Umewahi kuchunguza kwanini ccm sasa imeanza kuchukiwa mpaka vijijini? Kama bado soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kuchunguza kwanini ccm sasa imeanza kuchukiwa mpaka vijijini? Kama bado soma hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENGETI, Feb 14, 2012.

 1. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Wana JF wote salaam sana
  Nimekaa na kutafakari sana kwanini watu hawaitaki CCM tena kwenye maisha yao. Pamoja na tabu na ugumu wa maisha kwa watanzania unaotokana na Uzembe,upuuzaji na Ufisadi wa viongozi wa serikali inayoundwa na CCM pia yapo mambo mengine mengi ambayo chama hicho kinawafanyia watanzania hasa wanachama wake.
  Pamoja na Ruzuku ya Tsh milioni mia nane kwa mwezi,vyanzo vya vingine vya mapato chama hicho ilivyodhulumu kutoka watanzania enzi ya chama Kimoja kuna unanyang'anyi mwingine mkubwa wanaofanyiwa wanaCCM.
  kwenye Attachment ni Fomu inayoitwa ya Mshikamano wa kumdhamini baba mwanaasha. Na sijui anadhaminiwa wapi na kwanini! masharti ya fomu hii ukiipoteza unatakiwa uwasilishe Tsh 50,000 la sivyo unafunguliwa mashtaka mahakamani. Fedha hizi zinaenda moja kwa moja makao makuu ya Chama . Fomu hii imegawanywa mpaka kwa katibu wa tawi ambaye ana nguvu kuliko hata mwenyekiti wa Kijiji. Kuna sehemu ya nchi hasa huku Kilimanjaro usipochangia fomu hii UNAPAMBULIWA (yaani kunyanga'nywa sehemu ya mali ili kufidia mchango unaopaswa kuutoa)
  Naomba kuleta kwenu kwa mjadala zaidi Je ni haki kwa CCM kuwafanyia wananchi maskini kitu hiki
   

  Attached Files:

 2. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ujinga wa Watanzania ndio mtaji wa ccm
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Naunafki wao PIA
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tusipobuni njia muafaka ya kuwatoa whawa majambazi wezi,mafisadi wadhulumaji tutalaanika na kamwe nchi ya asali hatutaiona sasa ni vipi sisi watanzania tumeshindwa kujua mbinu wanazofanya za wizi wa kura najiuliza hakuna mtu mwenye akili ya kutengeneza utaratibu wa kuhakikisha hawa wezi hawaendelei kushika uongozi wa nchii -CCM wezi wote tuseme CCM byE bye
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona hata CHADEMA huwa wanakusanya michango ya kukichangia chama kwa kutumia gari lao dogo aina ya Suzuki vitara
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  ccm ni chama cha siasa na wanapaswa kujiandaa kwa mambo mengi, ikiwemo pamoja na chaguzi za ndani, sio vibaya kuchangisha wanachama wake na wapenzi wake. Kibaya ni kukwiba fedha za serikali kwa faida yao.

  Sioni tatizo katika hili, kwani tumechangia mengi ikiwemo hata kwa njia ya simu. Wangeendelea hivi, halafu wakarudisha mali yetu waliyobinafsisha wakati wa mfumo wa chama kimoja na kuacha wizi na ufilisi wa mali ya umma kama vile mashirika ya bima ili kuchangia kampeni zao ingekuwa safi sana. Tungeanza kuona mabadiliko ya dhati
   
 7. d

  davidie JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We kengemutope jibu hoja ya msingi acha kuwa kama job nugai alipoulizwa mambo ya posho za wabunge akakimbilia kutoa mifano ya tra na makanisani, wewe umeulizwa ccm unaulizia chadema kwani cdm ndio mfano wenu wa kiutendaji?
   
 8. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Aghhhhhhhhh nsha choka na hili li chma
   
 9. H

  Hiraay Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usikichoke bana!!! Kigumu Chama cha Magamba.
   
 10. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Binafsi sioni chochote ulichosimlia kuhusu form hii. Nilidhani kuna exclusive clauses katika fomu hii ambayo inaelezea hayo unayotamka kumbe ni from your mouth. Mchango kwa chama si dhambi kwani ndiyo sehemu kuu ya mapato.Hilo la kulazimishwa sijapata kusikia ama kusoma kwani ni hiari ya mwanachama.

  WanaJF tusiwe wepesi kuchangia mada ambazo hatuna uelewa wa kina kisa tu imerushwa na sababu ni CCM.Tuwe makini kushirikisha mbongo zetu na tusiwe bias (personal interest) tujadili facts/ideas.
   
 11. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ujinga wa watanzania ni mtaji wa wanasiasa....!
   
 12. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu hoja yangu sio jinsi kukusanya Hoja ipo kuwa fedha zote hizi zinaenda kufanyia kazi gani? CCM hawajengi Shule, zahanati na hata barabara. Huku kwenye wilaya na Kata Chama kinaendeshwa kimagumashi kwani hakuna hata centi inayokuja huko wilayani! fedha za kukodisha malori ni Halmashauri za wilaya zinatoa na wafanyabiashara waoga wanachangishwa . Bado EPA wanazo kwiba , kuna michango ya wabunge inayoenda makao makuu ya Chama. Fedha zote hizo zinakwenda wapi kama sio hizo wakina Migulu wameanza kuzitawanya huko Arumeru? hivi ni kwanini basi mtu wa CCM asione tabu kuuwa mtu ili mradi awe tu kiongozi?
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lakini cdm hawachangishi michango yao kwa 'mtutu wa bunduki' kama nyie m.a.gamba.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  SISIEM wanamiliki rasilimali nyingi sana za umma hawatakiwi kuendelea kuwakamua wananchi mpaka tone la mwisho. On top of that walishajichangishia siku nyingi kutokea EPA, Kangoda, Meremeta n.k. kupitia kwa mafisadi. Wanachotakiwa kufanya ni kwenda kwa mafisadi na kuchukua akiba yao mpaka zitapoisha.
   
 15. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Acha jazba m2 wangu. mimi naulizia tu haya mapesa yote yanakwenda wapi? kama si unyonyaji wa wazi? Kama ni makadi yao tunanunua na kuyalipia ada! hizi nyingine zinakwenda wapi?
   
 16. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Haya matembezi yatakuwa tarehe ngapi? Je fomu hii ni namba ngapi kati ya zote zilizotolewa? imetolewa na nani kwa jina halisi?...anyway hizi ndio loopholes za kuzitumia

  Nimeiweka kama kumbukumbu kwa wanangu na vijukuu
   
Loading...