Umeshawahi kujiuliza ni aina gani ya marafiki ulionao ?

Jollie

Member
Jul 26, 2019
35
64
Katika maisha utakutana na marafiki wengi, wapo marafiki watakao kusaidia katika kupiga hatua kutoka hali duni kufikia maendeleo pia wapo watakao kurudisha hatua moja nyuma yaani kutoka maendeleo kwenda hali duni.

Rafiki mwenye kukusaidia kupiga hatua kwenda mbele ni yule ambaye kwanza atafurahia mafanikio yako, hatokuonea aibu kukurekebisha pale ambapo umekosea au umemkosea, kufeli kwako kutakuwa maumivu kwake pia atajali muda wako.

Rafiki ambaye atakurudisha nyuma katika maendeleo yako kwanza hatofurahia mafanikio yako, hatojali muda wako, ukikosea hawezi kukuelekeza hata kama anatambua kabisa hapa umekosea na kuna huitaji wa kurekebishwa.

Je , umewahi kujiuliza marafiki ulionao ni wale wanaokusaidia kupiga hatua kwenda mbele au kukurudisha nyuma?
 
Wanasema Rafiki wa kweli Pesa nililigundua hili nlipopatwa na magumu, kila mtu anakukimbia hata wale nliokuwa wema kwao kipind cha neema, nilijifunza mengi sana, nampenda na kumheshim sana mpenz wangu licha ya magumu yote alionesha ukomavu wa hali ya juu hadi mambo yakawa sawa. Naweza kusema huyo ndio rafik wa kweli kwangu hata kama akija kubadilika ila kashapiga chapa isiyofutika moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom