Umeshindwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako?!soma hii nikupe tiba!

pageup

Senior Member
Oct 12, 2012
156
59
sport-girl08.jpg
MITANDAO YA KIJAMII

Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba, pamoja na kwamba mitandao ya kijamii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuendesha mijadala na kukuza ufahamu wa mambo mengi, suala la mapenzi limetajwa! Utakutana na mtu Facebook (mfano), mmekuwa marafiki, lakini siku ya siku anaanzisha mambo ya mapenzi. Kwa sababu umeshakuwa naye karibu kwa muda mrefu, umekuwa wazi kwake ni rahisi kuanguka!
Hisia za mapenzi wakati mwingine hudanganya. Ngoja niwaambie ukweli, unapokuwa unawasiliana sana na mtu wa jinsi tofauti na yako, hisia za mapenzi huwa kali sana, kiasi kwamba ukiambiwa tu unapendwa, ni rahisi kuingia mkenge!

Kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Facebook, BBM, Twitter na mingineyo maarufu kuna utamaduni wa kuweka picha. Wakati mwingine picha hudanganya…kwa haraka haraka mtu eti anasema amekupenda. Hakuna lolote zaidi ya kuwaza ngono tu! Huo ndiyo ukweli. Tatizo ni kwamba, huwezi kujua kama kuna hatari hiyo mbele yako. Unao marafiki wengi, mnataniana kila wakati, siku akilianzisha, inakuwa ngumu kuchomoka. Hata hivyo, kuna mambo madogo sana ukiyafanya yatasaidia kukutoa kwenye mtego.

Utakuta mtu ana mpenzi wake, mke au mume. Kifupi yupo kwenye uhusiano, lakini kwenye mtandao anaandika yupo ‘single'. Kwa nini hutaki kujulikana kuwa upo kwenye uhusiano? Hujiamini? Humpendi mpenzi wako au tatizo ni nini hasa? Rafiki zako wanapoona huna mtu kwenye maelezo yako, wanatumia nafasi hiyo kukutega. Kwa nini ujiweke kwenye mitego? Kama upo kwenye uhusiano, kuwa mkweli, andika.

Ikiwezekana sehemu ya kuweka picha yako, weka ya mpenzi wako au mliyopiga pamoja, hii itasaidia marafiki kukuheshimu na wale wenye tabia za kipuuzi kujitoa mapema. Wanaotumia mitandao ya kijamii ni mashahidi wa hiki ninachokizungumzia hapa
 
Unachoongea kina mantiki sana mkuu..!

Ngoja nijitoe kwenye mitego.. Asante kwa kutukumbusha..!
 
Huo ni ukweli mtupu ndugu,na wasichana wengi sana wamechezewa
 
Hapo kwenye kuweka picha ya mupenzi sidhani kama inasaidia.
Nina rafiki angu kaweka pics za kutosha za mshkaji, profile pic wapo wote lakini kazi za nje anazo za kutosha na kaka angu akiwa ni mmoja kati ya kazi za nje!!!!
 
tatizo sio marital status ya mtu katika.mtandao... tatizo ni KUPOROMOKA KWA MAADILI HASA KWA VIJANA WA SASA. unakuta mtu kaoa ama kuolewa lakini anatoka nje ya ndoa yake kisa kavutiwa na mdada/mkaka wa kwenye mtandao.
 
tatizo sio marital status ya mtu katika.mtandao... tatizo ni KUPOROMOKA KWA MAADILI HASA KWA VIJANA WA SASA. unakuta mtu kaoa ama kuolewa lakini anatoka nje ya ndoa yake kisa kavutiwa na mdada/mkaka wa kwenye mtandao.

hahaha heri mimi baadhi wananivutia kuwa marafiki tu na si wapenzi.... kama kwenye vikao vya kubadilishanamawazo kama kile cha siku ile nilichokimiss charminglady
 
Back
Top Bottom