Umewahi kukutana na swali hili kwa mpenzi wako, "eti wewe ni kabila gani?"

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,249
1,340
Habari wana JF,

Hivi umewahi kukutana na swali hilo toka kwa mpenzio? Na je pana changamoto yoyote kati ya wawili wapendanao sababu ya kabila la mmoja wao?

Tushirikishane uzoefu na kama uko miongoni mwa walokutwa na kadhia hiyo, tushirikishe namna ulivyokabiliana nayo.
 
Mi nliulizwa bhana. Nikamwambia mie Mmasai OG. Ghafla ikaingia mada ya ndoa za mke zaidi ya mmoja.. Haikuwa rahisi sana kumaliza hiyo topic.. Swala la kabila si la kubeza. Kuna baadhi ya kabila zina tabia fulani fulani ambazo zipo sana. Intermarriage is OK Ila kuna kabila hazipo compatible.. Mtaishia kutwangana.
 
Kukutana na swali la kabila kutoka kwa mpenzi ni lazima na mpenzi kutaka kufahamu kabila sio mbaya

Na binafsi kabila halijawahi kuwa changamoto kabisa katika mahusiano yangu
Suala la kabila la huyo mpenzio halijawahi kuwa changamoto kwako .... ama kabila lolote halitakuwa kikwazo ktk suala la nani apaswaye kuwa mpenzio?
 
Mi nliulizwa bhana. Nikamwambia mie Mmasai OG. Ghafla ikaingia mada ya ndoa za mke zaidi ya mmoja.. Haikuwa rahisi sana kumaliza hiyo topic.. Swala la kabila si la kubeza. Kuna baadhi ya kabila zina tabia fulani fulani ambazo zipo sana. Intermarriage is OK Ila kuna kabila hazipo compatible.. Mtaishia kutwangana.
Takwenya elayeni
 
Kuna siku nilienda na binti nyumbani alipoondoka mama akaanza "Yule mpenzi wako" mimi "Hapana" akaendelea "Anaongea kama mtu wa pwani" nikajibu "Ndiyo anatokea Tanga" akasema "Mh mbona ana many0ny0 makubwa sana? Mimi maswala ya mjukuu wangu kupaliwa na maziwa sitaki, huyo kaka yako kaja na mwanamke (naye anatokea Tanga) ana miguu mirefu myembamba kama kuni, sijui mnatoa wapi wanawake zenu"

Mimi sikujibu kwakua nilishasema siyo mpenzi wangu, baadaye baba akaniambia "Mama yenu hataki uoe mtu kutoka Tanga kwa sababu kuna mjomba wenu hadi leo hatujui yuko Tanga sehemu gani mara ya mwisho kutuma barua ilikua 98 na alisema ameoa na ana watoto na hataki kurudi nyumbani"

Of course kabila lina nafasi yake, haswa kwa wazazi.
 
Mimi niliulizwa na demu wa Kihaya we kabila gani? nikajibu mi Mchaga, kaniambia mbona hufananii na Mchaga? nikamuuliza kwani Wachaga wanafananiaje? akashindwa kunijibu
Ila kuuliza nauliza ili kufahamu kwao basi , makabila hayana umuhimu kama mpenzi wako ni mtu reasonable, maana makabila yote yana mila za kishenzi
 
Kuna siku nilienda na binti nyumbani alipoondoka mama akaanza "Yule mpenzi wako" mimi "Hapana" akaendelea "Anaongea kama mtu wa pwani" nikajibu "Ndiyo anatokea Tanga" akasema "Mh mbona ana many0ny0 makubwa sana? Mimi maswala ya mjukuu wangu kupaliwa na maziwa sitaki, huyo kaka yako kaja na mwanamke (naye anatokea Tanga) ana miguu mirefu myembamba kama kuni, sijui mnatoa wapi wanawake zenu"

Mimi sikujibu kwakua nilishasema siyo mpenzi wangu, baadaye baba akaniambia "Mama yenu hataki uoe mtu kutoka Tanga kwa sababu kuna mjomba wenu hadi leo hatujui yuko Tanga sehemu gani mara ya mwisho kutuma barua ilikua 98 na alisema ameoa na ana watoto na hataki kurudi nyumbani"

Of course kabila lina nafasi yake, haswa kwa wazazi.
Mama zetu kwa kuwachambua utafikiri wao mamiss world.

Utaskia yaani ole wako uniletee mwanamke kucheka hajui kulia hawezi. Mtumiane huko ukileta leta mwanamke wa kueleweka
 
Kuna siku nilienda na binti nyumbani alipoondoka mama akaanza "Yule mpenzi wako" mimi "Hapana" akaendelea "Anaongea kama mtu wa pwani" nikajibu "Ndiyo anatokea Tanga" akasema "Mh mbona ana many0ny0 makubwa sana? Mimi maswala ya mjukuu wangu kupaliwa na maziwa sitaki, huyo kaka yako kaja na mwanamke (naye anatokea Tanga) ana miguu mirefu myembamba kama kuni, sijui mnatoa wapi wanawake zenu"

Mimi sikujibu kwakua nilishasema siyo mpenzi wangu, baadaye baba akaniambia "Mama yenu hataki uoe mtu kutoka Tanga kwa sababu kuna mjomba wenu hadi leo hatujui yuko Tanga sehemu gani mara ya mwisho kutuma barua ilikua 98 na alisema ameoa na ana watoto na hataki kurudi nyumbani"

Of course kabila lina nafasi yake, haswa kwa wazazi.
Je changamoto hiyo ya kabila either lako ama la mpenzio kama unae ikikutokea ama kwa wazazi wako kuuliza au kuulizwa wewe na mpenzio, utaikabiri vipi?
 
Habari wana Jf ....

Hivi umewahi kukutana na swali hilo toka kwa mpenzio .... ?

Na je pana changamoto yoyote kati ya wawili wapendanao sababu ya kabila la mmoja wao .... ?

Tushirikishane uzoefu na kama uko miongoni mwa walokutwa na kadhia hiyo, tushirikishe namna ulivyokabiliana nayo ....
Nilimjibu tu 'unaniuliza kabila yangu unataka kutambika?'
 
Mimi nilimjibu usiniulize mambo ya kijinga, ukabila hauna nafasi yoyote katika maisha yangu,wala mimi sitaki kujua kabila lako. Hadi leo hajaniuliza.
Ni kipindi gani kishapita tangu jibu hilo litolewe na pana "mutual understanding" kati yenu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom