Umesoma vitabu gani mwaka 2018?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,886
Wakuu ni mwisho wa mwaka tutumie hizi siku zimebaki kujitathmini usomaji wetu kama ilivyo deaturi yetu.

Mi usomaji wangi haukuwa mzuri. Nimesoma vitabu vitatu na vingine viwili sikumaliza.
1.A god who hate. Hiki kuna member Alisina niliona amekiupload.Nikakipakua na kikanivutia kusoma. Huyu mama muandishi anaeleza maisha ya mwanamke wa kiislamu na magumu yake. Pia anashutumu imani hiyo. Kinavutia na rahisi kusoma.

41smK42d3iL._AC_SY400_.jpg


2. 1984
Hiki kitabu nilianza kusoma muda ila mwaka huu nikashawishika kukimaliza. Ni fiction lakini kipo serious sana. Kinazungumzia ubaya wa ujamaa, serikali ya mabavu, uminyaji wa uhuru nk.Wakati wa Nyerere kilipigwa Marufuku sijui kama wamekifungulia.
1788282361.jpg

3.The Capitalist Nigger. Haka kakitabu kuna mdau alikaweka humu ndani. Ni katkitabu kafupi kama page 50. Kanazungumzia hali ya mtu mweusi hasa kiucgumi na kielimu. Kana idea nzuri ya jinsi mtu mweusi anaweza kukomboka. Ila kaba lugha kali.
images-7.jpg


4.Kitabu changu.Niliandika na kuchapa kakitabu mwaka 2013. Huwa karibu kila mwaka nakasoma. Na kila nikikasoma napata kitu kipya!!!

5.The man who mistook his wife for a hat.
Hiki kitabu nilianza zamani kusoma lakini sijakimaliza. Ni kitabu kifupi na kinavutia sana.Kinazungumzia wagonjwa wa akili wenye matatizo adimu na ya kushangaza.
41ZTiXcD3hL._AC_SY400_.jpg


6.The politics book.
Haka kakitabu kanaelezea historia ya siasa toka zama za zamani kabisa. kanaeleza kwa njia rahisi na fupi. Ni kazuri ila sijakamaliza bado.
61st5PRktiL._AC_SY400_.jpg


Malcom Lumumba , Kiranga Wick mitale na midimu Nalendwa zitto junior MSEZA MKULU et al
 
nimesoma vingi ila kitabu kinaitwa perennial seller -ryan holday imebamba list yangu ni kitabu kizuri sana
 
Nimesoma vitabu vifuatavyo :

1. Our Philosophy
2. Blasting the foundation of Atheist
3. Where is Allah
4. Reason,Revelation and Reconstitution of Rationality.
5. Ibn Taymiyyah against the greec Logicians
6. Defining Legends
7. Vitabu vya Lugha.
8. Vitabu vya Imani yangu (Uislamu)
 
nimesoma
1) Zetetic Cosmogony by thomas winship 1897
2) One Hundred Proofs That the Earth Is Not a Globe by William Carpenter 1885
3) Zetetic astronomy by Samuel Rowbotham 1865

vitabu hivi vimesaidia kutambua how deep we are under so many layers of lies in the world,kuanzia sisi binadamu ni nani,mpaka "dunia ni kitu gani"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom