tunakumbana na misukosuko ya hapa na pale, mojawapo ni kupatwa na aibu mbele za watu, tena isiyo yako. ngoja nishee nanyi kisa kimoja cha aibu nisiyoitarajia katika vingi kiasi vilivyowahi kunikuta. Samahani kuna maneno ya ukakasi kidogo!
imenitokea juzi mkoani Lindi. nilikuwa katika guest moja hivi inaitwa south honour. baada ya kupewa tu chumba nikakimbilia uani sababu nilikuwa nimebanwa na haja ndogo ile mbaya. kufika nakuta choo cha sinki kimechafuliwa vibaya, kuna kimba moja na nusu limegoma kwenda na maji. nikaona sio kesi si nitalisukuma tu na maji nikimaliza kujisaidia hiyo haja ndogo! ebwana yalinikuta.
kila nikimwagia maji yanaenda yenyewe tu hakuna zaidi. ndoo kama tatu ziliisha. nikashindwa, nikizingatia kuwa sikuharibu mimi nikaamua kutoka zangu. nje nakutana uso kwa uso na dada mhudumu akiwa amejianda kuanza usafi vyooni maana ilikuwa asubuhi sana. nikaendelea na hamsini zangu.
Ile nafunga mlango wa chumba ili niwahi kutoka kuwahi appointment fulani, naisikia sauti ya yule dada (mwenye uonekano wa kimcharuko kwelikweli) akinijia kwa kasi huku akifoka, ''we kaka huu ustaarabu gani, mambo gani haya ya aibu unatufanyia? likinyesi lako uliloliacha pale akalisafishe nani? kwa hela gani unayolipa hadi utufanyie mambo ya kinyaa namna hii?''. alimwaga sumu nyingi yule dada balaa, watu wote walijua kinachoendelea. kutokana na mazingira nilishindwa kabisa kueleweka na hivyo ikanibidi niondoke na aibu yangu tu. hivyo ndivyo nilivyoaibika kizembe kwa kosa lisilo langu.
karibuni!