Umewahi kujiuliza kwanini biashara ya vyuo vikuu imeshamiri Tanzania?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Hili ni swali muhimu sana kwa wadau wa elimu nchini...Unapojibu hapa utaelewa ni vita vya namna gani Rais wa JMT anavyotaka kupamabana navyo...

miaka ipatayo hamsini ujinga ni mojawapo ya maadui watatu waliotamkwa kulikabili taifa hili.

Leo hii Magufuli anaamua kupamabana na ujinga wa kisasa....

Ujinga wa kisasa ni pamoja na taasisi zetu za kielimu kuingiza vihiyo na vilaza kwenye soko la ajira halafu baadaye wanageuka walalamishi wa kushindwa kushindana kiajira,

Tuna wanasheria wasioelewa mikataba ya kimataifa halafu tinataka vilaza waachwe tu wapite...ha ha ha....

Gesi ikichimbwa na wataalamu kutoka nje tunalialia tu kwa kuwa hatuna uwezo huo kwa ku wa chujio la vilaza lilikuwa kimeharibika.

Huwezi kuwa na wasomi weengi wa level ya degree kwenye taifa lenye utapiamlo na udumavu wa akili kwa kiwango cha karibu nusu ya watoto wetu.

Hii biashara ya elimu itatutokea puani!!!

Wale wazungusha mikono njooni na maana ya neno Elimu Elimu Elimu mtueleze mlimaanisha Elimu hii ya kuwakweza vilaza??
 
Chadema hakuna msomi pale ndio maana wanatetea vilaza wenzao...mbowe.mnyika.sugu.lema.profesa j wote ni vilaza form four failure
 
Wakati Mhe. Fulani (toka Mkoani Iringa) akiwa Waziri wa Elimu ya Juu ndipo kosa lilifanyika ili ku-boost chuo kikuu binafsi toka mkoani mwake. Ziliandaliwa programu kemkem chuoni hapo (ilihali vyuo vikuu vya umma) vilikuwa na uwezo wa kuendesha programu hizo. Bongo tambarare.
 
Watu wanapiga honors kirahisi sana siku hizi halafu ukija kwenye kazi hakuna ubunifu wowowte ...tunaishia kuimport vitu kutoka china na dubai
Swala la importation sio la mtu binafsi mkuu. Hili ni la nature ya binadamu wa tanzania. Ukiwa na uwezo bila ya kuwa na miundombinu unakuwa hujafanya lolote. Ifike atua kuwe na sehemu za reshearch center kwa ajili ya inovation kama mataifa mengine yalivyo fanya mfano japan. Lasivyo hakuna mabadiliko
 
Hivi kilaza sio yule aliyeisababishia serikali iliyopita hasara kwa kuwalipa wachina meli yao ya uvuvi.
 
sawa mkuu, ila elimu yetu imechakachuliwa sana,
Hivi mkuu nani anahusika na usajili wa hivi byuo vikuu vingi kama njugu?
Ni ule mfumo ulioyumba na sasa uko kwenye marekebisho makubwa...ambayo yanaumiza wengi.

DAWA YA JIPU NI KUKAMULIWA TU INGAWA LINAUMA
 
Back
Top Bottom