Umewahi kukutana na mwanamke ambaye amewahi kuwa na msululu wa wanaume wanyanyasaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kukutana na mwanamke ambaye amewahi kuwa na msululu wa wanaume wanyanyasaji?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 19, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Imesemwa sana na itaendelea kusemwa kuhusu kutojiamini kwenye uhusiano. Wataalamu wanaamini kwamba, watu wasiojiamini, wanakuwa na matatizo makubwa na magumu au mabaya zaidi wanapokuwa kwenye uhusiano, kuliko kwenye maeneo mengine ya kimaisha.

  Kwa wanawake wanakabiliwa na adhabu mbili kwenye jambo hili. Kutokana na mfumo dume, mwanamke anakuwa tayari amepoteza kujiamini anapokuwa mbele ya mwanamume. Wakati mwingine hata kama alikuwa akijiamini hapo kabla, yaani kabla hajaingia kwenye uhusiano.

  Kwenye uhusiano wa kifujaji, kama mwanamume ndiye mfujaji, mara nyingi sana, mwanamke aliye kwenye uhusiano huo, anakuwa ni yule mwenye kupenda kujibandikiza kama kupe, ambaye anaamini kuwa hawezi kuishi bila mume huyo. Anapigwa, analaliwa nje, anadhalilishwa kwa njia mbalimbali, lakini ameng'ang'ania.

  Ni mara chache sana kukuta mwanamke asiye na utegemezi, yaani asiye tayari kumng'ang'ania mtu, kuolewa na mume mnyanyasaji. Umewahi kukutana na mwanamke ambaye amewahi kuwa na msululu wa wanaume wanyanyasaji? Anaishia kubadili kutoka kwa mnyanyasaji wa kwanza, wa pili na kuendelea. Hajui kwamba, anakutana na wanaume hawa kwa sababu ya kutojiamini kwake.

  Mwanamke anayejiamini hana hofu ya kumwacha mwanamume mnyanyasaji. Anajua kwamba hastahili kufanyiwa vile. Anatengeneza nguvu ya kihisia yake mwenyewe na anakuwa barabara, ngangari hata akiwa peke yake. Mwanamke anayejiamini hahitaji kukubalika kwa wengine kama ni ajenda yake ya kila siku.

  Kutojiamini au kuhisi kuwa huko salama hadi wengine wawepo au wathibitishe, kunaweza kusababisha madhara makubwa, hasa kama hujui kutojiamini maana yake nini. Watu wengi wasiojiamini wanapenda kutoa visingizio wanapopata matatizo, wakiwa hawajui kwamba wao wenyewe ndiyo chimbuko la matatizo waliyo nayo. Jiambie kwamba, umekamilika na usitake mume akukamilishe, kwani hataweza.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa. Kutojiamini hufanya mtu ang'ang'anie mahusiano ambayo kwa namna moja au nyingne yana manyanyaso ndani yake. Kuna mdada mzuri namfahamu alikaa muda mrefu bila kuwa na mpenzi. Sasahv yupo kwenye mahusiano ambayo upendo umeelemea upande mmoja. Hajiamini, anahisi akitoka hapo hatapata mtu.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  ...malizia
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmmh, ya kweli haya?!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante Baba yangu
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  tayari TANMO. Ahsante kwa kunikumbusha.
   
 7. Loly

  Loly JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Hakuna kitu nachukia duniani kama mwanamke asiyejiamini, najiamini am a SUPER LADY nasibabaishwi na mwanaume yeyote kwa sababu yoyote hakuna kinachonishinda kwenye maisha yangu wamuhimu ni mimi mwenyewe ndio maswala mengine yanafuatia, nawashanga sana wanawake wanaonyenyekea wanaume na ndo haohao wanaokutana na hiyo mifumo dume,
  ushauri wa bure kwa wanawake ukiona mwanaume haeleweki anakunyanyasa anakutenda achana nae haraka wala usikubali kupigwa na mwanaume, wanaume wastarabu wa maana wamejaa kibao na hata siku moja mwanamke usijipe moyo kwa neno kama nitaangaika na wanaume mpaka lini acha tuu nivumilie
  ukishafikia hapo jua umekwisha shost jua umeyakubali mateso nakuyakumbatia, kwanini usiwe huru mwenye amani na furaha ukubali machangu kisa? Toka haraka fungua akili yako wewe mama, binti, msichanana na wengine wote
  mwanamke wakisasa ndani ya kizazi hiki sio wa kuvumilia tabu wala mateso.
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  .....hiii sredi tamu sana...nitarudi kuchangia muda si mrefu...
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Loly,hayo maneno yako yanaashiria hujiamini kabisa!Mtambuzi umenikumbusha mbali kweli,yani we acha tu,nikikumbuka Jitambue moyo unasikitika sana!
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  aiseeee....maneno juu ya msitari bana, swadaktaaaaaaaaaaa!

  lakini swali ninalojiuliza? naomba muwe wawazi kabisa kuchangia...
  kwanini kina dada wengi ni wagumu kujiamini?????
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  @ Eiyer............. Jitambue linahitajika sana hasa kwa hiki kizazi cha DOT COM..................... Kuna juhudi za makusudi nazifanya ili kulirejesha, na inshaallah ipo siku utaliona mitaani.....................
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Loly, achana na Eiyer, wewe unaonekana ni ngangari na unastahili kujiita SUPER LADY........................
   
Loading...