
huyu utamkuta anapesa nyingi kuliko familia au ukoo wote...

Maamuzi yote yanayofanyika bila kuhusishwa huwa ni batili...

anachokisema yeye hakiwezi kupingwa adharani kwa wanandugu au familia kuogopa kukosa misaada...

huwa wako radhi kuhujumu wanafamilia wanaojikongoja kujikwamua kiuchumi kwa kuhofia nafasi yake ktk ktk familia au ukoo...

Msaada wowote atakaotoa sio ili ufanikiwe kabisa ila ni ili upate nafuu na kuendelea kuwa ombaomba...

Huyu huwa na vibaraka na wapelelezi ndani ya ukoo au familia ukimsema vibaya au ukipiga hatua yoyote taarifa zote humfikia...

Hata kama alikusaidia nauli ukakomaa kwa juhudi zako ukatoboa ukoo wote utaaminishwa ni juhudi za yule kigogo wa familia...

huyu ndio mbabe wa familia/ukoo ni ni maarufu katika makabila mengi nchini.
Umewahi kukutana na mbabe wa namna hii?

Usiombe akawa ni mwanamke...
 
Mkuu dah umenikumbusha mbali sana.
Aisee pesa hii nyie iacheni iitwe pesa maana nyeusi inaweza geuka nyeupe na nyeupe nyeusi as long as mwenye pesa kasema iwe hivyo.
 
mmmmh! ndio maana sisi kule kwetu uchagani (kwa wachaga) mtoto akiwa na pesa nyingi baba na mama yake mzazi utasikia wanamwamkia "SHIKAMOO MANANGU!" hahahaahahahahahaha
Ngoja nisubirie kupopolewa mawe na watani zangu hahahahahah
 
No one can make you to be you but can help you to be you. Ni kupambana tu hakuna mchawi mwingine zaidi ya uzembe kwenye maisha
kuna mdau mbabe wao alikuwa muajiri mkuu hoteli flani kubwa jijini, anaajiri kihalali na kwa madili watu baki ila alipoenda yeye akamwambia kuna banda anataka kujenga shamba amnunulie unga na dagaa ili awe anamlindia...wakati anasema haya pembeni yupo mdau anafanyiwa magumashi ya kukamata fursa ambayo yeye anaambiwa aende shambani.

haya mambo yapo kwenye jamii mkuu. Ila kikubwa ni Self relience na sio kutegemea mtu yoyote yule ktk kutoka.
 
mmmmh! ndio maana sisi kule kwetu uchagani (kwa wachaga) mtoto akiwa na pesa nyingi baba na mama yake mzazi utasikia wanamwamkia "SHIKAMOO MANANGU!" hahahaahahahahahaha
Ngoja nisubirie kupopolewa mawe na watani zangu hahahahahah
Uchagani seemu gani mkuu ? Sijawahi sikia au kuona hii
 
Shida inakuja Wanapofulia ni lawama kwa kila aliekula shilingi yake, Wanaishi maisha ya kujificha ficha kama Nguchiro, Wanapokea ushauri kutoka hata kwa Watoto wale wanaoita Mma, Wakati wa Ibada ndo wanakuwa mstari wa mbele kupokea Wokovu, Wanakuwa ni washauri wazuri katika kubana Matumizi..,
 
Sehemu yoyote lazima kuwe na mtemi wake ila mimi hata uwe na pesa kiasi gani huwezi kunipelekapeleka tu kama gari bovu lazima uwe na nidhamu
 
Daa! aisee,, hii habit ni mbaya sana,kuna rafiki yangu anasuffer ktk hili,yaani mkubwa wa familia yao ni dada yao wa kwanza,aliachiwa kiwanja cha familia akitunze kama kuwahifadhi tu yeye na mumewe lakn dada huyu kajimilikisha na hataki kupaachia na anaogopwa na wanaume wote(wadogo zake) anasema kama watataka achie eneo basi apewe milioni 30 tena cash na sio za kutoka ktk kuuza eneo hilo na kama mtu atatokea kudai kisheria atapambana nae kufa kupona.
 
Ukiona kwenye ukoo wenu kuna mtu wa hivyo basi jua uo ukoo wenu ni dhaifu sisi kwetu hakuna ayo mambo kuna wanaume wamekaa wanaheshimiana
ni hulka ya mwanadamu kutaka kutawala wenzake hasa kunapokuwa na gap kubwa kiuchumi na wengine waliobaki wakiwa na mentality za utegemezi .

Hata US katawala dunia nzima inabidi uwe na roho ya NK au iran ili uepuke mkono wake au uwe na uwezo wa kujisimamia kiuchumi kama Russia na China.

hii dhana inashuka chini hadi kwenye level ya familia na koo.
 
Haahahh kuna jamaa nilifikia kwake nikitafuta shule
Badaye nikapata makongo nikahamia hostel
Lakini JAMAA KAAMINISHA WATU NDO ALINISOMESHA...
boys kweli MTU hawezi hata kumsaidia baba yake mzazi anakomaa eti amenisomesha
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom