Umewahi kubadilisha maisha yako kwa kupitia pesa za betting?

Kraftwerk

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
227
321
Habari wana JF.

Hivi ni kweli watu unapiga pesa kupitia company za betting au kubashiri kuhusu mpira au baadhi ya michezo mengine.

Kikwel sijawh kuon mtu kapata pesa kupitia betting wala sidhn na kuna watu unapiga pesa kwel au ni maisha yao ya kila siku.

PESA ZA BETTING YAMEWAHI KUBADILI MAISHA YAKO?
 
Wapo watu wamepiga mshindo, kuna jamaa yangu milioni 34 na chenji zake,wapo wengi wamepiga hela nawajua mie niliwahi kupata milioni 2 na chenji, milioni 1 point kadhaa mara 3 na vilaki laki zaidi ya mara 4

Tuje kwenye kubadili maisha.. binafsi betting haijanibadilishia maisha zaidi ya kunifilisi, mpaka nikaamua kuacha mwenyewe.
 
Nimenunua kiwanja kwa hela ya betting ...nimeanza ujenzi kwa juhudi zangu ,majuzi tena nikapunga nipo namalizia finishing.

Tatizo hela za betting inakuja kwa bahati ,kwenye hali ya kujipongeza unakuta imeisha . Hela yoyote ukipiga fanya uamuzi fasta
 
Maisha Ni mipango,mikakati hivyo lazima uheshimu Kila pesa unayoingiza bila kujali umepata kwa njia gani

Kuna mtu anaiheshimu laki nne anayoipata kwenye ajira yake,

Labda kwakuwa kawekeza muda mwingi takribani siku 27 kwenye kazi yake

Cha ajabu haiheshimu milioni nne aliyoipata kwenye betting

Kwakuwa ame stake elfu hamsini na kashinda milioni nne ndani ya muda mfupi

Unabashiri asubuhi jioni unapiga Hela zako yaani Ni mtaji kidogo faida nyingi kwa masaa

Hapa kwa haraka huwezi kiheshimu hii pesa uloshinda kwakuwa pengine hujaitolea jasho kivile

Hapa Ni Bata kwa sana na ulevi mwingine mwingi.

Iko hivi asikwambie mtu Ni rahisi kupanga bajeti zako kwa kutegemea mshahara wako wa mwezi ujao lakini ni ngumu kupanga bajeti kwenye Hela ya kamari ambayo hujui utapata au laa
 
Indeed
 
Halafu hela za fasta hivi za kupiga bila kutegemea unakuta mtu anaanza kujitosa tena ili apige pakubwa ,na ukishakuwa na hela kwa mda huo huangalii options zenye risk ndogo we unataka faida kubwa zaidi ,mwisho wa siku inaisha tena huko huko ,unatakiwa ukipiga hata mil 2 fanyia kitu kwenye mtaji endelea kama mwanzo kama unabetia buku mbili
 
Betting inafilisi vijana hakuna pesa ya haraka ikafanya maendeleo kwa kuwa maendeleo ni PROCESS endelevu.

Wengi walioshinda fedha za haraka utakuta hakuna kitu cha maana wanafanya na hata akifanya kwakuwa hakuwa na malengo nacho utashangaa hakidumu.
angalia waliochinda BBA, BSS na wengine walioshinda 100M kwenye kubashiri huishia kuzitumbua na kurudi tena mtaani
 
Wapo wengi tu,ila ukipiga mpunga mrefu wa beting tuliza kichwa na uhame chaka ukiendelea kubeti unaisha.
Dogo langu alipiga 25 milioni akanunu brevis ya kupigia misele huku akiendelea kubeti, mzigo wote ukarudi kwa Kanji Bhai akapaki gari maskani kakosa hata pesa ya mafuta Kima yule.
 
mimi sio mbetiji but kuna jamaa namfahamu tena hakuwa hata anajua kubet ila alikua anakuja kwa jamaa mtaani anabetisha kwa mashine zile anachagua game sio zaidi ya 3, then anaweka si chini la kaki 3 mpaka 5 nadhani asee jamaa alianza ujenzi kabisa maana alikua kula million 2 au 3 mpaka 5 ni kawaida sana kwakwe.
so nadhani inawezekana kinachosababisha vijana wengi wanaobeti wasile ni pesa huwezi kuweka timu 20 uweke jero upate milion 15 hiyo ni bahati nasibu kweli kweli.
 
Uyo jamaa anabahati sana,eneo la kwanza kwenye beting ni kuwa na bahati alafu kingine mtaji na ujue kubeti.
 
Kuna Mwamba hapa kitaa ni jamaa yangu kabisa mwaka 2017 alipiga million 7 alifungua duka na saiz yuko mbali Sana duka limekuwa kubwa saiz kafungua na mgahawa kaajir watu ,Ila tokea apige Ile Pesa aliacha kabisa kubet ,had Leo hatak kabisa habar za kubet.

Yeye anasema mungu alinipa kwa njia hiyo sasa Sina haja ya kubishana na mungu kuwa hela ulionipa kwa njia hii haitoshi ,Zaid hiyo Pesa anaiendeleza kwa style hiyo na Ana nidham na Pesa yake hakuna mfano.
Mambo ya Pesa Ni nidhamu tu IL wadau kadhaa imewapa maisha ingawa walio wengi inazid kuwafilisi siku had siku
 
Back
Top Bottom