Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 211
Nilikuwa natafuta kitu cha kuandika katika blogu yangu kabla ya kulala , nikafikiria wee , nikakosa basi ikabidi niende duka moja la madawa kuongea na mfamasia nipate hili na lile .
Nikakutana na kijana mmoja kamwita dada anayeuza dukani akamnongoneza kwamba anataka kondom , halafu akaanza kucheka kama vile amefanya kitu cha ajabu na kitu ambacho hakiendani na utamaduni wake .
Ni kweli kabisa vijana wengi wanaona kuomba au kuulizia kondom dukani ni kitu cha ajabu anafikiri labda jamii itafikiria yeye ni Malaya , mzinzi au muhuni hana adamu na kadhalika kwahiyo wanaficha kabisa inakuwa siri .
Nikamsogelea yule dada na kumwomba na mimi anionyeshe kondom akanitolea salama kondom 3bomba , raha na zingine nyingi , nikamuuliza mbona hizi raha condom siku hizi hazipigiwi muziki kama zamani ?
Daktari akaingilia kati akaniambia hizo raha condom zililetwa kwa ajili ya majaribio hata serikali inajua hilo lakini wao wanafanya siri kwahiyo niwe makini sana bora nichukue kondom za ulaya .
Tukaendelea na maongezi yetu , nikamwomba anipe zile za bure basi manake hizi za ulaya ni bei ghari siwezi kumudu , hizi raha zimeletwa kwa majaribio je zile za bure inakuwaje ?
Akaniambia pia zile za majaribio ni hatari zaidi hazijadhibitishwa hata na tbs angalia hata mabox yake kama yana nembo ya tbs au mamlaka ya madawa Tanzania hazina chapa yoyote ya taasisi hizo kwahiyo inakuwaje ?
Nikashikwa na kigugumizi ,
Yule mfamasia akaniambia bora niogope kuliko nimpoteze ninayempenda kwa kutumia vitu ambavyo havina havina uhakika katika matumizi yake .
Kweli nikapata kitu cha kuandika katika blogu yangu , elimu ya ukimwi inatolewa sana lakini hakuna aliyewahi kwenda kuhoja watu haswa vijana wanafaidika vipi na elimu hii au jinsi wanavyotumia elimu hii katika maisha yao ya kila siku
Si unaona anaogopa kuulizia kondom dukani ? angekosa hapo labda angeenda kufanya tendo la ndoa bila kinga na huo ndio ungekuwa mwanzo wa safari yake ya ndefu ya maumivu sio kwake peke yake hata kwa ndugu na jamaa zake .