Umewahi kufikiri kuhusu usalama wa watoto wako kijinsia?

Inasikitisha sana kijana mtu mzima ana afya ya akili kuandika upumbavu wa kiwango hiki, unless aseme ana matatizo ya afya...
Binadamu tuna aina tofauti ya kukabili matukio yasiyopendeza machoni, akilini au mioyoni!
pengine ndiyo namna yao ya kukinzana na hiki kilichoandikwa!
 
Sheria mbovu za nchi.Fanya utumbo Arab country ama some asia countries.Yemen wanakuwasha hadharani.
 
Mimi nakumbuka dada yangu(mtoto wa baba mkubwa) alikuwa akifunga mlango wa chumbani halafu ninaanza kumyonya matiti ila alikuwa hataki nimshike vuzi.hapo nilikuwa niko darasa la kwanza
Baada ya mama na baba kutengana ilibidi aje atulee maana yeye ndio alikuwa kamaliza la saba huko tabora.
Hadi leo huwa nakumbuka sana hilo tukio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masheikh madrassa wanawaharibu Sana mabinti wa kiislamu,samahani lakini
a-875x500.jpg
Maaskofu na mapadri hunyemelea watawa kimapenzi – Papa Francis – Taifa Leo
  • Feb 07, 2019
Maaskofu na mapadri hunyemelea watawa kimapenzi – Papa Francis
Na MASHIRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis amekiri watawa wengi wamekuwa wakidhulumiwa kimapenzi na mapadri na maaskofu.

Hii ni sakata nyingine inayohusu dhuluma za ngono katika kanisa hilo ambalo limekuwa likikumbwa na kashfa tele za wahubiri wake kulawiti watoto wa kiume.

Akizungumza Jumatano akiwa safarini kwenye ndege yake kutoka ziara ya Milki ya Kiarabu (UAE) kuelekea Vatican, Papa Francis alisema makao makuu ya Kanisa Katoliki yalipokea ripoti kuhusu mapadri wanaodhulumu watawa hapa Afrika katika miaka ya tisini, na kuongeza kuwa tatizo hilo bado lipo hadi sasa hasa katika makanisa mapya.

“Kuna mapadri na hata maaskofu ambao wamewahi kufanya hivyo. Nadhani ni kitu ambacho kingali kinaendelea kwa sababu hiki si kitu ambacho huisha tu ghafla, la hasha!” akasema.

Aliongeza: “Sitaki kusikia ikisemekana kwamba kanisa halina tatizo hili, kwa sababu ukweli ni kuwa lipo. Tunahitajika kujitahidi zaidi kulikomesha na tuna nia ya kufanya hivyo.”

Alisema hayo alipoulizwa swali kuhusu ripoti iliyochapishwa majuzi kwenye jarida la ‘Women Church World’ ambalo husambazwa na gazeti la Osservatore Romano linalochapishwa Vatican.

Ripoti hiyo ilifichua jinsi watawa wamekuwa kimya kuhusu dhuluma ambazo wamekuwa wakipitia kwa miongo mingi mikononi mwa maaskofu na mapadri kwa sababu wanaogopa kuadhibiwa wwakifichua.
Suala hilo liligonga vichwa vya habari mwaka uliopita baada ya mtawa kudai askofu wa kanisa lililo nchini India alimbaka mara kadhaa.

Katika kisa hicho, Askofu Franco Mulakkal wa miaka 53, alikamatwa Septemba 21 kwa kushukiwa kumbaka mtawa huyo mara 13 kati ya mwaka wa 2014 na 2016. Papa Francis alimsimamisha kazi kwa muda siku moja kabla akamatwe.

Nchini Kenya, kumekuwa na kashfa tele katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu madai ya ubakaji na ulawiti unaotendwa na viongozi wa kanisa hilo. Kisa cha majuzi kiliripotiwa Kiambu ambapo padri alidaiwa kushiriki ngono na wasichana wachanga waumini na pia kuwasaidia kuavya mimba.

Mwaka uliopita, shirika la International Catholic Organisation lilitoa wito kwa akina mama wenye watoto ambao baba zao ni mapadri wajitokeze ili watoto hao wafanyiwe uchunguzi wa DNA kwa ajili ya kufanya baba zao wawajibikie ulezi wao.

Papa Francis alisema kuna viongozi wengi wa kidini katika kanisa hilo ambao wamesimamishwa kazi kwa kudhulumu watawa na afisi yake imekuwa ikijitahidi kusuluhisha tatizo hilo kwa muda mrefu.
Kulingana naye, tatizo lenyewe ni la kidesturi lililo na mizizi yake katika jinsi wanawake wanavyotazamwa kuwa wasio na thamani katika jamii.

Alitoa mfano wa kisa kilichotokea Ufaransa ambapo mtangulizi wake, Papa Benedict wa 16 alijaribu kuchukua hatua lakini juhudi zake zikazimwa na baadhi ya maafisa wakuu wa Vatican:
Kumekuwa na mapendekezo kuwa Kanisa Katoliki liwaruhusu mapadri wake kuoa.
 
Hili kweli ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu za kiafrika. Nadhani tunaweza kutatua hili tatizo kwa njia kuu mbili tu...

1: Sisi wazazi au/na walezi tujitaidi sana kutumia muda mwingi sana tukiwa na familia zetu, hususani watoto. Naamini mzazi / mlezi anapokuwa karibu na mtoto, hakika huyo mtoto atamchukulia mzazi kama rafiki yake. Kuanzia hapo mzazi/mlezi atakuwa ametengeneza room ya kuweza kuyajua yote yanayomsibu mtoto....maana mtoto mwenyewe atakuwa tayari kufunguka kiurafiki....bila mashaka au uoga wa kukalipiwa au kupigwa na mzee.

2: Pia nadhani ni wakati sahihi sasa wa kuunda UMOJA WA FAMILIA SHIRIKISHI (kama ilivyokuwa zamani 60's-80's).....m/watoto walikuwa wakikutwa wanafanya mambo ya ovyo, hakika walikuwa wanapewa adhabu na mtu mzima yoyote yule. Hii ilisaidia sana kufanya mtoto akue katika maadili staiki....

---Hapa tunaweza kuanza kwa kuunganisha angalau familia 3 za eneo moja (watoto wanapoishi)....hatimahe mdogo mdogo kadili +ve impacts zitakavyokuwa zinaonekana, ndivyo familia mbalimbali zitakuwa zinaongezeka katika umoja huo.

Nawakilisha hoja....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu nimempa somo sana wakati nampeleka boarding nikiona nyuzi kama hizi moyo unaniuma sana.

Mambo mengine tunamwachia Mungu tu
Cha kwanza kama mdau wa elimu nikuulize kwa nini umpeleke mtoto boarding akiwa mdogo? Maana kuna wakati napokea mtoto wa boarding wa miaka 3 hadi unamuuliza mzazi why? Wakati mwingine sisi kama wazazi tunakimbia majukumu yetu ya msingi ambayo ni kulea. Mimi nimelelewa na baba mkubwa toka nina miaka 13. Nina tabia zake nyingi maana alikua anahakikisha kama ni masomo lazima umletee daftari, mitihani, huchezei rasilimali hovyo. Je wewe mwanao atafanana na wewe hata kidogo? Kumleta mtoto boarding akiwa mdogo japo kwetu ni biashara yenye mkate ila huwa na changamoto hasa ninapofikiri kwamba hatafanana na mzazi wake chochote zaidi yasura. Hapa millenia inabidi tujifunze kitu kutoka kwa Baby Bomers.
 
Tafiti na shuhuda nyingi zinathibitisha usalama finyu wa kijinsia unaowakabili watoto.

Leo tutizame maeneo HATARI ZAIDI KWA WATOTO
Haya ni MAENEO YANAYOFIKIRIWA KUWA NI SALAMA KABISA!
-MAJUMBANI.
Watoto huharibiwa zaidi na ndugu, kaka zao, dada zao, mabinamu, babu, baba, mama, wajomba, baba wadogo, mama wadogo jamaa marafiki wazazi, majirani, watoa huduma kama nannies.

(TUKIPITISHA KURA HAPA WENGI WETU BIKRA ZA KIUME NA KIKE ZIMETOKA CHINI YA PAA LA NYUMBA YA BABA ZETU, wanaume ni mashahidi zaidi wa hili, namna walivyojifunzia ngono mapajani mwa dada zao waliokuwa wanawalea, UNAFKR MWANAO HALIWEZI KUMKUTA?UMEWAHI KUFIKIRI NAMNA YA KUMLINDA , AU NAMNA YA KUMSAIDIA AKIPATA THE SAME SAGA ULILIPATA? ANAWEZA KUKWAMBIA?)

-MASHULENI
Walimu, wanafunzi wenzao, wahudumu wa shule kama madereva wa magari, matrons/patrons, viongozi wa madarasa,viongozi wa mabweni. Watoto huamini walimu wao sana, watoto huamini wezao sana, watoto hutumia muda mwingi shuleni kuliko nyumbani! Kile mzazi atasema ,ili kiwe na mashiko ni lazima mwalimu au anko wa shule akisisitize! UMEWAHI KUFIKIRI KUHUSU HATARI YA MWALIMU NA ANKO WA SHULE ANAMWAMBIA NINI MWANAO? UMEWAHI KUWAZA IWAPO HABARI UNAZOSIKIA ZINATOKEA KWA WENGINE PENGINE NA MTOTO WAKO ANAAMBIWA MANENO YALE YALE? UNAJUA NAONGEA NINI NA WENZIE? ANA TAARIFA KINZANI YENYE UKWELI KUHUSU LOLOTE ANALOAMBIWA KIASI LISISHIKE AKILI YAKE?



-NYUMBA ZA IBADA
Walimu wa dini, makasisi, mashekhe, wahudumu wa kanisa na misikiti. Elimu duni pembeni hii ni elimu ya kiroho! Kama vile umwaminivyo kiongozi wako wa kiroho , ndivyo na yeye mwanao anavyomztizama pengine kama mungu(kulingana na anachoelewa kuhusu mungu)USIWAZE POPOTE KUWA KUNA KITU ATAAMBIWA NA KIONGOZI WA KIROHO AKATAE! kwanza kwa imani pili kwa vitisho! Tena akipitia mistari na nukuu zile zile.
-MTAANI
Vyombo vya usafiri, mitandao ya kijamii, vichochoro vya njia, makondakta , madereva, bodaboda, bajaji, wauza maduka, wauza vitu vya kula kama chipsi, lambalamba, ubuyu, kashata , ice cream, chama.


HAYA NI MAENEO TU.
Kuna IMANI ZA KISHIRIKINA , kuna MIHEMKO YA UMRI, kuna ELIMU RIKA POTOFU, kuna MIKUMBO NA KUIGA.

KWA KIFUPI HAWAPO SALAMA!
HAWAPO SALAMA!
HAWAPO SALAMA!
Weka nukta, puuza, ona ni ya kupita , ona halikuhusu LAKINI MY DEAR WATOTO WETU HAWAPO SALAMA!

TUFANYE NINI?
TUPEANE MAWAZO!


Asante kwa kutuweka hadhiri. Kwakweli tuna shida kubwa sana kwani nchi zetu tupo kipindi cha mpito, mifumo ya kimaisha imebadilika kwa kasi sana na kuathiri maisha yetu. Kibaya zaidi jamii yetu si watu wa kujiongeza, wengi bado tunaishi kizamani sana, kuaminiana kusiko kwa msingi. Mpaka leo tunaishi majumbani kwa kuaminiana sana, kwa mfano, watoto wako unajua kabisa hawajaweza kujiamulia mambo yao wenyewe unawalaza chumba kimoja na wakubwa.

Sasa utaona kwanini wazungu wanaonekana wabinafsi, yani vile wanaishi peke yao peke yao, wamefika hadi hatua wanawapeleka wazazi nyumba za kulelea wazee, na sisi siku zinanukia. Japo sababu ni nyingi, lakini hili pia linaepukwa!

Asante kwa kushare nasi
 
Malezi ya sasa changamoto kubwa tuliyojengwa nayo ni usiri uliopitiliza kuonesha wakubwa hawakosei. Ishu za molestation zipo nyingi tu kwenye familia zetu lakini kwa vile hatupo tayari kufumbua vinywa vyetu na kuviongea vitabaki kama siri kwa miaka mingi itakayoendelea. Tunahitaji tuwe na uthubutu wa kuvisema hadharani, kukemea bila kuangalia rangi pamoja na kuchukua hatua stahiki. Trauma zinazokula kizazi chetu ni kubwa sana. Tunahitaji uthubutu wa kuongea ili kizazi kinachokuja kisikute hii hali ya uwoga iliyopo sasa hivi. Tukisimama na elimu kwa watoto wetu tutaweza kuangaziza tatizo hili lakini tukilifungia kabatini kuna siku mawe yataongea kutushitaki kwa nini hatukuchukua hatua.
Pia tunatakiwa tuwe makini na sign wanazotoa watoto wetu. Kwa mfano unakuta mtoto anakwenda tuition kwa fulani ila inafika siku mtoto anakataa kwenda tuition kabisa. Mzazi badala ya kumuuliza mtoto ni kwa nini unachukua fimbo na kumchapa. Tunahitaji tuelewe kwamba kwa woga na aibu anaweza shindwa kusema ila mwili huwa unatoa alama zinazo ashiria kuna tatizo. Usalama utategemea na mazingira tunayolelea wanetu pamoja na namna mbalimbali za kushughulikia. Tuige mfano kwa kanisa katoliki na yanayoendelea. Huwezi kuficha milele.
 
Naona kuna mtu hapa kapata sehem ya kuchafua kanisa hasa RC. Utadhani mashehe na maustadhi wao hawana vikojoleo... wakati mimi nimeshudumia walimu wengi wa mdrasa wakiahalibu watoto wa shule za msingi na kuwaachisha shule kwa lengo la kuwaoa...
sidhani ni issue ya DINI IPI!
msihamishe mada tafadhali!
MISIKITINI NA MAKANISANI watoto WANAHARIBIWA!
UMEPATA MFANO WA KANISANI!
doesn't mean HAIPO YA MIKITINI!
tafadhali isituhamishe kiini cha mada!

''WATOTO WAPO HATARINI''

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kuna mtu hapa kapata sehem ya kuchafua kanisa hasa RC. Utadhani mashehe na maustadhi wao hawana vikojoleo... wakati mimi nimeshudumia walimu wengi wa mdrasa wakiahalibu watoto wa shule za msingi na kuwaachisha shule kwa lengo la kuwaoa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanisa Katoliki Marekani lapinga kufuatiliwa kisheria makasisi wanaotuhumiwa kwa ubakaji

Mar 07, 2017 04:27 UTC
  • 4bmv175eebd708ntko_800C450.jpg
Kanisa katoliki nchini Marekani limezuia kuchukuliwa hatua ya kisheria ya watu waliobakwa na makasisi.

Ripoti kutoka Marekani zinasema kuwa, Kanisa Katoliki lilizuia kupasishwa sheria ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka makasisi watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watu hususas watoto wadogo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa, kanisa hilo lilifanya kila lililoweza kuzuia muswada uliokuwa umewasilishwa Bungeni ambao kama ungepasishwa na kuwa sheria, basi ungewafuatilia kisheria makasisi wa kanisa hilo watakaokabiliwa na tuhuma za ubakaji hususan watoto wadogo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, kupasishwa sheria hiyo kungekuwa na ahueni kubwa kwa wahanga wa vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na makasisi wa kanisa katoliki nchini Marekani, vitendo ambavyo vimeripotiwa kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
4bmvbc73ce8bbdntjq_800C450.jpg
Dunia nzima imekuwa ikikemea vitendo vya ubakaji

Katika kuhalilishwa kutopasishwa kwa sheria hiyo kanisa hilo limedai kwamba, kama sheria hiyo ingepasishwa ingekuwa na madhara makubwa ya kifedha kwa taasisi zinazojuhusisha na masuala ya watoto.

Kashfa mbalimbali za kimaadili na kifedha zilizoikumba Vatican na Kanisa Katoliki katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikigonga vichwa vya habari na kuwa gumzo kubwa lisilokwisha duniani.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, kuna mamia ya kesi za ubakaji na ulawiti zinazowakabili makasisi ambazo zimerundikana katika mahakama za Ulaya na Marekani zikisubiri kufanyiwa uchunguzi jambo ambalo kwa hakika limeshusha hadhi ya Kanisa Katoliki ulimwenguni.
 
Naona kuna mtu hapa kapata sehem ya kuchafua kanisa hasa RC. Utadhani mashehe na maustadhi wao hawana vikojoleo... wakati mimi nimeshudumia walimu wengi wa mdrasa wakiahalibu watoto wa shule za msingi na kuwaachisha shule kwa lengo la kuwaoa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Papa Francis: Makasisi wanaonajisi watoto ni nyenzo za shetani, wanaharakati wasema hajachukua hatua za kutosha

Feb 25, 2019 07:56 UTC
  • 4bsec9decb15001ddnw_800C450.jpg
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametoa wito wa kukabiliana vikali na maaskofu na wahubiri wa kanisa hilo wanaowanyanyasa kingono watoto wadogo akisema kuwa watu hao ni nyenzo za shetani.

Akifunga mkutano wa Kanisa Katoliki wa kukabiliana na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, Papa Francis amesema kuwa, kanisa hilo litakabiliana vikali na kadhia hiyo.

Papa amesema kuwa, baadhi ya maaskofu na makasisi wamechafuliwa na madaraka na unafiki na maaskofu wanaowanajisi watoto wadogo ni nyenzo za shetani.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki amesisitiza kuwa kanisa hilo halitasita kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wala halitaficha wana kupuuza uhalifu huo.

Hata hivyo wanaharakati wa kutetea haki za watoto wamekosoa mkutano huo wa Vatican na matamshi ya Papa Francis kuhusiana na wahalifu wa ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto unaofanywa na makasisi na wahubiri wa kanisa hilo wakisema kuwa, hakutangaza vita ya opande zote dhidi ya wahalifu hao na maaskofu wanaoficha na kukingia kifua uozo huo.

4bse0741fd7f4f1db4n_800C450.jpg
Papa Francis
Sambamba na mkutano huo wa Kanisa Katoliki uliotishwa kujadili njia za kuwalinda watoto katika kanisa hilo, wahanga na waathirika wa uhalifu wa makasisi na maaskofu wamefanya maandamano mjini Roma wakilaani kitendo cha Kanisa Katoliki na viongozi wake cha kuficha uhalifu huo kwa miongo mingi.

Inaelezwa kuwa, kuna mamia ya kesi za ubakaji na ulawiti zinazowakabili makasisi na viongozi wengine wa kanisa hilo, ambazo zimerundikana katika mahakama za Ulaya na Marekani zikisubiri kufanyiwa uchunguzi, jambo ambalo limelichafua Kanisa Katoliki Duniani.
 
Mada nzuri sana hii na fikirishi pia, "Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo" kwa uzoefu wangu binafsi kila tabia inayoumbika kwa mtoto chanzo chake ni TAARIFA (information), kwa hiyo kama Mzazi/Mlezi lazima tuwe vyanzo vya kwanza na vya kuaminika vya taarifa kuhusu ukuaji wa mtoto, hii itafanya kuwe na kubadilishana taarifa katika Mtoto na Mzazi/Mlezi, hata akipta taarifa nje kuhusu jambo lolote atataka ufafanuzi wa kwanza kutoka kwako, ila tukiaacha mtoto apate taarifa kutoka vyanzo vingine hapo ndio madhara yanapoanzia.

Jambo lingine ni ufuatiliaji wa karibu wa mahusiano ya mtoto na watu alio nao karibu katika maeneo yote anapokuwa kama shuleni, kanisani, msikitini na nyumbani pia. Nilikuwa nazungumza na Walimu kwenye shule za serikali, wakasema toka elimu bure ianze wazazi hawana sababu ya kutembelea shuleni, na hiyo imeleta madhara mengi kwa wanafunzi kwasababu hakuna uhusiano wa kimalezi kati ya Wazazi na Walimu.
 
Wazazi tujenge tabia ya kuongea na watoto wetu kwa upendo kabisaaa!
Tuwe tunawaelimisha madhara ya hiyo michezo ambayo wanaianza wakiwa na umri mdogo!

Tuhakikishe tunawapatia huduma muhimu na kwa wakati ili kupunguza vishawishi!

Lakini zaidi ya yote tuwaombee watoto wetu kila iitwapo leo! Hakuna linalomshinda Mungu jamani, tuwafiche kwenye mbawa za Malaika wa Mungu! Na kuhakikisha mtoto anakuwa katika hofu ya Mungu!

Hapa ukiuliza utagundua kuna mzazi hana muda wa kumwambia Mungu amlinde mwanae! Jitolee hata siku moja funga sababu ya watoto wako, toa sadaka mshukuru Mungu wako hakika na Mungu atawasimamia kila iitwapo leo!
 
Daaaah! mleta huu mjadala umewaza sana njee ya box,kiukweli watoto hawako salama kabisa ,ni jambo la Kuomba Mungu na kushiriki kwenye malezi ipasavyo
Mimi pia naweza sema ni muhanga wa shida kama hiyo ,ukiwa na watoto mabinti hasa ile hali ya kukua wanajaribu vitu vingi sana unaweza kuta anamchukua hata mdogo wake wa damu na kujaribu kufanya sex
Dada yangu wa kwanza(marehemu) huyu yeye huyu alikulia upande wa bibi (mzaa mama) nakumbuka tulifunga safari kwenda kumuona bibi kijijini nilikua mdogo sana arouund 5-6 years ,bibi na mama walitoka wakatuacha wawili sikuwa na ufahamu wowote kipindi hicho aliniita chumbani akavua akanikamata akawa anapeleka kwenye sehemu yake ,kwa umri ule sikujua nini anamaanisha.
baada ya hapo akaniambia usimwambie mama,sikuweza kumueleza hadi leo huwa ni siri nimetunza,

kumbuka hata watoto wako wa kuzaa mwenyewe wanaweza kujijaribu wenyewe pia
 
Wazazi tujenge tabia ya kuongea na watoto wetu kwa upendo kabisaaa!
Tuwe tunawaelimisha madhara ya hiyo michezo ambayo wanaianza wakiwa na umri mdogo!

Tuhakikishe tunawapatia huduma muhimu na kwa wakati ili kupunguza vishawishi!

Lakini zaidi ya yote tuwaombee watoto wetu kila iitwapo leo! Hakuna linalomshinda Mungu jamani, tuwafiche kwenye mbawa za Malaika wa Mungu! Na kuhakikisha mtoto anakuwa katika hofu ya Mungu!

Hapa ukiuliza utagundua kuna mzazi hana muda wa kumwambia Mungu amlinde mwanae! Jitolee hata siku moja funga sababu ya watoto wako, toa sadaka mshukuru Mungu wako hakika na Mungu atawasimamia kila iitwapo leo!



Ulilo lisema ni jambo la muhimu na msingi sana Mkuu,katika kuwaelimisha hapo wazazi wasione hayan kuwaeleza watoto juu ya maeneo yao sehemu zaa siri, na ni kwanini hawatakiwi kuguswa wala kupigwa picha(imekuwa mtindo mpya sasa) na watu wengine hata kama ni mtu wa karibu, tujaribu kuwaelekeza kwa juhudi na maarifa kwelikweli ma tuwaelekezavyo shughuli za nyumbani kama kuosha vyombo na kupika.
 
Back
Top Bottom