Umewahi kuingilia ugomvi usiokuhusu halafu yakakukuta makubwa?

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
31,979
64,000
Kuna watu hatupendi wengine waonewe hivyo tunaingilia ingilia sana ugomvi wa watu. Magu anasema 'Kuwashwa washwa' anyway wakati mwingine show unayoiingilia jukwaa ni kubwa show ndefu halafu wewe pumzi ndogo.

Nina visa vingi vingi (si unajua ukiwa mlinzi wa club eeh? Au kuishi uswazi?) Basi nitaandika kimoja kimoja kadri nitakavyokumbuka.

Nilipanga chumba maeneo fulani hivi kulia napakana na mshkaji bachela kama mimi kushoto yupo jamaa na mkewe na kachanga nahisi kama miezi miwili haizidi minne.

Basi siku hiyo usiku kama saa nane nikawa nasikia mwanamke anamwambia mwanaume (hakuna ceiling board)
"Mi sitaki bwana niache" nasikia jamaa akinong'ona kwa besi akili yangu ikaniambia jamaa anataka tendo.
Kisha nikasikia kilio cha binti kile chembamba cha chini chini lakini cha kwikwi.

Akili yangu ikaniambia jamaa anaomba jicho nini analila kilazima. Kisha sauti ikaongezeka halafu nikasikia chombo cha udongo kinavunjika halafu zikafuatia purukushani na mwanaume akitukana, hapo nikashtuka.
Nikafungua mlango, nafika sebuleni nakuta wapangaji wengine walikua hapo muda tu, wamama wawili na yule mshkaji wa kulia kwangu.

Basi nikajitia ujasiri nikaenda kugonga mlango purukushani zikakoma nasikia kilio tu cha binti. Nikazidi kugonga mara mlango ukafunguliwa akatoka yule mwanamke mbio jamaa akaja mlangoni kufunga mlango.
Tukakutanisha macho, hakusema kitu na mimi kimya tunatazamana tu. Akafunga mlango.

Wamama wakasema yule binti atakua kakimbilia ukweni kwake.

Nikarudi kulala..........

Ndugu Mwenyekiti,

Ilikua MARCH 2016 usiku wa kuamkia jumapili.

Wiki hiyo yote nilikua na misukosuko ya kutosha, basi kama zali weekend hiyo ikawa ni birthday ya shemeji yangu(mdogo wake wife)- halafu huyu shemeji yangu ni maarufu wengi humu wanamjua ila sitomtaja.

Sasa wao wakaamua birthday ikafanyiwe pale "Bulls" survey njia ya kwenda UDSM, sasa pale home kwenye friji nilimnunulia wife castlelager kama 6 hivi 1week before, ila hakunywa, tulikua tunaishi na dogo mmoja hivi anatusaidia kazi pale home, sasa hiyo jumamosi mida kama ya saa 11jioni kupitia kwenye friji nikakuta zile bia, wife akasema hana mzuka nazo(alikua na ujauzito wa kama wiki 6 hivi) nikaona siyo issue nikamwambia yule dogo anayetusaidia kazi azipige.. dogo akazifakamia akachangamka kichizi.

Mida ya saa tatu usiku safari ya kwenda Bulls kwenye birthday ikaanza, tulipofika pale kwakweli palikua "pamenoga sana", tukaendelea kuvesha, wakalishana cake pale mambo yakaendelea . Kipindi hicho mimi nilikua nakunywa " vikali" sasa pale nilikuta watu wanavesha "nyagi dry" mzee baba "nikaliunga", hapo tulienda na yule dogo wa kunisaidia kazi, kichwani alikua na castlelager 6 tayari, alipoiona nyagi akawehuka na yeye akaendelea kuvesha, alikua anahamu nazo sana maana alikua anakunywa kwa kujifichaficha pale home nisijue ila mimi nilikua nishajua huyu dogo nae ni mkata maji mzuri tu so nilipompa huo "uhuru wa manyani" akawa so excited.

Hapo kama siku mbili zilizopita wife aliniambia kuwa Boyfriend wa mdogo wake-huyu birthday girl wetu ambaye ni shemeji yangu ameoa. Yaani jamaa ni mume wa mtu ila hajamwambia ukweli huyu binti, so binti hajui lolote anajua huyo ndiye future husband wake, lakini daily walikua wanagombana binti anaforce apajue nyumbani kwa jamaa maana jamaa kajenga goba ila jamaa anamchomolea kumpeleka kwake wanaishia kwa binti tu, hapo jamaa anaprovide kila kitu kwa binti.

Sasa kumbe wife alifanikiwa kuijua hiyo siri kupitia "washakunaku" faster akamwambia mdogo wake ukweli wa mambo kuwa jamaa kaoa, ni mume wa mtu zaidi ya miaka miwili, mdogo mtu akatafuta perfect time ya kuanzisha ugomvi, na kwa timing zake akaona siku hiyo ya birthday ndo aliamshe dude.

Basi bwana turudi pale Bulls, shughuli ilikua inafanyikia ndani mule kuna club, Tulilewa, Tukalewa, Tukalewa- Yesu wangu! Ukafika muda wa kuondoka, ilikua kama saa tisa hivi usiku, tokatoka nje pale, tupo kama watu 10 hivi, wakati huo yule dogo niliyotoka nae home alikua kazima kama mida ya saa nane hivi so nikampeleka kwenye gari nikamlaza seat ya nyuma.

Tukiwa pale nje kwenye parking tunataka kuagana varangati likaanza! Plan yangu ilikua nimpakie shemeji na boyfriend wake nikawadrop kwake(sinza) halafu sisi turudi home Africana-mbezi. Hapo mimi nilikua sijajua kama kuna mkakati wa kuliamsha dude, mara naona wanajizungusha, nikamwambia wife twendeni basi muda unaenda tukapumzike nimechoka, mdogo mtu akadakia, akasema kwa sauti kubwa mbele ha madereva tax na bodaboda "Shem yaani leo nataka nikalale kwa mume wangu, nataka akanit.o.mbeeeeee mpaka nijisikie kuwa leo kweli nim.et.ombwaaa", DAH..!!! kusikia vile madereva tax wakalipuka kwa makelele oyooooooo.... noma ... noma !!
Nikageuka kumtazama yule boyfriend wake nikaona anatabasamu lakini ni kama anahofu sana, akili ika'click kwamba hapa wanataka kumletea jamaa zengwe waende kwake waka'prove kama kweli jamaa kaoa au la!

Nikasema ngoja nimuokoe mwanaume mwenzangu, hapo wote tumelewa isipokua huyu boyfriend-ake. Wakati huo yule dogo kwenye gari katapika nyongo seat za nyuma huwezi kuzitazama mara mbili.. Nikamwambia Shemeji yangu, " Shem skia, kwasasa ngoja niwapeleke sinza, pakikucha mtaenda home kwa jamaa" akajibu "hapana, haiwezekani kila siku yeye hataki nipajue kwake, sasa nasema hivi hapa kama tunaondoka safari ni goba, siendi popote zaidi ya kwake", hapo kuna nyomi lishatuzunguka, nikaona ngoja nimvute pembeni nimpige darasa atanielewa tu, ile kumshika mkono tu wife nae akadakia "unataka uk.a.mt.ombe wewe?, unaingilia nini wewe yanakuhusu?"

Nilimrukia nikamlima kofi moja akaanguka chini, akanyanyuka mzimamzima akaniparamia mzee baba nikajikuta chini akanikalia kifuani halafu sasa yeye ni "giant" nikajikuta nashindwa kunyanyuka, akaniparua na kucha + ngumi, mzee baba nikaona fedheha gani hii tena, nikajikaza kiume nikampindua nikainuka, sasa nikaamua ngoja niende kwenye gari nisepe niwaache, ile nashika kitasa cha gari nilivutwa mpama chini tena, tulibiringishana pale mpaka akanichania vifungo vyote vya shati nikabaki vest nje.

Akafanikiwa kunitight vizuri sana, kila nikijaribu nikaona hii issue inakua series sasa nikaanza kumvesha ngumi, lakini kwakua nilikua tungi kila ngumi ninayompiga nikaona haimuingii, nikamng'ata mkono akashtuka kidogo hajakaa sawa nikamtia meno ya mgongo tena halafu nikainuka yeye yupo chini analia, nikaenda kwenye gari nikaweka D safari, hapo yule shemeji yangu, mumewe na marafiki wengine wanahangaika hawajui cha kufanya,! kufika pale calabash roho ya huruma ikanijia nikakumbuka pale alipo mbuni kipande hana, atafikaje home, nikapiga u-turn kupitia ile service road nikawakuta wote kwa pamoja wanatembea mdogo mdogo, nikageuza gari nikamwambia panda twende, akagoma nikashuka kwa hasira nikaanza kumburuta washkaji wanania muache tu uaimfanyie hivyo nikawaambia kama kweli mnamuhurumia nisaidieni kumbeba tumuweke seat ya nyuma, nikaweka ile child rock ya milango ya nyuma maana alikuwa na tabia tukizinguana tukiwa kwenye gari anafungua mlango ili kuruka.Basi tukambeba pale tukamuweka nyuma na yule dogo, nikatia gia safari.. Mpaka leo wife ana alama ya meno mkononi, ya mgongoni ilishafutika.
 
Hahahaha ni kipi kikakusibu sasa mana umenifanya nisome had mwisho halaf haijaisha
 
Sasa natakiwa kwenda Kigamboni asubuhi nikawa nipo Mwananyamala A nasubiri gari la Stesheni upande wa pili namuona yule mshkaji.
Mshkaji kuniona akaanza kukimbia, sijui ujinga niliutoa wapi, nikamuunganishia bwana.

Nikaenda kumkamata pale shule ya Kisiwani. Basi ile kumfikia na kumshika tu jamaa kilimtoka kichwa hiko kikatua moja kwa moja kwenye paji la uso.
Bado mawenge yamenivaa nashangaa nipo chini, kumbe nimekula mtama.

Ghafla jamaa yuko juu anapeleka mikono mvururu usoni, hapo naomba Mungu wasamaria waje. Wakaja kumtoa nipo chini hoi shenzi mimi.

Nyumbani tulipofika hatukuongeleshana.

Huo ugomvi namba moja.
 
Kuna rafiki yangu anamiliki video library so anaburn miziki na watu wa ofisi hizi hua wanaweka sauti za muziki juu sana.

Basi tumekaa hapo mara akaja jamaa, mtu wa makamo kama miaka 45 hivi mfupi, mweusi, mwili mdogo mdogo, akauliza.
"Nani mhusika hapa?"
Mshkaji akajibu "Mimi"
Jamaa akaendelea "Watu wanasema wamekufuata kama mara nne upunguze sauti"
Mshkaji wangu akajibu "Hapana hapa hajaja mtu au Castr umemuona mtu?"
Nikajibu "Hapana" (Ni kweli hakuja mtu)
Akaendelea yule jamaa "Basi sawa, punguza sauti"
Mshkaji wangu akamjibu "Siwezi kupunguza, wateja wanatakiwa wajue kua nipo"

Yule jamaa akajibu sawa akaondoka, baadaye kidogo akarudi na mtu mwingine. Wa makamo pia ila ana mwili kumzidi huyu, mrefu na mweupe lakini anaonekana kalewa au ni mlevi wa kila siku.

Jamaa wakaanza tena utata juu ya sauti. Mimi nikasema kwani mbona mnamsumbua mshkaji wangu shida nini. Yule mwenye mwili mdogo akajibu "Haikuhusu kaa pembeni"
Nikasimama nikapeleka kitasa, kikampata yule mlevi wa kila siku akasema "Wewe unaipiga serikali?" Nikamwambia "We mwenyewe unasemaje?"

Hapo watu wakawa washajaa, si unajua uswazi? Kwahiyo nikawa nakula ujiko natamba. Nikamwambia "Toeni vitambulisho basi kama nyie serikali"

Nilikua sijui serikali hua inaajiri walevi mbwa kwa ajili ya kazi zao, hivyo sikudhania kuwa hawa wanaweza kua watumishi wa serikali.

Vitambulisho vikatoka.

Mweupe ni mtendaji wa kata ya Mwananyamala kwa Kopa na mweusi ni askari kanzu wa kituo kidogo cha Kwa Kopa.

Nilinywea.

Natamani kukimbia lakini nahofia watu wataona kumbe jamaa muoga.

Niliyempiga kitasa akatoa pingu,nikavalishwa mpaka kituo kidogo cha kwa Kopa.

Mizunguko miiiiiiingi lakini nikatoa hela ndiyo nikatoka.
 
Kuna rafiki yangu anamiliki video library so anaburn miziki na watu wa ofisi hizi hua wanaweka sauti za muziki juu sana.

Basi tumekaa hapo mara akaja jamaa, mtu wa makamo kama miaka 45 hivi mfupi, mweusi, mwili mdogo mdogo, akauliza.
"Nani mhusika hapa?"
Mshkaji akajibu "Mimi"
Jamaa akaendelea "Watu wanasema wamekufuata kama mara nne upunguze sauti"
Mshkaji wangu akajibu "Hapana hapa hajaja mtu au Castr umemuona mtu?"
Nikajibu "Hapana" (Ni kweli hakuja mtu)
Akaendelea yule jamaa "Basi sawa, punguza sauti"
Mshkaji wangu akamjibu "Siwezi kupunguza, wateja wanatakiwa wajue kua nipo"

Yule jamaa akajibu sawa akaondoka, baadaye kidogo akarudi na mtu mwingine. Wa makamo pia ila ana mwili kumzidi huyu, mrefu na mweupe lakini anaonekana kalewa au ni mlevi wa kila siku.

Jamaa wakaanza tena utata juu ya sauti. Mimi nikasema kwani mbona mnamsumbua mshkaji wangu shida nini. Yule mwenye mwili mdogo akajibu "Haikuhusu kaa pembeni"
Nikasimama nikapeleka kitasa, kikampata yule mlevi wa kila siku akasema "Wewe unaipiga serikali?" Nikamwambia "We mwenyewe unasemaje?"

Hapo watu wakawa washajaa, si unajua uswazi? Kwahiyo nikawa nakula ujiko natamba. Nikamwambia "Toeni vitambulisho basi kama nyie serikali"

Nilikua sijui serikali hua inaajiri walevi mbwa kwa ajili ya kazi zao, hivyo sikudhania kuwa hawa wanaweza kua watumishi wa serikali.

Vitambulisho vikatoka.

Mweupe ni mtendaji wa kata ya Mwananyamala kwa Kopa na mweusi ni askari kanzu wa kituo kidogo cha Kwa Kopa.

Nilinywea.

Natamani kukimbia lakini nahofia watu wataona kumbe jamaa muoga.

Niliyempiga kitasa akatoa pingu,nikavalishwa mpaka kituo kidogo cha kwa Kopa.

Mizunguko miiiiiiingi lakini nikatoa hela ndiyo nikatoka.
Enheeew endelea siku nyingine ikawaje
 
Back
Top Bottom