Umewahi fedheheka?

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Mimi na rafiki yangu siku moja tulifedheheka vibaya, ilikuwa hivi; Enzi zile tukiwa shule, Wakati wa likizo nilikwenda kwa rafiki yangu kumtembelea kwao. Home kwao kulikuwa na nyumba kubwa na kila mtu na chumba chake. Jamaa shule tulikuwa tukimwita pastor like boy, kumbe jamaa anazuga. Baba yake alikuwa mchungaji pale kijijini kwao. Mchana wa siku ya pili tulikuwa peke yetu pale kwao, tukala chakula,kumbe jamaa ana vibotro vichache chini ya uvungu wa kitanda. Tukashushia. Mtoto wa kaka yake mkubwa kumbe aliona vile vibotro, akauliza nini hiki baba mdogo,akajibiwa haya ni maji. Dogo akatulia.

Jioni wakati tuko mezani karibu familia nzima tunakula, mzee akaomba aletewe maji ya kunywa, kale katoto kakachomoka fasta kwenda chumbani kuchukua maji ya ilala. Sisi tulishasahau kuwa tulikalia bomu. Kakafika pale kumpa babu yake ashushie. Kisia nini kilitokea?

Yule mzee alisema, kijana( yaani mimi) unaniharibia mwanangu. Usiku ulikuwa mrefu sijapata kuona, sijakanyaga pale mpaka leo. :angry:
 

Fab

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
763
14
pole sana mkuu ila mie najiskia kucheka..hahaaha!hilarious!
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Kumbe na wewe ulikuwa unajificha! Hakuna aja ya kufadhaika

Kweli nilikuwa najificha, tatizo ni pale yule mzee alipodhani mimi ndio mwalimu wa mwanae ktk haya mambo ya vibotro, kumbe mwanae ni member mzoefu.
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Mkuu, pole sana.
I can very well understand the emotional turbulance you went thru !!

Nikikumbuka mkuu huwa nachoka, ilikuwa saa mbili jioni na inabidi nilale pale na baada ya msosi kuna maombi kabla ya kulala, maombi ni kwa familia nzima pamoja na wageni. acha kabisa mkuu.
 

hsigira

Member
Nov 23, 2010
8
0
Najua kilichokufedhehesha ni utoto, na maneno ya mchungaji. Pole sana. Kwa kuwa sasa umekua kama mzee yupo kaza kamba mwelezee hali ilivyokuwa.
 

Dreamliner

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
2,036
209
Nenda kamsalimie na umkumbushe yaliyojiri wakati ule.. Huyo jamaa yako bado yupo? Pole sana...
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Najua kilichokufedhehesha ni utoto, na maneno ya mchungaji. Pole sana. Kwa kuwa sasa umekua kama mzee yupo kaza kamba mwelezee hali ilivyokuwa.
Mkuu umesema kweli kabisa, mimi nilishaacha vibotro muda mrefu sana, lakini mwanae/rafiki yangu anachapa maji hadi basi. Siku moja nilionana na dada yake nikampa ukweli wa tukio. Nikimwendea nitaamsha hasira zake bure.
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,710
3,695
Nenda kamsalimie na umkumbushe yaliyojiri wakati ule.. Huyo jamaa yako bado yupo? Pole sana...

Jamaa bado yupo, na mzee bado yupo na nguvu zake. Kisa cha kuandika historia hii ni kwa sababu nilitaka siku moja niende kumsalimia mzee yule, lakini nikimwona jamaa yangu alivyo chapombe nakosa nguvu kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom