umewahi ishi mazingira haya

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
13,087
15,981
vax.jpg

pata picha ndo unakaa humo ndani,jamani tumetoka mbali sana.
 
Da! mkuu inaonekana wewe ni wa kishua sana!
Mbona hiyo nyumba ni ya kawaida tu ndugu yangu!!
 
mode fungieni huyu mutu ananikumbusha machungu ya maisha yangu.
 
Wewe umezaliwa wapi na unaishi wapi? mbona nyumba safi tu hiyo kibongobongo!?
Kule kwetu hapo panaitwa Mabatini.
Amini usiamini viongozi wetu wengi ambao sasa hivi wanalilia mabwawa ya kuogelea kwenye nyumba za kuishi za serikali wamezaliwa kwenye nyumba mbovu kuliko hiyo, Lakini wanajifanya wamesashau.
 
Hiyo mbona iko kiwango mazee. zile za kule kwetu juu makuti na mlango wa matete ndio chimbo tulikotokea mwana!!! usione tunajishebedua na vi-harrier mjini huku...ndio maana tunamaliza miaka kibao mtu hujatia mguu kwenu..
 
siwe muongo sijawahi

Unataka kuwambia watu kuwa wewe huna kwenu huko Vijijini ?silazima uwewe unaishi humo siku nenda siku rudi lakini unapokwenda vijijini kwenu kuna wazazi wa wazee wako ambao wanaishi katika nyumba kama hizo na unapowatembelea japo siku moja unabaki hapo kwa kuwajulia hali ,au wewe ndio miongoni mwa wale wanao kana makabila yao na lugha zao kwa kisingizio hawakelewi na wanaongea swahili (hafu)na kuishi mjini
 
Nguli hii nyumba ni poa tu mbona, tena imeezekwa kwa bati - nilidhani ya nyasi. Mlango ni wa kufunga - nilifikiri utakuwa ile wa kuegesha unakandamizia na kigogo cha mti ili usipeperuke na upepo.

Hapa naona ni fresh tu mbona.
 
unajua kwann tunafell mitihani?hatufati instruction"tumeulizwa umewahi kuishi mazingira hay?sio kutembelea
Unataka kuwambia watu kuwa wewe huna kwenu huko Vijijini ?silazima uwewe unaishi humo siku nenda siku rudi lakini unapokwenda vijijini kwenu kuna wazazi wa wazee wako ambao wanaishi katika nyumba kama hizo na unapowatembelea japo siku moja unabaki hapo kwa kuwajulia hali ,au wewe ndio miongoni mwa wale wanao kana makabila yao na lugha zao kwa kisingizio hawakelewi na wanaongea swahili (hafu)na kuishi mjini
 
mode fungieni huyu mutu ananikumbusha machungu ya maisha yangu.
he he hee,mkuu lazima ukumbushwe maana mnajisahau sana mkijua kubonyeza keyboard.lakini juzi si ulitoka maeneo hayohayo kilosa ama?
 
View attachment 8751

pata picha ndo unakaa humo ndani,jamani tumetoka mbali sana.

Wewe babu kijana kwani hapo shida ni nini ni hiyo miti? Nyumba kama hizi zipo kibao hapa Dar tembelea tandale, manzese na kwingineko infact utazikuta zingine zimechoka kuliko hiyo. Tena watu wengi wanaoishi nyumba kama hizo wanavaa sana zile fulana za "bora maisha kwa kila mtanzania"
 
Kwa watanzania wengi hii ni nyumba inayozidi viwango vyao......
 
Best kule kwetu kiruruma mbona hii nyumba safi kabisa, afadhali mwenzetu ushatoka huko. Wengi wetu bado tuko hapo. Kijijini kwetu mwenye nyumba nzuri kama hii ni hedi ticha tu!
<input id="gwProxy" type="hidden"><!--Session data--><input onclick="jsCall();" id="jsProxy" type="hidden">
 
Nimegundua kuwa humu kuna watu wa dot com, hii ni nyumba ya maana sana, ebu nenda Dom, Singida nk, mbona hii ni ya kitajiri sana tena ina bati!!!!!! we vipi?????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom