Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Pununkila

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
276
1,000
Wadau kwa hii sijui aliyekuwa na dharau ni yupi.. Nikiwa mkoa wa Arusha nafanya biashara mwaka 2015/2016 nilikuwa na hizi mashine za betting za kampuni Premier na huwa mauzo yao yanatumwa kwa m-pesa kwanda namba yao ya kampuni. Siku moja nikatuma mida ya saa nne nikaendelea na kazi zangu. Sasa hii kampuni ilikuwa kama hujatuma mauzo yao mashine inafungwa. Basi mida ya saa kumi jioni nashangaa mashine imefungwa. Kucheki salio la m-pesa pesa imetoka ukiwapigia Premier wanasema sijatuma na kweli sms haijarudi ila hela imekatwa.
Basi nikawapigia Voda wanasema kweli nimetuma hela na wanaiona ipo hewani nivumulie baada ya masaa 72 (kama sijakosea) itafeli itarudi kwangu. Nikaamua kutafuta hela nyingine nikalipa kwa namba nyingine ili biashara iendelee.
Kesho yake mida ya asubuh nikapita vodashop moja ipo karibu na clock Tower Arusha. Nikaeleza tatizo langu kwa wahudumu wakaona hawaliwezi wakanipeleka kwa meneja wao pale jina limenitoka. Akanipokea vizuri na akaona tatizo langu na akasema hela anaiona ila anaomba nije kesho yake. Kesho yake nikaenda asubuhi hayupo naambiwa nije saa nane, sikuweza kurudi nikakaa siku mbili tena nikarudi nikamkuta akadai alikuwa nauguliwa na mtoto so hakuweza kutatua shida yangu ila nije kesho atakuwa amekamilisha.
Ikumbukwe Wakati naenda vodashop pia nilikuwa napiga simu customer care majibu yao ni mepesi tuu hela ipo hewani itarudi kwako. Lini itarudi hawana jibu na kili nikiwapigia nilikuwa nawarecord. Na pia nikishamaliza kuongea nao walikuwa wanatuma sms inatosema tatizo lako limepewa id ****** utajulishwa likikamilika. Na mimi nikawa natunza kama ushahidi.
Nimerudi kwa meneja wa hapo vodashop sound ni zile zile nikachoka. Basi niakona niende vodashop nyingine ya pale karibu na metro pole hapo hapo Arusha. Huyu alisema lipo nje ya uwezo wake niende vodashop kubwa ba kubwa ndio iyo hapo clock tower.
Nikaona hii hela ishapotea sina cha kufanya. Basi nilikuwa na mshakaji wangu ndio ametoka chuo kusomea sheria nikamwelezea akaniambia waandikie demand letter wape siku saba kama hela haijurudi kafungue kesi mahakamani.
Nikaona huu ushauri ni wa kuzidi kupoteza muda nawezaje kupambana na kampuni kubwa kama vodacom? Baadae nikasema potelea pote ngoja na mimi nikajionee nini kitatokea huko mbeleni kweli nikaandika demand letter nikapeleka pale branch ya clock tower naambiwa hakuna wa kupokea labda nipeleke pale karibu na metro pole. Nakapeleka akasema hilo lipo nje ya uwezo wake nipeleke pale pale nikarudi nikaambiwa nilete kesho yake nitamkuta meneja. Kesho yake nikapeleka kweli nikamkuta na ananikumbuka vzr tuu. Akasema siku mbili tuu jambo langu litakuwa tayari.
Nilikaa jumla ya siku 33 sijawahi kuona hela ikirudi wala kupigiwa simu na voda kuhusu hela yangu. Basi kama kawaida rafkiyangu akaniongoza kwenda kufungua kesi mahakamani. Hapa kuna utaalam mwingi kidogo kuhusu hizi kesi za namna hii. Basi nikafuta ushauri wake nikafungua kesi nikapewa na samansi (Summons) niipeleke voda.
Hapa ndio nilianza kuona nguvu ya Mahakama. Basi meneja wa kwanza kakimbia hataki kupokea, meneja wa pili nae nduki hataki hata kuskia hicho kitu. Basi tukashauriana niipeleke ofisi ya kanda ya vodacom ipo pale summit center karibu na kilombero. Kufika pale nilikutana na secretary wa meneja wa kanda wakuu ukiskia dharau ndio nilikutana nazo ana kwa ana. Akaniuliza unaapointment na meneja nakumbuka hadi jina la meneja alikuwa anaitwa Hendrish. Nikamjibu hapana nimeleta Summons inatakiwa nikabidhi na isainiwe. Akanijibu peleka makao makuu Dar yapo pale mlimani City hapa hatupokei na kwani hujui mtandao unaweza kukwama mda wowote na maneno kibao ya shombo.
Nilikuwa na uyo mshkaji wangu akajibu kwa upole tuu dada kwani tumeleta kesi kwako au tumesema tunataka kuonana na meneja wa kanda? Akajibu kwa dharau yupo busy na kama huna appointment naye huwezi kuonana nae.
Mshakaji akamjibu hizi dharau zako hazina mda mrefu sana, sisi tutaweka hii summons hapo posta wala sio hela nyingi ifike isifike matajua wenyewe sisi tutaenda na ushaidi wa resit ya ems mahakami kwa hiyo wala hujatukomoa.
Kumbe wakati tunazozana pale meneja alikuwa anaskia akamwambia secretary waambie waje ndio kuingia kwa meneja na kueleza a-z ya tukio zima. Basi meneja wa kanda alikuwa mstaarabu sana kwa kweli . Basi akapokea summons akasaini kaomba nirudi kesho yake tuzungumze na secretary akaambiwa asija akanizuia tena siku yoyote nitakayofika ofisini kuonana na meneja wa kipindi icho Mr Hendry.
Baada ya kutoka hapo ofisini nikaenda kwenye biashara yangu kuendelea na shughuli zangu baada ya masaa mawili nikaona sms ya mpesa muamala umerudi iyonilikuwa kama siku ya 36 hivi.
Nilipoenda kesho yake kwa meneja akaomba iyo kesi niifute maana kama ningekuja mapema kwake yasingefika huku. Mshakji wangu akasema kama wanataka wafute walipe fidia ya hasara tuliyopata shilingi milioni mbili. Hapa nilibaki hoi maana mshakaji nasema hadi hela tulizotumia kula hotelini mjini wanatakiwa kulipa maana tilikula tukiwa tunafatilia kesi.
Hendry akasema hiyo hela hawezi kuilipa basi watakuja kwenye kesi. Siku moja kabla ya kesi nikaanza kupokea simu nyingi sana za wanasheria wa vodacom wakitaka tunegotiate msimamo ukabaki milioni mbili wakasema wanatia laki mbili nikakataa. Wakanitishia sana tuu ila nilikuwa nimelishwa maneno na mshakji kuwa waambie mahakama itaamua na itakachoamua mahakama nitakubaliana nacho hata kama ni elfu moja.
Basi kweli majibu yangu yalikuwa na nguvu usiku wake kesho kesi wakanipigia tena wakaanza kunibembeleza nichukue hata milioni moja tuondoe kesi mahakamani. Nikawaambia mwisho kabisa milioni moja na laki mbili kama hawataki kesho tukutane mahakamani.
Kesho yake kweli akaja hadi mahakamani wakataka tuondoe kesi wamekubali kulipa icho kiasi. Basi hakimu anamuiliza mmekutana na kiboko yenu ee akamjibu hakimu hio hela kidogo sana kwa kampuni kama vodacom. Ee bana ee hakimu akawa mbogo ghafla akasema haya njoo hapa andika madai ya milioni 8 achana na hizo kidogo. Jamaa aliomba sana kwa ile dharau aliyoonyesha pale kwa hakimu. Badae wakamaliza kinamna. Basi na mimi nikajaza form flani hivi kule voda inayoonyesha kesi imeisha na nimeridhika na makubaliano tuliyoyafikia.
Nikakaa kama mwezi nikapokea hela yangu nikampa mshakaji nusu na mimi nikala nusu.
*****×**************×*********
Mtanisamehe kama sijaandika vizuri.
Safi Sana Yani umetisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom