Umeshawahi kuona mtu anafumaniwa kwa mkewe wa ndoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeshawahi kuona mtu anafumaniwa kwa mkewe wa ndoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 4, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Je, umeshawahi kusikia mtu anashitakiwa kwa kuzini na mke wake wa ndoa? Ni swali la kuchekesha kidogo, lakini ukweli ni kwamba, jambo hilo, limeshawahi kutokea.Wapi na kwa nani? Ilikuwa kwenye kesi ya Ramadhani dhidi ya Mohamed ya mwaka 1983 ukurasa wa 309 wa ripoti za sheria Tanzania (Tanzania Law Report).

  Kesi hii ilianzia mahakama ya mwanzo ambapo mtuhumiwa alishitakiwa na Mohamed kwa kuzini na Mwanaidi wakati mwanaidi alikuwa ni mke halali wa ndoa wa Ramadhani. Katika kesi hii Ramadhani alishinda, lakini Ramadhani alikata rufaa katika mahakama ya wilaya na rufaa hiyo alishinda.

  Lakini hata hivyo kwa uchungu wa kuporwa mkewe, Ramadhani naye alikata rufaa katika Mahakama kuu. Je, hukumu ilikuwa ni nini? Hebu tupate kwanza historia kamili ya kesi hii.

  Hukumu katika mahakama kuu ilitolewa tarehe 29 mwezi Julai mwaka 1983, na katika hukumu hiyo, jaji alisoma historia ya kesi na historia hiyo ilianzia Desemba 1978 ambapo Ramadhani alimuoa Mwanaidi Mwiru na walikuwa wanakaa wote kwa wazazi wa mwanamke na Ramadhani alimlipia mkewe mahari ya ng'ombe wawili.Mwaka 1980 Ramadhani alipata safari ya kibiashara na kwenda Endasak (bila shaka mkoani Arusha).

  Lakini mara tu bwana Ramadhani alipoondoka ndugu wa mke waliingiwa na tamaa na wakaamua kumwoza kwa mwanamume mwingine aliyeitwa Mohamed na ndoa ilifanyika tarehe 9 Julai 1980 kwa mahari ya ng'ombe watatu.

  Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu kwani mwezi Oktoba, 1980, walishindwana na Mwanaidi alirudi kwao na Mohamed aliahidiwa kurudishiwa ng'ombe wake.

  Mwezi wa Novemba, mwaka 1980, Ramadhani alirudi nyumbani kutoka katika safari yake ya kibiashara na alishangaa kuambiwa kuwa ndani ya miezi kadhaa aliyokuwa hayupo, mkewe alishaozwa kwa bwana mwingine.

  Ramadhani hakutaka maneno mengi, bali alichofanya ni kwenda nyumbani kwa kina Mwanaidi na akamchukua Mwanaidi na kuondoka naye hadi nyumbani kwake.
  Mwezi Aprili, mwaka 1982, Mohamed alimshitaki Ramadhani kwenye mahakama ya mwanzo, akidai kuwa Ramadhani alizini na mkewe (Mwanaidi) na hivyo anamdai fidia ya ng'ombe saba.

  Hata hivyo, madai yake hayo yalitupiliwa mbali na Ramadhani alishinda kesi hiyo na hakimu wa mahakama ya mwanzo alidai sababu ya kumpa ushindi Ramadhani ni kuwa ndoa yake ilitangulia, ingawa ndoa zote ni halali.

  Mohamed hakupendezwa na kushindwa kwake katika kesi hiyo, hivyo alikata rufaa kwenye mahakama ya wilaya na katika mahakama hiyo mambo yaligeuka na Mohamed alishinda kesi na sababu ya kushinda, hakimu alisema ni kuwa ndoa ya Ramadhani ilikuwa ya kimyakimya yaani haikuwa na "shangwe za harusi," hivyo ilikuwa ni batili na hata jamii haikufahamu kama Ramadhani alimwoa Mwanaidi, wakati ya Mohamed ilikuwa na shangwe na zaidi ya hapo ilifanyika baada ya matangazo ya siku 21 na ilifuata taratibu zote na hivyo ikajulikana na jamii nzima.

  Katika kipindi hiki kulikuwa na mvutano kati ya wanasheria, kama ili ndoa itimie ni lazima kuwe na sherehe. Wapo waliosema kuwa, sherehe ni lazima ili ndoa iwe ndoa, lakini wengine walisimamia zaidi vifungu vya sheria na kusema shangwe si lazima alimradi tu kuwe na makubaliano huria na ndoa iwe kati ya jinsia mbili tofauti zilizodhamiria kuishi maisha yote pamoja.

  Ramadhani hakufurahishwa na maamuzi hayo ya kuporwa mke wake yaliyofikiwa kwenye mahakama hiyo ya wilaya, hivyo naye alikata rufaa Mahakama Kuu.Katika mahakama kuu suala lililokuwa katika mgongano lilikuwa ni ndoa ipi ni halali kati ya ile ya Ramadhani na ya Mohamed? Na katika kufikia maamuzi, Jaji alitumia sheria kama inavyosomeka, ‘literal meaning' na hakuruhusu au hakutazama mazingira mengine katika kutafsiri maana ya ndoa.

  Katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 aliyotumia Jaji, kifungu cha 9 (1) ndoa inatafsiriwa kama muunganiko huria kati ya mwanamume na mwanamke waliodhamiria kuishi pamoja kwa maisha yao yote. Zaidi ya hapo Jaji alisema kwamba katika jamii ambazo zinafuata sheria za kimila, ndoa halali huweza kufungwa kwa kutumia sheria za kimila na kutokuwepo shangwe za harusi na kutokufuata milolongo mingine, hakuwezi kubatilisha ndoa hiyo kama viini vyote vya ndoa halali kama ilivyotafsiriwa kwenye kifungu cha 9 (1) cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 vipo.

  Jaji aliendelea kusema kuwa Ramadhani na mashahidi wake, akiwemo mshenga wake walithibitisha kuwepo kwa ndoa kati yake na Mwanaidi. Zaidi ya hapo Mwanaidi mwenyewe pia alikiri kuwa walifunga ndoa ya kimila na Ramadhani. Kwa kuongezea Mwanaidi alisema kuwa ndoa kati yake na Mohamed ilifanyika baada ya kulazimishwa na wazazi wake. Hivyo, kutokana na sababu hizo hapo juu, Jaji alisema kwamba, ndoa kati ya Mwanaidi na Ramadhani ilikuwa halali japokuwa haikuwa na shangwe na aliibatilisha ndoa kati ya Mwanaidi na Mohamed.

  Kwa kuongezea Jaji alisema kuwa sheria zetu haziruhusu mwanamke kuolewa na wanaume wawili kama inavyoonekana kwenye vifungu 15 (3) na 152 (1) vya sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971.Kwa kumalizia Mahakama Kuu ilisema kwamba mahakama ya mwanzo haikufanya makosa kwa uamuzi iliyotoa, ingawa ilikosea pale tu iliposema ndoa zote ni halali. Hivyo, rufaa ilikubaliwa na Ramadhani alirudishiwa mkewe na Mohamed alitakiwa kulipa gharama za kesi hiyo.
   
 2. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Its so fun ila kuna kufundisho hapo
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  Asante, nimeisoma.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ukistaajabu ya Musa....
   
 5. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  Hata kama ndoa ya Mohamed isingekuwa ya kulazimishwa na wazazi wa mwanaidi, bado sio ndoa halali kwakuwa hiyo tayari ni kesi nyingine, Mwanamke akiolewa na wanaume wawili inaitwa bigamy na atashitakiwa kwa kosa hilo. Pili inashangaza kuona Bwana Ramadhani hakuwa incorporate wazazi wa mwanaidi kama accomplice katika kutenda kosa hilo, labda ni kuwaheshimu tu lakini nao wana hatia equally na Mohamed.

  Mwisho sheria ya ndoa Tanzania inatambua aina tatu za ndoa kati ya mwanamke na mwanaume, yaani ndoa ya kimila, serikali na ya dini. Pia sheria haitoi fulsa kwa sherehe kuwa kama kigezo cha kuhararisha au kubatilisha ndoa.
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu Lazima nioe kwa shangwe, then mshenga lazima!
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Sio bigamy ni POLYANDRY
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Hawa wazizi wa mwanaidi ful sanaa, wapo kimasilah zaidi teh!
   
 9. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  Bigamy (noun) crime of being simultaneously twice married

  Polyandry (noun) simultaneous marriage to multiple husbands ( the custom of having more than one husband at a time)


  Zingatia hizo red mbili, nilimaanisha crime (Uharifu) sio utamaduni (customary)
   
 10. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kumbe haya yameanza zamani eeh? Last month kuna engneer kamdamp mke wake halafu kamvalisha binti mdogo pete ya uchumba. Mke kagundua ameweka pingamizi, mume anadai kachoka kero za mke na mke anadai bdo anampenda mumewe. Alieveshwa pete ni mjamzito na ni mtoto wa mchungaji. Kesi nadhan iko mahakamani, nadhani kila m2 atapata haki yake.
   
 11. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wazazi wengine wanafanya watoto wao mradi, sijui hata kama hii kesi walihudhuria, ila nimependa msimamo wa msichana japo mwanzo alishawishika badae akagundua kosa na kujirudia nyumbani

  Off topic, hivi Mulama hapo kwenye avatar yako ulikuwa unafanya nini, nimepata hisia mbaya kama nini, nakuona kama umemshika mtu kiuno, unaondoka kichuma mboga, sorry hahahaaaa
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hivi hawa kina Mwanaidi, Mohamed na Rashid wapo wap? I wish wangekutanishwa pamoja wajadili hoja tupate burudan teh! Najua mpaka sasa mohamedi ana HASIRA!
   
 13. A

  Aine JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Very interesting, sipati picha sasa alivyoshinda mohamed alimchukua mwanaid na kwenda kuishi naye kama mke wake au? kazi kweli kweli. Wazazi ndio tatizo hapo ndio maana wanawake tunaitwa bidhaa, tunauzwa uzwa hovyo tuu kama binti hana msimamo na hana watu wakumsaidia basi ni shida kweli
   
 14. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hii kali.. Thank yuo for a very interesting story.
   
Loading...