Umesoma vitabu gani mwaka 2021?

Ancient Greek Tales.

Wengine ni Hekili, Yasoni, Anteo ,Orpeo(malenga) na Atlas. Pia wapo miungu wa kiume na wa kike(gods and goddesses) bila kuwasahau mazimwi(monsters) kama Gorgo na dada zake, joka la Andromeda na Sirens, wale wadada watatu ambao sauti zao tamu huvutia meli kuvunjika juu ya miamba.

Utajifunza mengi na kuburudika zaidi kama utasoma The Iliad na The Odyssey vya Homer. PDF zake zipo google.
Nashukuru sana mkuu,namaliza mwaka kwa burdan taam ya hivi vitabu.
Ubarikiwe mkuu
 
Sites zipo nyingi. kuna app nyingi sana za vitabu vya bure kama light reader au ReadEra. Vingi ya hivyo vya kiswahili vipo maktaba app. Kununua mi nanunua kwenye app ya kindle, bei ni afadhali.

Hiz app znapatkana kwenye ios?
Maana me nshatafta sana bila mafankio jaman
 
Kaka, nami nashare orodha hiyo hapa Chini, ingawa vingi nimeviacha kwa kuvisahau. Mwakani nitaanza weka record sawia.

Usomaji wangu wa Vitabu mwaka 2021.

Hatimaye, kwa baraka zake Mungu Mkuu, tunaelekea kuumaliza mwaka 2021 na kuunza mwaka 2022.

Kama ilivyo ada, kwenye jamii ya usomaji vitabu, kushirikisha vitabu ulivyosoma ni utamaduni muhimu na wenye manufaa makubwa hasa kubadilishana vitabu, kutambua vitabu na kuhamasisha usomaji vitabu zaid kwa wengine na kwa mshirikishaji yeye mwenyewe binafsi.

Sikumbuki idadi ya vitabu Nilivyovisoma kwa sababu sina utamaduni wa kuweka lengo la idadi ya kusoma kwa sababu siku zote husoma, usomaji imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

Tofauti na mwaka jana, mwaka huu nimesoma Riwaya nyingi (hasa za waandishi wa kiafrika) na nitaendelea zaidi kusoma Riwaya nyingi za kiafrika kwa sababu zina mguso wa moja kwa moja na zinaakisi zaidi. Pia nimesoma vitabu vya kujijenga binafsi vingi zaidi mwaka huu kuliko miaka kadhaa nyuma. Lakini bado vitabu vya Historia, Siasa na siasa za kimataifa bado vimeendelea kuwa aina ya maudhui ninayapendayo zaidi.

Hivi ndio orodha ya baadhi ya vitabu nilivyosoma mwaka 2022.

Changes; A love Story ya Ama Atta Aido.

Riwaya hii ilitoka mwaka 1991, lakini maudhui yake bado yanaakisi Ulimwengu wa sasa. Riwaya hii inaelezea kisa cha mwanadada Esi ambaye anapambana kukidhi maisha ya ndoa katika Tamaduni za kiafrika na uislam kama mwanamke msomi na mwenye kuipenda kazi yake. Kwenye Riwaya hii inafunza kuhusu mitazamo ya wanawake juu ya ndoa, kazi na ndoa, mapenzi na familia.

The Girl with the Louding Voice yake Abi Adere.

Riwaya hii inaelezea kisa cha Binti aliyezaliwa na kukulia kwenye maisha ya hali ya chini, ambapo anaozeshwa na baba yake kwa lazima [kinyume kabisa na utashi na ahadi aliyompa marehemu mkewe] ili tu baba apate fedha na huduma kutoka kwa mkwewe. Akiwa ndani ya ndoa ya mtaala, analazimika kukimbia kijijini kwao baada ya mke mwenza kufariki huku yeye akihisiwa kuhusika. Katika kukimbia huko anaishia kupata elimu inayomkomboa. Riwaya hii inasisitiza juu ya elimu kuwa ndiyo nyenzo ya kuwapa sauti watoto wa kike kwenye jamii.

Sooley, Riwaya yake John Grisham
Riwaya hii inaelezea safari ya Kijana Sooley kutoka kwenye maisha ya kijijini na vita huko Sudan Kusini anayefanikiwa kwenda nchi Marekani kucheza mpira wa kikapu na hatimaye maisha yake kukatishwa masaa kadhaa kutoka kuanza safari yake ya mcheza kikapu wa kulipwa kutokana na kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi na kufariki. Riwaya hii inaakisi Maisha kwenye nchi zenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, sekta ya mpira wa kikapu Marekani hasa vyuoni, maisha ya kijamii nchini Marekani, na changamoto ambazo watu maarufu wanavyozungukwa nazo hasa starehe zinazoambatana na mafanikio. Somo kubwa kwenye riwaya hii ni namna ya kuwianisha mafanikio na misukumo hasi ya maisha inayokuja sambamba na mafanikio.

Ikigai: The Japanese Secret to a Long and Happy Life chao Francesc Miralles na Hector Garcia
Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti wa waandishi katika kijiji cha Ohgimi huko Okinawa, Japan kubaini kwa vipi watu wa kijiji hicho huishi maisha marefu zaidi (90–100 yrs). Kitabu hiki kinaeleza mifumo ya maisha, ulaji, ufanyaji kazi, familia, imani ya watu wa eneo hilo. Mafunzo kwenye kitabu hiki ili kuwa na maisha marefu; kuwa na lengo la maisha, lala vya kutosha (masaa 6–7 kwa siku, isiwe mchana—mchana usilale zaidi ya dakika 20), kula 80% ya tumbo lako, lala masaa mawili baada ya mlo wa usiku, kuwa na mwili active muda wote, kuwa na shughuli ya kukutoa jasho kila siku—bustani ni jambo jema, mazoezi ya kila siku n.k., epuka msongo wa mawazo, jichanganye na watu, epuka imani zinazokupa msongo wa mawazo, epuka kabisa kula sukari (walau miwa).

Left to tell; Discovering God Amidst the Rwanda Holocaust chake Immaculee Ilbagiza.

Kitabu hiki ni simulizi ya kumbukumbu za kisa cha Binti huyu wa kitusi, akisimulia madhila aliyopitia wakati wa janga la mauji ya kimbari mwaka 1995 huko Rwanda. Kwenye kitabu hiki, Immaculee anaelezea jinsi gani alivyoishi kwenye chumba kidogo cha Choo, yeye na wenzie sita kwa muda wa miezi mitatu kuhofia kuuliwa. Mambo mengi yameelezwa; mifumo ya kibaguzi ilivyokuwa ikiratibiwa na serikali ya habyarimana, jinsi gani wafaransa walikuwa wakiwaunga mkono wauji wa kihutu dhidi ya watutsi.

MBS:Rise to Power of Mohammad Bin Salman cha Ben Hubbard.

Nilitamani sana kumfahamu MBS. Bila shaka huyu ni mmoja ya watu wenye nguvu sana mashariki ya kati kama si ulimwenguni. Machache sana yanafahamika kuhusu yeye, angalau kitabu hiki mwandishi amejaribu kumuangazia ni nani huyu bwana. Nilivutiwa sana na maono yake ya kisekyula, na mpenda mabadiliko ambaye kwa kweli anafaa kuwa kiongozi wa Saudi yenye muelekeo mpya wa maisha nje ya utegemezi wa mafuta—Saudi2030. Pia humu ameangaziwa kama kiongozi mwenye maono makali sana, kiasi cha kuwa katili kwenye kutekeleza ayatakayo—ukiukwaji wa haki za kiutu kwenye vita huko Yemen, kuwazima wakosoaji wake kama Jamal Khashoggi (humu ameeleza jinsi gani yalivyoratibiwa mauji hayo).

Powers of Geography chake Tim Marshalls.

Kitabu hiki ni muendelezo wa kitabu chake cha Prisoners of Geography (ambacho alielezea jinsi gani jiografia imetengeneza siasa za dunia ya leo Kihistoria). Katika kitabu hiki ameelezea maeneo Kumi na namna gani ambavyo siasa zake zitatawala dunia yetu kwa miaka kadhaa ijayo. Maeneo hayo ni Ethiopia, Uingereza, Iran, Saudi Arabia, Uturuki, Australia, Ugiriki, Hispania, Sahel na Anga. Kitabu hiki kimetoka mwaka 2020, na mfano Ethiopia ameeleza namna gani ujenzi wa bwawa la GERD na sera ya kuinganisha Ethiopia italeta machafuko na Wanamajimbo kitu kinachotokea sasa kati ya Tigray dhidi ya Abbiy Ahmed. Pia, ameeleza namna ambvyo Vision ya Erdogan kutaka 'kuifufua' Ottoman Empire, itaipa uturuki utawala siasa za dunia, mfano kwa sasa anaeneza ushawishi wake huko Ethiopia. Sura yenye upekee ni kuhusu mivutano ya wakubwa wa dunia kutaka kutawala anga la dunia.

Rumba on the River chake Gary Stewart.

Napenda muziki na ninapenda sana muziki wa Kongo—Kinshansa na Brazzaville. Hiki ni kitabu ambacho sikusita kukisoma. Stewart ametafiti na kuelezea historia ya muziki wa Kongo kutoka miaka ya 1880 hadi 1995. Ameeleza namna gani band na wanamuziki wameeibuka nchi hizo. Somo kubwa kwenye kitabu hiki ni kuwa, muziki wa Kongo umekuwa mkubwa na wa Kipekee kwa mambo manne—Jiografia yake, demografia, ukoloni na mchango wa kipekee wa Rais Mobutu Seseko.

Securing Democracy: My Fight for Press Freedom and Justice in Brazil, kitabu chake Glenn Greenwald

Hiki kwangu ni kitabu bora kabisa cha masuala ya kisiasa katika mwaka 2021. Greenwald ni mmoja ya waandishi ninawakubali sana kwa sababu mbili, moja si muoga pili ni mwenye kusimamia misingi. Mwandishi huyu ndiye aliyeshirikiana na Edward Snowden, kufichua udukuzi unaofanywa na serikali ya Marekani kwa raia wake. Mwaka 2014, Brazil ilifanyika Operesheni iliyoitwa Car wash, lengo lake ilikuwa ni kufichua na kuadhibu mafisadi nchini humo na hatimaye Rais wa wakati huo, Lula alifungwa. Wabrazil waliipongeza sana Operesheni hii kwani walichoshwa ufisadi. Greenwald anafichua kuwa, Operesheni hiyo iliongozwa na malengo ya kisiasa ya kumtoa madarakani Rais Lula, huku ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kisheria ukikiukwa mfano, mwendasha mashitaka mkuu, Moro alishirikiana na majaji katika kuratibu na kupanga ushahidi hatimaye hukumu. Greenwald alifanya ufichuzi kipindi hiki cha mtawala dikteta, Bolsonaro. Somo kubwa kwenye kitabu hiki, ni kuwa kama jamii inapochoshwa na watawala na mifumo yake, inahitajika tahadhali kubwa sana kuepusha wanasiasa wenye nia ovu kutumia hali hiyo kutimiza agenda zao za kisiasa.

Kane and Abel, Riwaya ya Jeffrey Archer. Riwaya hii inasimulia watu wawili, waliozaliwa siku moja, kwenye mazingira tofauti kabisa, mmoja akizaliwa porini na kuokotwa na muwindaji baada ya mama yake kufariki (Abel) na Mwingine kuzaliwa kwenye hospitali iliyokodiwa binafsi na familia, familia ya kitajiri(Kane), watu hawa wanakuja kutana baadae kwenye biashara na kuwa na vita kubwa za kibiashara, kisiasa na kifamilia.

Soldiers of Fortune: The Abacha and Obasanjo Years cha Max Siolun

Siolun anaelezea maisha ya siasa za Nigeria miaka ya 1980 hadi 1990 zilizotawaliwa na Mapinduzi ya kijeshi. Watu waliotawala siasa hizo ni San Abacha, Olusegan Obasanjo, Mashaka Abiola, Muhammad Buhari na Ibrahim Babangida. Kitabu hiki kinafunza sana sanaa ya mapinduzi namna gani inafanywa, mazingira na ufundi wote ulio ndani yake, huku Mwalimu Mkuu akiwa ni Ibrahim Babangida. Som kubwa kwenye kitabu hiki ni kuwa, nchi ikishapitia tu mapinduzi ya kijeshi, basi huwa ni ngumu kutoka kwenye hali ya ujeshi na kurudi kwenye utawala wa kiraia.

Kenya: Between Hope and Despair, 1963–2011 cha Daniel Branch.

Majirani ni taifa ambalo linakabiliwa na siasa zenye ukabila, mauji na ufisadi wa kiwango cha juu. Haya si mapya, Branch anaelezea kwa kwa mtiririko toka 1963 mambo haya yamekuwa yakitokea vipi. Somo kubwa nililolipata baada ya kumaliza kukisoma hiki kitabu ni kuwa, Nyerere alifanya kazi iliyotukuka sana ya kulijenga taifa la Tanzania. Kenya inahuzunisha sana.

Upheaval: How Nations Cope with Crisis and Change cha Jared Diamond.

Diamond ndiye mwandishi wangu bora kabisa wa masuala ya sayansi ya jamii. Kitabu hiki Diamond anaelezea njia 12 ambazo mataifa yanaweza zitumia [kwa kurejea mifano ya Kihistoria], katika kutatua migogoro inayokabiliana nayo. Njia hizo 12 pia Zinaweza tumika katika maisha binafsi ya mtu.

Why Sex is Fun cha Jared Diamond.

Humu Diamond anaelezea jinsi gani wanadamu tumepitia safari ya mabadiliko ya sexuality katika maelfu ya miaka kuwa hivi tulivyo leo. Kwenye kitabu hiki Diamond, anatulezea sisi wanadamu kwanini tunatenda jinsi tutendavyo inapokuja suala la ngono na Uzalianaji. Kitabu hiki kimenifungua mambo mengi ambayo sikuwa ninayafahamu, mfano sisi, wanawake wanakoma kuzaa wakifikisha miaka kuanzia 45, ili waendelee kuishi vinginevyo wangekuwa wanakufa sana kwa sababu ya complications za mimba na kuzaa. Pia ameeleza namna gani wanyama wengine wanatenda kwenye masuala ya kuzaliana. Mfano, wakati sisi wanaume tukishampa mimba tu mwanamke, kibaolojia tunabaki hatuna kazi tena, mbuni wao jike likitaga mayai basi dume ndio huwa linabaki na kazi ya kulea na mayai na watoto. Cha kufurahisha, wakati sisi tunaona wanyama wengine ni waajabu inapokuja masuala ya uzalianaji, sisi ndio tuna mifumo ya ajabu katika wanyama wote takribani 4,000.

Collapse cha Jared Diamond
Hapa Diamond anaelezea jinsi gani jamii mbalimbali mf Maya, Easter Ireland, zilianguka, na vipi jamii kama China au Australia ziko hatarini (kwa kipindi hicho cha mwaka 2005) ama jinsi gani jamii zilikabiliwa na misukosuko lakini zikafanikiwa kunyanyuka. Humu Diamond anaelezea mambo matano yanayoamua maanguko ya jamii—Uharibifu wa mazingira unaofanywa na watu, mabadiliko ya tabia nchi, uadui wa majirani, kusitishwa kwa msaada wa majirani na jinsi gani jamii yenye inachukua hatua juu ya madhila inayokumbwa nayo. Humu nilivutiwa sana na utafiti ulioonyesha namna gani uhaba wa ardhi ulichangia kasi ya mauji haya hasa kati ya wahutu kwa wahutu wenyewe mf eneo la Kanama.

50th Law of Power cha Robert Greene. Greene ndiye mwandishi wangu bora zaidi wa masuala ya stratejia. Miaka mingi sikuvutiwa kukisoma hiki kitabu hadi nilipopata msukumo kutoka kwa Paula Paul Hiki kitabu kinatoa mafunzo ya namna gani unaweza pambana katika maisha kutokana na mapito aliyopitia 50 Cent. Somo kubwa humu ni Kuushinda Uoga. Mafunzo yote kumi aliyoyaeleza Greene na 50, yanahitaji uushinde uoga ili uweze kuyafanikisha.

Vitabu vingine baadhi nilivyosoma ni

The world Untill Yesterday; What can we learn from Traditional Societies.

