Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.

Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo.

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba.

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa.

Nilikua na location 9, nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee.

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga"?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi.

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki.

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayowee, pembeni kuna jamaa kajikalia kachoka kanyoosha miguu na mizigo yake ananung'unika, sijui nini kimempataa.

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa.

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini.

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia.

Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza.

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi.

Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo.

Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta.

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"

Ilifika hatua nakutana na Henganjifu na maji yangu, ndio nashtuka kumbe nazunguka hapa hapa.
 
K.koo unaweza uone mwenzako yupo bussy kutafuta pesa kumbe kapoteanaaa anajitafuta.

Maajabu ya Kariakoo kuzunguka na kushangaa umerudi duka ulilotoka ni kitu cha kawaida, ila dhamilia kutafuta duka ulilotoka sasa kama utalipata.

Kuna jamaa yangu naye alipoteana, inafika jioni anasema au niende polisi?????

Nikamuuliza unaenda polisi umetapeliwa? Haya lets say umedanganya ukadai umetapeliwa, haya wakikuambia tupeleke utaenda wapi?...

Kariakoo achana tuu na duka, ukiingia kule kati, kuitafuta tuu barabara kuu ya msimbazi pale polisi ni mtihani, badala ya kuifuata unaitoroka kuelekea mnazi mmoja, unakutana na mtu posta unamuuliza aggrey ipo wapi hapa?????
Au unamuuliza mtu, "huku naenda wapi?"

Mimi kipindi ndio naanza machimbo ilikua nikifika sehemu nikifanya manunuzi nikaacha mzigo, naigingia google map na search location then na save au ku screenshot, baadae nafuatilia tuu, kwa njia hio sijawahi potea, kwa sasa sihitaji uongozi wowote popote natoka...

Niliwahi kupotea Tanga usiku kwenye zile barabara zao za namba, ikabidi nirudi baharini nianze kuhesabu barabara.

Kama google map haipandi, tumia Google earth.
 
Bhs wewe sio mzoefu na Kariakoo, Kariakoo unatakiwa uijue mitaa yake ma majina yake mfano machimbo ya nguo ni Congo street na nyamwezi street lakin kuna mitaa ambayo inakutana na congo au nyamwezi ukijua hlo bhs kariakoo huwez potea mtu akikwambia nko agrey na congo chap unakimbia. Kariakoo kila bidhaa najua mtaaa inakopatikana
 
Njia rahisi sana ya kufanya ni kuchukua contacts zao

Maduka yenyewe 9 hapo ungechukua namba zao kwani lolote laweza tokea na moja wapo ni hili la kusahau mzigo wa thamani umeuacha wapi

Lingine la kufanya ni kujua location kwa google map na kuweka point zako zote
Hii itakusaidia kwa mizunguko yako

Mimi miji yote ninayoenda kama natamani kutembea kwa miguu natumia ramani tu na itanirudisha nilipokuwa hata kama ni Paris
 
Wakati unanunua si pia unaandika kwa kitabu yako? Basi pale juu andika jina laduka na number zao

Dubai wanakupa busness card

Maana kama unanunua sehemu zaidi ya 9 hata kama ni mzoefu ni rahsi kusahu

Mali bila daftari ...
 
Mimi nikiwa sehemu nimepotea vile ninavyotembea kwa kudunda kiblazameni na kujidai ili watu wasinishtukie unaweza kusema huyu jamaa ni mwenyeji wa eneo hili,kumbe kichwani nina stress tele sijui hata naenda wapi.

Niliwahi kupotea zanzibar maeneo ya mji mkongwe,kila ninapopita sipo na milango inafanana,nilizunguka nadhani watu wa mtaa ule walishanizoea tayari siku ile
 
Kuna dada alipiga yowe kama wewe na anachagua watu wakuuliza mimi nilivaa suruali ya kitambaa kubwa nimekula mkanda nje ndio akanifuata kuniuliza alizunguka kuanzia saa nne asubuhi Hadi nakutana naye saa kumi.

Alinunua kandambili baada ya viatu vya mchuchumio kumchosha kwa kuzunguka

Alikuwa anataka atoke akapande bus za mbagala
 
Hahahaha hii sio chai mkuu maana umenifanya nicheke Kwa nguvu
Kuna dada alipiga yowe kama wewe na anachagua watu wakuuliza mimi nilivaa suruali ya kitambaa kubwa nimekula mkanda nje ndio akanifuata kuniuliza alizunguka kuanzia saa nne asubuhi Hadi nakutana naye saa kumi.

Alinunua kandambili baada ya viatu vya mchuchumio kumchosha kwa kuzunguka

Alikuwa anataka atoke akapande bus za mbagala
 
Siku moja natoka tegeta na lift ya gari la mshikaji mida ya saa moja usiku,tulipofika k/koo jamaa kanishusha akaelekea zake ferry anaenda kigamboni mm ikabidi nichukue usafiri wa home kule gerezani..nikikumbuka Ile siku kilichotokea nachekaga tu maana jamaa tulipofika k koo aliniamsha Tu oya mwanangu kariakoo hii km vp tomorrow basi..nikashuka!!

usingizi jumlisha usiku sikujua kbs nimeshuka mtaa gani. Akili iliganda km nusu saa najiuliza jamaa kanishusha wapi hapa? Ikanibidi nitembee Tu mm mtoto wa mjini bn siwezi potea k/koo lkn bado akili haisomi kbs ninakoenda ni wapi

Nikasema isije nikatokezea kusikojulikana maana nimetembea kishenzi sifiki gerezani ngoja niulize.Nikamcheki muuza mayai kumuuliza asee naelekea iliko stend ya mwendo Kasi gerezani akanijibu sasa huku unakoenda mbona unakaribia kufika mnazi mmoja ..nikamwambia niitie bodaboda akanijibu labda bajaji.Nikakodi bajaji Kwa buku 4 Hadi gerezani..nikikumbuka najiuliza hivi ilikuwaje nikapotea k/koo siku ile.Sipati jibu
 
Kuna dada alipiga yowe kama wewe na anachagua watu wakuuliza mimi nilivaa suruali ya kitambaa kubwa nimekula mkanda nje ndio akanifuata kuniuliza alizunguka kuanzia saa nne asubuhi Hadi nakutana naye saa kumi
Alinunua kandambili baada ya viatu vya mchuchumio kumchosha kwa kuzunguka
Alikuwa anataka atoke akapande bus za mbagala
We jamaa comedian side,jf ni burudani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom