Umepoteza ajira? Namna ya kupata fao lako NSSF

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,423
2,000
Hakuna fao linaloitwa la kujotoa Bali Kuna fao la kukosa ajira. Hili Kila mtu anaweza kupata Kama ifuatavyo:-

KWANZA, fao la kukosa ajira linalipwa kwa mwanachama ambae hauafikisha umri wa miaka 55 na ambae ajira yake imekoma

MASHARTI

1) Uwe umechangia mfuko (NSSF) kwa muda usiopungua miezi 18 sawa na Mwaka mmoja nanusu.

2) Ajira yako iwe imekoma kwa sababu zozote, isipokuwa kuacha kazi mwenyewe.

3) Uwe raia wa Tanzania.

4) Uweze kumthibitishia Mkurugenzi (NSSF) kuwa kwa kipindi Cha miezi 6 hujaweza kupata ajira nyingine.

UKITHIBITISHA Hayo utalipwa asilimia 33.3 (33.3,%) ya kiwango Cha mshahara wako Cha wakati wa kukoma kwa ajira yako.

AIDHA ikiwa ulichangia chini ya miezi 18 au chini ya mwaka mmoja nanusu, Utalipwa nusu (50%) ya michango uliyochangia na ndani ya miezi 18 toka ulipwe nusu hiyo, na ikiwa hujapata ajira nyingine, utawasiliana na Mkurugenzi ili kuabidili salio la michango yako kwenda kwenye scheme nyingine ya chaguo lako.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
42,862
2,000
Unawajuwa NSSF au unawasoma tu? Nenda kwenye corridor za NSSF kama hujarudi kufuta huu uzi wako.
 

Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,353
2,000
Hii asilimia thelathini na tatu (33.3%) inalipwa kama mshahara?
Italipwa kwa muda gani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom