Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
966
20842129_1429550570443323_1178979454123691461_n.jpg

Basi leo ngoja nikueleze habari ya kufurahisha kuhusu nyoka huyu, kwanza ni miongoni mwa viumbe ambao wamesaidia lugha ya kiswahili kukua, kwa waliosoma kiswahili wanaweza kufahamu vyema kuwa miongoni mwa mambo ambayo husaidia kukua kwa lugha ni pamoja na lugha kukopa maneno, misimu pia kufananisha umbo la kitu na maneno, ikiwa pamoja na mambo mengine mengi,

Basi nyoka kifutu amefananishwa umbo lake na jina alilopewa, ukimuona kichwani ni mwembamba na mkia mwembamba lakini mwili wa kati ni kibonge mbaya.

Nyoka huyu hatagi bali anazaa ! Sasa usitoe macho, kama ulikuwa hujui nakufahamisha hivi nyoka katika masuala ya uzazi wamegawanyika katika makundi matatu, kundi la kwanza hutaga, kundi la pili huzaa na kundi la tatu huwa wanataga na kuzaa (hapa ndio utashangaa yaani anataga na akitotoa akabaini watoto bado dhaifu basi atawameza na kuwazaa hapo baadaye, au akiwa na mayai akabaini kwamba mazingira hayo si rafiki atameza mayai na kuzaa baadaye).

Turudi kwa kifutu wetu yeye huzaa watoto 20 na kuendelea huko, na watoto huendelea na maisha yao punde tuu baada ya kuzaliwa, Chakula kikuu cha mnyama huyu ni pamoja na wadudu, panya, mayai ya ndege, wanyama wadodo wadogo kama sungura nk, hapa hutegemea sana na umri, wapo katika makundi mawili moja wale ambao hujitokeza sehemu ambazo binadamu hufanya shughuli zake kama shambani nk.

Hawa huwa na sumu lakini si kali sana, ila waishio polini akikuuma una hatari ya kufa mapema sana na nyoka huyu ni miongoni mwa nyoka ambao wapo katika kundi la nyoka walioua sana binadamu.

Ana meno mawili juu na makali sana yaliyochongoka kama ambayo huonekana kwa simba au chui, na meno ya chini ni madogo na hujipanga kwa wingi sana lakini hayazidi kumi.

SIFA ZAKE
  1. Bingwa sana wa kujificha, watu wengi humkanyaga kwakuwa ni ngumu kumuona kwa urahisi.
  2. Si mkorofi pamoja na ukatili alionao, lakini akiona binadamu humkimbia, pamoja kwamba atakukimbia lakini atarudi mara kwa mara kuangalia je umeondoka ! Lengo likiwa ni kuendelea na shughuli zake, hivyo akikupa heshima na wewe uwe mstarabu kumpisha.
  3. Akikuona sura yake huitengeneza kama anatabasamu, sasa sio anataka kukuchekea anaweka meno sawa.
  4. Ana aibu pia.
  5. Anapowinda akiwa penye ardhi laini hujifukia, sasa kanyaga.
  6. Ana urefu wa mita moja na kilo sita au zaidi.
  7. Akikuuma utapatwa na yafuatayo, kutwoka sana na jasho, kutapika na kuishiwa nguvu.

Je umeshawahi kujua nyoka akikuuma yatakiwa ufanye nini ?

[HASHTAG]#wasalaam[/HASHTAG].
=======

Nimekopi nikiamini humu ntapata ufafanuz wa kutaalam zaidi hasa kwenye kuzaa hapo
 
Niliwahi kukutana na vifutu wakijaribu kupandana kule Kigwa, Tabora. Nafikiri Kigwa ndiyo makao makuu ya nyoka hapa Bongo, yaani kuna nyoka wa hajabu sijawahi kuona hapa Bongo. Kifutu si rahisi kuuma mtu, na ile siku nilikutana nao pale Kigwa nilijaribu kuwapisha ila wenzangu sasa walikuja kuwaua bila hata sababu. Nilisikitika sana.
 
kweli huyu nyoka mpaka umkanyage, niliwahi kuchunga ng'ombe utotoni nikabanwa na haja kubwa porini, nilipomaliza kukata gogo natafuta jani nichambe, kumbe pale karibu kabisa na niliposhusha gogo alikuwa katulia ananichora tu, ilibidi niondoke taratibu, nikaenda chambia sehemu nyingine, kumsimulia babu akasema huyo sio swila, huyo mpaka umkanyage, ndio akung'ate, na vile vile inasadikika katika kabila langu ukiwakuta kwenye shamba lako la mihogo basi mihogo itanenepa kama lenyewe na inakuwa hivyo, hizo ni imani tu za wahenga
 
Niliwahi kukutana na vifutu wakijaribu kupandana kule Kigwa, Tabora. Nafikiri Kigwa ndiyo makao makuu ya nyoka hapa Bongo, yaani kuna nyoka wa hajabu sijawahi kuona hapa Bongo. Kifutu si rahisi kuuma mtu, na ile siku nilikutana nao pale Kigwa nilijaribu kuwapisha ila wenzangu sasa walikuja kuwaua bila hata sababu. Nilisikitika sana.
Unahurumia snake!? Yeye hawezi kukuhurumia jombaa... Na tumeagizwa tuwaponde vichwa, hivyo hao jamaa walitimiza maandiko....

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kukutana na vifutu wakijaribu kupandana kule Kigwa, Tabora. Nafikiri Kigwa ndiyo makao makuu ya nyoka hapa Bongo, yaani kuna nyoka wa hajabu sijawahi kuona hapa Bongo. Kifutu si rahisi kuuma mtu, na ile siku nilikutana nao pale Kigwa nilijaribu kuwapisha ila wenzangu sasa walikuja kuwaua bila hata sababu. Nilisikitika sana.
Hahaaaa ukatili mkubwa sana kifutu pia ni dawa ya kukuza kibamia ukichanjia mkia wa kifitu ni shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu nyoka mpole sana wanapatikana sana maeneo ya baridi , siku moja nikiwa mafinga jkt nilitoroka mkesha nikaenda kulala porini nilikuwa na blanket nikiwa nmelala kumbe likaja likifutu na kuingia kwenye blanket asubuhi nashtuka linanitekenya...
Wala halikunidhuru
 
Huyo nyoka nakumbuka nilimkanyaga na baiskeli nikiwa speed enzi za utoto tairi ya nyuma ilipomkanyaga nikateleza nikadondoka sikumuona maana ilikua eneo la vumbi baadae nikamwona akitokomea vikachani kwa speed sana niliporudi kumueleza mjomba akanijulisha usiende tens eneo hill atarudi tena..
 
Back
Top Bottom