Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.

Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo.

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba.

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa.

Nilikua na location 9, nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee.

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga"?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi.

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki.

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee.

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa.

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini.

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia.

Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza.

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi.

Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo.

Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta.

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Ilinitokea hiyo mkuu hahahahaaa mwaka 2005 mbona jamaa akinichaji Elfu 20 anioneshe duka !!! Pole mkuu na hongera kwa kupata mizigo yako salama.
 
Pantomath pole Sana mkuuu..next time nicheki kwa usaidiz nikupe na new machimbo. Wasap # 0765929586
 
Njia rahisi sana ya kufanya ni kuchukua contacts zao

Maduka yenyewe 9 hapo ungechukua namba zao kwani lolote laweza tokea na moja wapo ni hili la kusahau mzigo wa thamani umeuacha wapi

Lingine la kufanya ni kujua location kwa google map na kuweka point zako zote
Hii itakusaidia kwa mizunguko yako

Mimi miji yote ninayoenda kama natamani kutembea kwa miguu natumia ramani tu na itanirudisha nilipokuwa hata kama ni Paris
Wazo zuri nahisi jamaa alignore sababu ya haraka
 
Nimewahi poteana hapo Kariakoo mtaa wenyewe sio complicated
Lengo langu niende NMB nyuma ya kituo cha polisi msimbazi ,nimepanda costa natokea manzese ,badala ya Costa kupita fire ikakatisha mitaa ambayo siijui nadhan ni kwenye ofisi za mwendo kasi pale ila sikunote nilikuwa nimelala,
Tukaenda shushwa mitaa siko familiar nayo
Nikaona isiwe tabu nikachukua bodaboda nikampa maelekezo anishushe BIG BON
Nikapelekwa ila akili yangu ikagoma kbsa kuwa pale ni big bon ,
Petrol station naiona,na kituo cha polisi nakiona ,Ili viko upande tofauti na vinapotakiwa kuwa(KWA mujibu wa akili yangu)
Yaani mfano akili inaniambia kituo cha polisi kinatakiwa kiwe upande wa kushoto kwako mimi naona kiko Kulia kwangu ,nikadaka wenge
Najua kbsa Nmb wako nyuma ya kituo cha polisi ,ila akili yangu inageuza mazingira
Nikaamua kujiripua kwenda mtaa unaonipeleka huko nyuma ya kituo cha polisi Ndo kama nikawa nimeRESET akili
Vitu vyote vikarudi kama vinavyitakiwa kuwa.
Hii inatokeaga mkuu
 
Njia rahisi sana ya kufanya ni kuchukua contacts zao

Maduka yenyewe 9 hapo ungechukua namba zao kwani lolote laweza tokea na moja wapo ni hili la kusahau mzigo wa thamani umeuacha wapi

Lingine la kufanya ni kujua location kwa google map na kuweka point zako zote
Hii itakusaidia kwa mizunguko yako

Mimi miji yote ninayoenda kama natamani kutembea kwa miguu natumia ramani tu na itanirudisha nilipokuwa hata kama ni Paris
Mkuu kwa Paris ni rahisi kutumia kuliko huku kwetu Tanzania sababu locations nyingi hazijawekwa kwenye ramani. Yaani binafsi nimekuwa nikiadd missing places nyingi tu, cha ajabu ni ofisi kubwa na bize lakini unakuta kwenye ramani hazipo.
 
Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.

Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo.

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba.

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa.

Nilikua na location 9, nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee.

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga"?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi.

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki.

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee.

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa.

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini.

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia.

Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza.

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi.

Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo.

Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta.

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Kama kisehemu kidogo tu kama Kariakoo unapotea, utaweza kuishi kwenye miji mikubwa kama Paris au New York kweli ?
 
Mkuu kwa Paris ni rahisi kutumia kuliko huku kwetu Tanzania sababu locations nyingi hazijawekwa kwenye ramani. Yaani binafsi nimekuwa nikiadd missing places nyingi tu, cha ajabu ni ofisi kubwa na bize lakini unakuta kwenye ramani hazipo.

Unajua tatizo ni kuwa watu hawana muamko bado wa technology ambapo duniani kila biashara inataka ijulikane kupitia mitandao na map ni muhimu sana
Mfanyabiashara yuko peke yake na duka lake halafu unakuta hata elimu hana
Lini atajua aweke jina humo?
 
Hata mie nilipotea,harafu nikawa nasubiliwa na watoto wa kike wachukue mzigo,mm nazunguka tu ,wao wanauliza upo wapi ??,mie nakujaaaa,unaanzaje kumwambia mtoto wa kike umepotea mchana kweupe? Walikuwa askari fulani, wananiambia tupo hapa sheli ,mm sheli naifaham ila siku hiyo niliitafuta bila kuiona

hadi wakakata tamaa ,wife ananipgia cm kuuliza nipo wapi ,si nikaanza kumlaum ,mnakaa mnanituma tuma tu,mm nimepotea ,ndo kuniulizia nipo maeneo yenye mwonekano gani ,nikamtajia ndo kuniambie nishike welekeo gani ndo pona yangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom