Umewahi chapwa fimbo na mama mzazi? Hakuna kama Mama

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,774
Kuelekea siku hii muhimu duniani,inasemekana mama mzazi kumchapa mtoto wake aliyemzaa mwenyewe huwa anahisi maumivu sana ila anakuwa lengo la kumfundisha adabu tu..Mimi mpaka kufikia umri nilio nao Nina familia sasa nakumbuka mama yangu aliwahi kutumia fagio la nyasi kunichapa Mara moja tu baada ya kumdungua mdogo wangu kwa manati nusura nimtoe jicho.. tuvute kumbukumbu wenzangu au nyie hamkuguswa kabisaaa...
 
Happy mchanganyiko Wa baba Na mama uliomfanya mtoto. Hongera baba rijali uliemtengeneza mama shujaa!!
 
Na: Simon Ngusa Jilala
TAFAKURI.

Ni kweli tunaukumbuka usemi wa "Hakuna kama Mama" kila mara.

"Hakuna kama Mama" iwe katika vitendo zaidi kwa sisi Watoto.

Mama ana huruma kubwa na watoto wake haijalishi umri gani unao, lakini Mama ni Kimbilio kubwa sana kwa Watoto. Ukipata changamoto za kidunia Mama ana huruma zaidi na zaidi. Na Wakina Mama huwa wanaomba usiku na mchana ili tufanikiwe katika maisha yetu kuanzia kwenye familia mpaka katika Jamii tunazozitumikia.

Je, tunawachukuliaje Wakina Mama/Walezi kuanzia kwenye familia zetu yaani wake zetu ukiacha wazazi au walezi wetu???

Kila mara unampiga mke wako pamoja na kumtukana matusi ya wazazi wake bila kujiuliza dhamani yake ndani ya familia yako ilivyo. Kama anakuuzi kupiga si suluhisho kaa na uongee naye uone kwa nini kama anakosea inawezekana chanzo ni Wewe au Yeye, kama chanzo ni Yeye basi tafakurini kwa pamoja namna ya kutatua lakini si kupiga na kumzalilisha kila mara tena mbele ya watoto wake.

Mke wako a)anakupikia chakula unakula b) anakufualia Nguo unapendeza c) analea watoto katika maadili mema wewe unaangalia Mpira wa Asernal, Real Madrid, Machester United, Bacerlona n.k d) Anafanya usafi wote wa mazingira ya nyumbani

Kwa upande wa Mama zetu au Walezi wetu na siku ya Wakina Mama Duniani nako ni changamoto kubwa kwetu.

Mbaya zaidi Mzazi wako kwa mfano yaani Mama au Mlezi wako akikuomba msaada visingizio kibao wakati unaonekana una uwezo wa kumsaidia kwa kile ambacho anataka msaada. Hata kama huwezi kwa sasa mara nyingi humuelezi kwa lugha nzuri na ya kutia matumaini.

Leo hii kwa sababu ya kuitwa SIKU YA WANAWAKE umeomba picha ya Mama yako/Mlezi wako kwa Ndugu zako maana wewe huna picha ya Mama/Mlezi kwenye simu yako zaidi ya michepuko. Na leo imebidi uombe picha ya Mama/Mlezi ili utumiwe na uiweke Facebook,Twitter, Instagram, BBM.

"Hakuna kama Mama" iwe katika vitendo kwa sisi watoto.
 
mamu.jpg

MWANANGU SITAKABARI(SIKU YA MAMA)
1.
Mwanangu ewe mwanangu, leo nataka kulonga
Kila jambo lina Mungu, heri na shari hupanga,
Tamu ligeuke chungu, asali iwe pakanga,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
2.
Mwanangu sicheke ufa, kumbuka kuna Jalia,
Siringe kutaka sifa, kiburi ukajitia
Aliye na afya hufa, mgonjwa akabakia,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
3.
Mwanangu hebu elewa, nakuomba zingatia,
Ugonjwa ni majaliwa, mauti ni yetu njia,
Hupona mkusudiwa,hufa mshika jambia,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
4.
Mwanangu naomba shika,nisemayo sio siri,
Haya yamethibitika, kitambo tena dahari,
Mbichi unanyauka, mkavu una nawiri,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari
5.
Mwanangu sifanye ngenga, usitambie ukwasi,
Mambo ukiyabananga, tamkufuru Qudusi,
Mbio hushinda kinyonga, aachwe mbali farasi,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
6.
Mwanangu usiwe chizi, cheo huwezi miliki,
Nataka ujue wazi, hakina hatimiliki,
Chifu awe mjakazi, mtumwa awe maliki,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
7.
Mwanangu yana Karima, kupanda hata kushuka,
Uwende mbele na nyuma, ufanye unavyotaka,
Mla chunga hula nyama, mla nazi hula daka,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
8.
Mwanangu sicheke mamba, nawe mto hujavuka,
Kwa kiburi ungatamba,hupindui la Rabuka,
Hukosa aliyeomba, hupata asiyetaka,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
9.
Mwanangu sifanye inda, aliyepewa kapewa,
Ujue heri ya shinda, kiumbe ulojaliwa,
Ukijua vya kutenda, sisaahu kutendewa,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
10.
Mwanangu niendelee, ama kikomo nitie,
Nilosema sichezee, wallahi sipuuzie,
Kitaka uogelee, wasia uzingatie.
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.

Pichani ni mama yangu mzazi, kwasasa ni marehemu na amefariki tangu mwaka 2000. Kwangu ndio kila kitu, nampenda sana mama yangu, ila Mungu amependa zaidi kiasi amchukue, nimetunga shairi hili maalum kwaajili yake, najua maneno hayo alitaka kuzungumza lakini muda haukuwa rafiki kwake.

Leo nayasema kwa niaba yake nikiambia nafsi yangu, naam, nafsi yangu isitakabari kwani dunia ndio hii na kwa vyovyote vila hayana budi.

Dotto Chamchua Rangimoto.(Njano5)
whatsapp/call 0622845394 Morogoro
 
mamu.jpg


NISIKIZE MWANANGU (SIKU YA MAMA)
1.
Nisikize ewe mwana, haya ninayo ongea,
Hali yangu mbaya sana, mwenyewe wajionea,
Tumaini sina tena, sioni pa kuponea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
2.
Nisikize kwa mapana, yapate kukuelea,
Usikughuri ujana, uzee wakungojea,
Leo mtoto wa jana, sicheze pata potea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea
3.
Nisikize we kijana, ulipo nimetokea,
Mapito yangu ya jana, siwezi kuyaendea
Sina nguvu za ujana, nilipo waelekea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
4.
Nisikize tena sana, muda usije chezea,
Lile la kuwezekana, lifanye sije ngojea,
Kamwe haurudi tena, muda ukishapotea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
5.
Nisikize nina nena, shika usije kosea,
Sijawahi kupa gana, ulevi sijakugea,
Nataka uchunge sana, njia unayo endea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
6.
Nisikize kwa maana, dunia yachechemea,
Muabudu Subhana, kwa hofu kunyenyekea,
Usiku ama mchana, ibadani elekea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
7.
Nisikize wangu mwana, mamayo najiendea,
Huna baba wala nina, uanze jitegemea,
Cha kukupa nami sina, usia wangu pokea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
8.
Nisikize leo mwana, andika nilo ongea
Riziki sio dafina, si kamari taotea
Yataka juhudi sana, siketi ukangojea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
9.
Nisikize wako nina, ninayosema rejea,
Kuna neno la mtana, usiku lenda potea
Ujifunze kunong’ona, na siri kujiwekea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.
10.
Nisikize tena tena, upate kuendelea,
Ukakope kama huna, mtaji kuongezea,
Ukishikwa shikamana, mbeleko sije chezea,
Sijiwezi sitapona, kaburi laningojea.

Dotto Chamchua Rangimoto.(Njano5)
whatspp/call 0622845394 Morogoro
 
Mama atabaki kuwa Mama, Japo sikumfaidi sana ila miaka 10 niliyobahatika kuwa naye nilitambua thamani yake.

Mungu bariki wakina Mama wote.
 
Nimefurah kuona Dp za watu zikipambwa na Picha za Mama zao bila kusahau Bonge la status ikisindikizwa na Neno la *Happy Mother's Day au #Ahsante Bi Mkubwa*



Swali ni Je Mama ataonaje huo Ujumbe ikiwa Smartphone ulimnunulia Demu wakoo?? ....


*Think Big* Hakuna kama mama
 
Wabongo hawaishi kuwashangaza wenzao...
Wengine wameandika ILOVE YOU MAMA...wengine wameandika ujumbe mzito na kumalizia NAKUPENDA SANA MAMA YANGU..wakati ukiangalia post zao zao za TBT zinachukiza kama siyo kuwazalilisha wamama au wanawake wenzao......lakini najiuliza ni wamama wangapi wanauwezo wa ku-access mitandao hii ya kijamii...kama Insta, FESIBUKU...TWIRA n.k

Siyo siri iwapo mama zao wana-access kwenye account zao basi watakuwa ni wamama wa ajabu kupitiliza coz mabinti hawa wanaojifanya kuwarusha kwenye hiyo mitandao na kutafuta kiki...wengi wao wanaongoza kwa kutupia picha za nusu utupu au za makalio yao..
SASA najiuliza..Je wamama hawa huwa hawawakanyi...?

Am so confused kwakweli....
 
Si kichapo ni kufinywa, lakini ninajuwa mimi ni special kwake. Mdingi hajawahi hata kunifinya, kwakuwa ni kitenda mimba. Kichapo nilichezea kutoka kwa makaka, hata madada walinidekeza kwakuwa wao walikuwa wakubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom