Umeshawahi kujihisi mwenye hatia?

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,187
8,213
Hii ni picha ya Stephen Whittle, shabiki wa Liverpool anayehesabiwa kama mhanga wa 97 wa maafa ya Hillsborough.

Aprili 15, 1989, Liverpool ilipangwa kukutana na Nottingham Forest kwenye nusu fainali ya Kombe la FA, dimbani Hillsborough huko Sheffield.

Ndugu yetu Whittle alikata tiketi yake kama mashabiki wengine wa Liverpool, ili akashuhudie chama lake.

Lakini baadaye ratiba ya majukumu yake ikambana, akashindwa kwenda uwanjani...ikabidi amtafute mtu wa kumuuliza tiketi.

Akapata mteja, akamuuzia tiketi...halafu akaendelea na hamsini zake.

Lakini bahati mbaya ni kwamba, wakati wa mechi, yakarokea maafa makubwa kwenye jukwaa la mashabiki wa Liverpool na kusababisha mkanyagano uliogharimu maisha ya watu 96 na wengine 766 kujeruhiwa vibaya.

Miongoni mwa watu walipoteza maisha ni yule aliyenunua tiketi ya Whittle.

Hiki kitu kilimtesa sana...kwamba bila yeye kumuuzia tiketi, yawezekana jamaa asingepoteza maisha. Au kama yeye angeenda uwanjani, basi labda na yeye angepoteza maisha.

Kila Aprili 15 ya kila mwaka, Liverpool huwakumbuka wahanga wa maafa yale, na yeye kila ikifika tarehe ile, mateso katika mawazo yake yalimrudia.

Akawa anahisi mwenye hatia na kujikuta akielemewa na msongo wa mawazo na sonona...akawa anatumia dawa za kumuondolea hali hiyo miaka yote.

Februari 26, 2011, wakati wa maandalizi ya maadhinisho ya miaka 22 ya maafa yale, hali ikamzidi na akajiua.

Alijirusha relini wakati treni inakuja, ikamgonga na ndiyo ukawa mwisho wake.

Aliacha wosia kuelezea kilichomsibu na kuagiza kwamba kwenye akaunti yake aliacha fedha taslimu kiasi cha pauni 61,000 ambazo zitumike kusaidia familia za wahanga wengine maafa yale.

Whittle akawa mtu wa 97 kupoteza maisha kutokana na maafa ya 1989, ambayo yaligharimu maisha ya watu 96 siku ya tukio, na mtu mmoja, miaka 22 baadaye.

zakazakazi_1618635315221.jpg
 
Kuna kujisamehe,ukishatenda kosa na kutubu kwa moyo wa dhati Mungu husamehe.

Ila nafsi yaweza kuendelea kuuma na kujilaumu hutokea,hivyo inabidi kujitahidi kujisamehe.
 
Back
Top Bottom