Umenunua kigari cha milioni 15 unakata bima comprehensive. Una akili sawa sawa wewe?

Ki-gari cha milioni 15 au chini ya hapo bima comprehensive inakusaidia nini? Hicho ki_gari ukikitembelea mwaka mmoja tu kimechoka na kugeuka kuwa chuma chakavu. Sasa bima comprehensive ya nini?

Unayatajirisha bure makampuni ya bima. Wewe hunufaiki chochote. By the way, kuna watu wana nyumba zao za milioni 50, 70, 100 au 200 lkn hawajazikatia bima. Lkn wakinunua viagari vya milioni 10, 20, 30 wanakata bima. Uzwazwa huu.

N.B. Nimeona wengi wanalipa bima ya comprehensive miaka 4 au 5 halafu wanaamua kujitoa na kuanza kulipa bima ndogo. Utaahira huu.

Kalaga baho!
Boss thamahani hivi lile zoezi la kufanya kitu iwe mnato lilifaa au ndo hili linakupa stress hizi?
 
Elimu hii yw bima imeeleweka kwenye upande wa magari tu? Yaani mtu huyo huyo anayemilki duka la milioni 200 Kariakoo hajalikatia bima lkn kivari Cha milioni 20 amekata comprehensive unaona ni sawa tu?
Hapo ni sawa kabisa kwa kigezo kuwa, Ukifanya risk analysis, uwezekano wa gari kupata ajali ni mkubwa zaidi kuliko duka la kariakoo. Hivyo kinacho hitajika ni kumuelimisha tu kuwa, aongeze na duka kwenye Bima
Hata kwa akili ya kawaida tu: Nyumba na gari linalotembea barabarani kila siku ni kipi kipo kwenye hatari kubwa ya kupata ajali?
 
Back
Top Bottom