Umewahi kujiuliza, ikiwa ni CCM wanawatumia Polisi, au ni Polisi wanawatumia CCM?

Ccm inawatumia Polisi.. Kumbuka hiyo ndyo fimbo yao, RPC yupo chini ya mwenyekiti wa mkoa Wa CCM. OCD yupo chini ya mwenykt wa ccm Wilaya
 
Hili suala la Hamza limenifanya nijiulize swali hili, hasa niliposikiliza kauli za viongozi wa Polisi kama IGP Sirro na viongozi wa CCM kama Mkuu wa Mkoa wa Dar Amos Makala.

Je, inawezekana kwamba tofauti na tunavyofikiria, kwamba CCM wanawatumia Polisi, ukweli ni kwamba ni Polisi wanaowatumia CCM na ndio maana wanafanya mabo mengi sana yasiyokubalika na wananchi bila hatua zozote kuchukuliwa dhidi yao, au hata serikali ya CCM kulifumua upya jeshi la polisi kama inavyopendekezwa na wengi?

Kwa mfano, katika suala la Hamza, tungetarajia Raisi Samia aunde chombo huru kuchunguza na kupata ukweli - lakini tofauti na hilo, anaagiza Polisi haohao ambao wamekuwa wakimshutumu Hamza na familia yake ndio wafanye uchunguzi. Sasa hapa nani anamtumia nani, kama sio Polisi wanaitumia serikali ya CCM katika mambo yao?

Inawezekana pia CCM hawajui kwamba wao ndio wanaotumiwa na Polisi, huku wakiaminishwa na Polisi kwamba wao ndio wanawatumia Polisi!

Inawezekana kwamba kitendo cha Polisi kutumika na CCM dhidi ya wanasiasa wa upinzani ni fadhira ndogo sana inayolipwa serikali ya CCM kwa jeshi la Polisi kuwatumia, lakini hilo ndio linapotosha watu kudhani ni CCM wanawatumia Polisi badala ya ukweli kwamba Polisi wanawatumia CCM. Kuthubutu alikoonyesha Sirro katika suala la Hamza sio kwa kawaida, bali kunakupa picha ana namna ya kuona "nani atanifanya nini".

Kwa mfano, umewahi kujiuliza nani amekuwa anakwamisha jitihada za kuunda chombo kinachojitegemea cha kuwasimamia Polisi? Nchi kama South Africa, kesi zote dhidi ya vitendo visivyofaa vya Polisi zinachunguzwa na kitu kinaitwa Independent Police Investigative Directorate (IPID), na nchi nyingi sana zinakuwa na chombo hiki ambacho kama kingekuwapo hapa Tanzania, ndio kingechunguza suala la Hamza, sio Polisi wenyewe. Nani amekuwa akikwamisha jitihada za kuwa na chombo hiki hapa Tanzania?

Malalamiko dhidi ya Polisi kwa sasa ni mengi sana, bara na visiwani. Sasa kama kweli serikali ya CCM haitumiwi na Polisi, basi tunamshauri Raisi Samia afanye haraka sana kuunda Independent Police Investigative Directorate (IPID) ya Tanzania (kwa Kiswahili Idara huru ya Kuchunguza Polisi) ambayo inapaswa kuwa chini ya Jaji Kiongozi au labda Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwenye hili la Hamza hatua madhubuti ni muhimu sana ichukuliwe na ukweli ujulikane na suluhu ya ukweli ipatikane ikiburuzwa ovyoovyo linaweza kuleta balaa kubwa zaidi ya kuzalisha waliochfukwa zaidi ya Hamza
 
Back
Top Bottom