Blood safari riwaya ya Deon Meyer inayoelezea changamoto za uhifadhi.

Ninaendelea na kitabu cha Atomic Habit cha James Clear (Asante kwa Hekima Book Club kwa kunipa msukumo mwingine wa vitabu—Self Help Books, walau kila siku saa 11–11:30 asubuhi kabla ya kwenda mazoezini husoma vitabu vya kujijenga.

Mwaka huu nilitaka nisome kazi zote za Jared Diamond (nimebakisha kitabu chake kimoja tu—Third Chimpanzee, ambacho kinanitia uvivu sababu maudhui yake yametokea kwenye vitabu vyake vingine ambavyo nilishavisoma hasa Guns, Germs and Steel), mwakani ninataka nisome kazi zote za Yuval Noah, nisome zaidi Riwaya za kiafrika, Kwa umuhimu, Vitabu zaidi vya kijijenga binafsi [mwaka huu nimefanikisha kuacha pombe, baada ya kutoka kwenye 'kifungo’ hicho nimejikuta najiona upya na kutaka kujiimarisha zaidi kiafya], na pia tawasifu mbalimbali.

My sista Paula Paul Asante kwa uzi wako , pale nimepata vitabu vingi ambavyo nitavisoma mwakani, pia nimejifunza mengi kutoka kwako.

Mapitio ya baadhi ya vitabu nilivyovisoma, vipo kwenye uzi huu

Thread 'Vitabu vyangu bora vya nyakati zote. Vipi vyako?' Vitabu vyangu bora vya nyakati zote. Vipi vyako?
 
Hongera kwa uchambuzi mzuri wa vitabu ulivyosoma.
 
Hongera na shukrani sana mkuu. Hii list ntakuwa naipitia kupata cha kusoma. Ila nafikiri ntaanza na hicho Soldiers of fortune. Mwaka huu nimepita sana Nairaland kuona habari za wanigeria. Pia 2023 wanauchaguzi, na mambo tayari ni moto. Na kingine ni kuwa hao jamaa, kama Buhari bado wanaendesha hiyo nchi.
 
1. Rich dad, poor dad
2. The richest man in babylon
3. Atomic Habits
4. Rich Dad's Guide to Investing
5. The Alchemist

This year nimeanza na How to win friends and influence people.
images.jpeg-257.jpg
 
Wakuu me naomba mwenye soft copy ya vitabu vya mzee wangu MYLES MUNROE. Huwa naenjoy sana na kazi zake huyu father(RIP)
 
Nilipata kusoma kadha wa kadha-2021.

1.MARTIN JACQUES- When china rules the World,

2. HA-JOON CHANG:
a)The political economy of industrial policy,
b)Ecomics:the user's guide,
c)23 Things they don't tell you about capitalism,

3: KEVIN & ROBERT-The art of invisibility,

4:MICHAEL SWAINE & PAUL-Fire in the valley,

5: ANTONIO -CHAOS Monkey,
6:GEORGE.G.M.JAMES-Stolen legacy(greek philosophy is stolen egyptian philosophy)

7:TOM OLIVE-Nothing is impossible.

8: DYNAMO MAGICIAN:-a)Dynamo(the book of secrets)
b)Nothing is impossible.
 
1
9: AYAAN HIRSI ALI:
a)Infidel my life,
b)Heretic(Why islam needs reformartion now
c) The caged virgin.

10)PHIL ZUCKERMAN:
a)Living the secular life"new answer to old questions".
b)What it means to be moral" why religion is not necessary for living an ethical life"
.
11: DAN BARKER-Life driven purpose" not purpose driven life"

12:BART D. EHRMAN:-
a) TRUTH"-Fiction in thd davinc code,
b) HEAVEN & HELL - A History of the afterlife.

13.ERNEST BECKER:- THe denial of death.
 
FICTION BOOKS:
A CHRISTMAS CAROL by charles dickens.

b) ORIGIN by dan brown.

C)(Nimerudia kukisoma)PAMBAZUKO GIZANI by karumuna mboneko.

d) THE SICILIAN by mario puzo.

e) NOT MY THING by raimond.
 
Back
Top Bottom