Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
8,435
2,000
Salaam wakuu! Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, katika mihangaiko yako ya maisha ya kila siku, umewahi kwenda sehemu kupata huduma fulani na ukaletewa nyodo na mhudumu husika, kwa sababu tu aidha mmiliki ni mpenzi wake, au vyovyote?

Karibuni!
Hili si ni kawaida kwa wanawake au? Awe na maisha au asiwe nayo kikubwa anamiloki kile kitobo
 

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
2,656
2,000
Ccbrt hawana nyodo boss tena kuna vipaza sauti kabisa kazi yako ni kusikiliza tu.

mimi wamenifanyi ccbrt wewe unasema hawana nyodo labda walikuheshimu wewe ila niliandika msg kwa boss wao na maono ya karatasi kwenye kibox chao
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
13,482
2,000
Ngoja nishee habari Moja kuhusu ma secretary wenye nyodo mwaka 98 nilikuwa na mgogoro wa ardhi na mtumishi mmoja wa umma akiwa Ni afisa ardhi. Baada ya suala kuwa halishughulikiwi nikaamua kwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa kupata msaada nilikuwa na miaka16 kipindi hicho.

Sasa nilipofika kwa katibu muhutasi huyo ili kupata ruhusa akanikatalia eti nimwambie shida yangu halafu akamwambie bosi wake akikubali ndo ataniruhusu, Katibu muhutasi akaniuliza kwa ukali "UNATAKA NINI NAWEWE KIBWENGO" Nikamjibu NIMEKUJA kuongea na Baba kwani Mimi hunijui? Basi akajifanya kunijua akaniruhusu nikaingia.

Muda kidogo akaniletea chai nzitoooo. Mkuu wake akashikwa na butwaa.alipotoka Yule muhutasi nikamueleza Mkuu Yule shida yangu Mambo yakaenda sawa.nikatoka na kumuaga.INA MAANA NISINGE MDANGANYA NISINGE WEZA KUFIKISHA UJUMBE WANGU KWA MKUU WA MKOA NA HUWENDA TATIZO LISINGEPATIWA UFUMBUZI
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,347
2,000
Nililetewa dhihaka na pump attendant Mimi kawaida yangu sikaagi na gari moja.
Nilikuwa na Rav4 nikauza, nikanunua Starlet nikauza, nikanunua Brevis nikaja nikauza nikaja nikanunua Passo rangi ya mgomba ndo siku naenda kujaza mafuta shell ambayo nimeizoea na kituo kizima wananijua. Huyo bidada akaanza nyodo eti hoo kashafulia kanunua kigari cha kike.

Nilimsikiliza sikumjibu kitu nikasema ww dawa yako lazima nikupige kapumbu. Kweli nikaja kufanikiwa nilipiga 3times.
....Hapa naona kama habari kuu sio kufanyiwa Nyodo bali habari ni kuhusu Mkuu unavyobadilisha Magari....!!
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,529
2,000
Nyoda naonyeshwaga sana kwenye restaurant zetu,unaagiza cocacola muhudumu analeta pepsi,ukimuuliza anakwambia cocacola zimeisha pepsi na cococala ni moja tofauti jina.
hii sasa sio nyodo ni kulahisisha mambo.

hana tofauti na yule mama aliyeonja chumvi kwenye maharage ya mteja kwa kutumia kidole chake,kisha kumwambia mteja chumvi imo humu,endelea na menu.
 

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
625
1,000
Kuna siku nmeenda buchani kununua nyama ya ng'ombe, nikamwambia muhudumu nipe nyama ya Kombe kilo 1, yeye akanikatia nyama nyingine tu tofauti na kombe afu imejaa mifupa mingi kwelikweli.
Nikamwambia kiustaarabu tu kua naitaji nyama ya kombe na kama huna ungenambia, akaanza kujibu ujinga wake pale; nikamuuliza blaza hii nyama nalipa mimi au unalipa wewe? Pia naenda kula mimi au unaenda kula wewe? Akawa Hana majibu, basi nikamwambia wewe baki na nyama yako nami nabaki na hela yangu. Alikasirika sana mjinga yule
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,461
2,000
Kuna bar moja nikwenda. Kufika tu akajipendekeza bar maid mmoja kuja kunihudumia. Basi nikamwambia akaniletee supu ya kuku jikoni na yeye achukue yake. Dakika tano nyingi supu hizi hapa. Huku nnaendelea kusoma gazeti na kunywa supu. Nikamwambia aniletee castle baridi na yeye achukue yake.

Dakika nyingi beer ziko mezani. Nikaagiza castle ya pili na yeye nikamwambia achukue yake. Baadae kidogo nikaomba bili nilipe niondoke. Kabla sijawasha gari namuona huyu ananikimbilia na kuniambia. Kaka umesahau kuchukua namba yangu.
Namba yake ili siku ukipanga kwenda, atoe huduma kama ya siku hiyo. Anajua biashara, lazima uhakikishe mteja anaendelea kuja hapo, au nakosea?
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,461
2,000
Enzi hizo za ujana wangu, kuna kipindi nilipeleka maombi ya kazi PPF, kuna mama wa makamo mapokezi aliniambia niweke bahasha langu tu mezani yamefika.

Kuondoka nikawa tu na wasi wasi sijasaini popote kuwa nimeyafikisha maombi yangu salama nikarudi lile bahasha halikuwepo mezani kuangalia vizuri niliona tu bahasha la kaki limewekwa kwenye dustbin zile nyeupe na linafanania na langu 100%(kuna mikunjo kabisa ya ile bahasha nilikuwa naiona).

Nikazuga kwa upole kuna sehemu juu sijaandika vizuri anuwani ili anipe nifanye marekebisho ili nione kama ndio hilo alilolitupa akakataa, niliwaka aisee nataka nionyeshwe bahasha yangu au anaona aibu kwa kuwa ameitupa, mwisho wa siku kuna braza mmoja na suti yake aliita mlinzi mmoja nikatupwa nje, sikuitwa hata interview
Pole! Mswahili akipata..
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,461
2,000
Ukipata nafasi nenda kamshukuru huyo Dada aliyekufanyia 'jeuri'.Amechangia pakubwa mno wewe kupata hayo mabulungutu bila yeye kujijua.
Hana mchango wowote, asipewe sifa asiyostahili. Jamaa alikuwa na mipango yake, na imekwenda kama alivyopanga na kutegemea.
 

Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
801
1,000
Salaam wakuu! Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, katika mihangaiko yako ya maisha ya kila siku, umewahi kwenda sehemu kupata huduma fulani na ukaletewa nyodo na mhudumu husika, kwa sababu tu aidha mmiliki ni mpenzi wake, au vyovyote?

Karibuni!
ukiletewa nyodo na mwanamke, wee litongoze, lipambe lisifie kinafki likijaa, litajiligeza tuu, Baada ya hapo litafune. Atakushukuru mwenyewe.
 
Apr 27, 2021
51
125
Enzi hizo nakunywa safari beer baridi nilikua na rafiki yangu tajiri wa mabasi ya mikoani, lkn huyu jamaa vaa yake usingejua kwamba Ni tajiri. Tulikwenda bar moja Ina wahudumu wawili, jamaa akamtaka mmoja white lkn white akajifanya matawi. Basi jamaa akamjaribisha yule sura mbaya na sura mbaya akakubali.
Jamaa yangu kila siku Basi likitoka mikoani lzm lije na Michele, samaki, ndizi, kuku ndio usiseme. Baadae akaamua kuoa kabisa.
Tukamwacha white na uzuri wake akiendelea kuuza bar.
Safi Sana
 

am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
570
1,000
Salaam wakuu! Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, katika mihangaiko yako ya maisha ya kila siku, umewahi kwenda sehemu kupata huduma fulani na ukaletewa nyodo na mhudumu husika, kwa sababu tu aidha mmiliki ni mpenzi wake, au vyovyote?

Karibuni!
Baba angu mkubwa mzee J
Yule mzee alisha Kaaga Us, Uk mpka U.S.S.R
So unavijua vidada vinginee Huwa vinajionaga much know......
Baba angu mkubwa aliwai kukashushua kamoja mbele yangu....
Haya maneno nanukuu kutoka kwake
Alipo kua akikawashia fire...

"Little Education is very Dengerous"

Alishushuliwa pale mpka aibu zikamjaa... ..

Jaman wadada muachage ma dharau.....

Binafsi mm Huwa nawa heshimu Sana watu.... Regardless..
 

Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
39,838
2,000
Wadau kwa hii sijui aliyekuwa na dharau ni yupi.. Nikiwa mkoa wa Arusha nafanya biashara mwaka 2015/2016 nilikuwa na hizi mashine za betting za kampuni Premier na huwa mauzo yao yanatumwa kwa m-pesa kwanda namba yao ya kampuni. Siku moja nikatuma mida ya saa nne nikaendelea na kazi zangu. Sasa hii kampuni ilikuwa kama hujatuma mauzo yao mashine inafungwa. Basi mida ya saa kumi jioni nashangaa mashine imefungwa. Kucheki salio la m-pesa pesa imetoka ukiwapigia Premier wanasema sijatuma na kweli sms haijarudi ila hela imekatwa.
Basi nikawapigia Voda wanasema kweli nimetuma hela na wanaiona ipo hewani nivumulie baada ya masaa 72 (kama sijakosea) itafeli itarudi kwangu. Nikaamua kutafuta hela nyingine nikalipa kwa namba nyingine ili biashara iendelee.
Kesho yake mida ya asubuh nikapita vodashop moja ipo karibu na clock Tower Arusha. Nikaeleza tatizo langu kwa wahudumu wakaona hawaliwezi wakanipeleka kwa meneja wao pale jina limenitoka. Akanipokea vizuri na akaona tatizo langu na akasema hela anaiona ila anaomba nije kesho yake. Kesho yake nikaenda asubuhi hayupo naambiwa nije saa nane, sikuweza kurudi nikakaa siku mbili tena nikarudi nikamkuta akadai alikuwa nauguliwa na mtoto so hakuweza kutatua shida yangu ila nije kesho atakuwa amekamilisha.
Ikumbukwe Wakati naenda vodashop pia nilikuwa napiga simu customer care majibu yao ni mepesi tuu hela ipo hewani itarudi kwako. Lini itarudi hawana jibu na kili nikiwapigia nilikuwa nawarecord. Na pia nikishamaliza kuongea nao walikuwa wanatuma sms inatosema tatizo lako limepewa id ****** utajulishwa likikamilika. Na mimi nikawa natunza kama ushahidi.
Nimerudi kwa meneja wa hapo vodashop sound ni zile zile nikachoka. Basi niakona niende vodashop nyingine ya pale karibu na metro pole hapo hapo Arusha. Huyu alisema lipo nje ya uwezo wake niende vodashop kubwa ba kubwa ndio iyo hapo clock tower.
Nikaona hii hela ishapotea sina cha kufanya. Basi nilikuwa na mshakaji wangu ndio ametoka chuo kusomea sheria nikamwelezea akaniambia waandikie demand letter wape siku saba kama hela haijurudi kafungue kesi mahakamani.
Nikaona huu ushauri ni wa kuzidi kupoteza muda nawezaje kupambana na kampuni kubwa kama vodacom? Baadae nikasema potelea pote ngoja na mimi nikajionee nini kitatokea huko mbeleni kweli nikaandika demand letter nikapeleka pale branch ya clock tower naambiwa hakuna wa kupokea labda nipeleke pale karibu na metro pole. Nakapeleka akasema hilo lipo nje ya uwezo wake nipeleke pale pale nikarudi nikaambiwa nilete kesho yake nitamkuta meneja. Kesho yake nikapeleka kweli nikamkuta na ananikumbuka vzr tuu. Akasema siku mbili tuu jambo langu litakuwa tayari.
Nilikaa jumla ya siku 33 sijawahi kuona hela ikirudi wala kupigiwa simu na voda kuhusu hela yangu. Basi kama kawaida rafkiyangu akaniongoza kwenda kufungua kesi mahakamani. Hapa kuna utaalam mwingi kidogo kuhusu hizi kesi za namna hii. Basi nikafuta ushauri wake nikafungua kesi nikapewa na samansi (Summons) niipeleke voda.
Hapa ndio nilianza kuona nguvu ya Mahakama. Basi meneja wa kwanza kakimbia hataki kupokea, meneja wa pili nae nduki hataki hata kuskia hicho kitu. Basi tukashauriana niipeleke ofisi ya kanda ya vodacom ipo pale summit center karibu na kilombero. Kufika pale nilikutana na secretary wa meneja wa kanda wakuu ukiskia dharau ndio nilikutana nazo ana kwa ana. Akaniuliza unaapointment na meneja nakumbuka hadi jina la meneja alikuwa anaitwa Hendrish. Nikamjibu hapana nimeleta Summons inatakiwa nikabidhi na isainiwe. Akanijibu peleka makao makuu Dar yapo pale mlimani City hapa hatupokei na kwani hujui mtandao unaweza kukwama mda wowote na maneno kibao ya shombo.
Nilikuwa na uyo mshkaji wangu akajibu kwa upole tuu dada kwani tumeleta kesi kwako au tumesema tunataka kuonana na meneja wa kanda? Akajibu kwa dharau yupo busy na kama huna appointment naye huwezi kuonana nae.
Mshakaji akamjibu hizi dharau zako hazina mda mrefu sana, sisi tutaweka hii summons hapo posta wala sio hela nyingi ifike isifike matajua wenyewe sisi tutaenda na ushaidi wa resit ya ems mahakami kwa hiyo wala hujatukomoa.
Kumbe wakati tunazozana pale meneja alikuwa anaskia akamwambia secretary waambie waje ndio kuingia kwa meneja na kueleza a-z ya tukio zima. Basi meneja wa kanda alikuwa mstaarabu sana kwa kweli . Basi akapokea summons akasaini kaomba nirudi kesho yake tuzungumze na secretary akaambiwa asija akanizuia tena siku yoyote nitakayofika ofisini kuonana na meneja wa kipindi icho Mr Hendry.
Baada ya kutoka hapo ofisini nikaenda kwenye biashara yangu kuendelea na shughuli zangu baada ya masaa mawili nikaona sms ya mpesa muamala umerudi iyonilikuwa kama siku ya 36 hivi.
Nilipoenda kesho yake kwa meneja akaomba iyo kesi niifute maana kama ningekuja mapema kwake yasingefika huku. Mshakji wangu akasema kama wanataka wafute walipe fidia ya hasara tuliyopata shilingi milioni mbili. Hapa nilibaki hoi maana mshakaji nasema hadi hela tulizotumia kula hotelini mjini wanatakiwa kulipa maana tilikula tukiwa tunafatilia kesi.
Hendry akasema hiyo hela hawezi kuilipa basi watakuja kwenye kesi. Siku moja kabla ya kesi nikaanza kupokea simu nyingi sana za wanasheria wa vodacom wakitaka tunegotiate msimamo ukabaki milioni mbili wakasema wanatia laki mbili nikakataa. Wakanitishia sana tuu ila nilikuwa nimelishwa maneno na mshakji kuwa waambie mahakama itaamua na itakachoamua mahakama nitakubaliana nacho hata kama ni elfu moja.
Basi kweli majibu yangu yalikuwa na nguvu usiku wake kesho kesi wakanipigia tena wakaanza kunibembeleza nichukue hata milioni moja tuondoe kesi mahakamani. Nikawaambia mwisho kabisa milioni moja na laki mbili kama hawataki kesho tukutane mahakamani.
Kesho yake kweli akaja hadi mahakamani wakataka tuondoe kesi wamekubali kulipa icho kiasi. Basi hakimu anamuiliza mmekutana na kiboko yenu ee akamjibu hakimu hio hela kidogo sana kwa kampuni kama vodacom. Ee bana ee hakimu akawa mbogo ghafla akasema haya njoo hapa andika madai ya milioni 8 achana na hizo kidogo. Jamaa aliomba sana kwa ile dharau aliyoonyesha pale kwa hakimu. Badae wakamaliza kinamna. Basi na mimi nikajaza form flani hivi kule voda inayoonyesha kesi imeisha na nimeridhika na makubaliano tuliyoyafikia.
Nikakaa kama mwezi nikapokea hela yangu nikampa mshakaji nusu na mimi nikala nusu.
*****×**************×*********
Mtanisamehe kama sijaandika vizuri.

Hahaha huyo ndio rafiki sasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom