Umemgonga mtu usiku na hakuna aliyekuona utafanya nini?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,281
6,696
Habari zenu Raia wema, naomba kuwauliza wale mnaondesha na wegine
ni matumaini yangu kuwa mtakuja kuendesha siku za baadae.
Iwapo umemgonga mtu usiku na una uhakika asilimia 80 - 90
Hakuna aliyekuona,

1. Utafanya nini ukigundua yule mtu amekufa?
2.Ni kipi utakifanya ukigundua yule mtu umemjeruhi vibaya?
 
Siku ikinitokea ndio n'tajua cha kufanya, kwa sasa acha nile supu yangu taratibu...
 
Niliwahi kumgonga dereva bodaboda usiku, nikasimama halafu alikuwa kalewa, nikataka kumsaidia. Madereva bodaboda wenzake wakafika eneo la tukio, ilikuwa mida ya saa sita usiku, waliniletea shida ila bahati nzuri nilikuwa nimeshapiga simu polisi na walipofahamu mwenzao alikuwa kalewa basi wakamtorosha pamoja na pikipiki. Polisi walipofika nikaamuriwa gari ikalale polisi.. aisee process za kuitoa gari nilitamani ningekuwa nimemgonga nikaondoka zangu maana hapakuwa na shuhuda isipokuwa dogo niliyekuwa naye kwenye gari. zilinichukua two days na faini nikapigwa mimi wakati wa bodaboda alikimbia na ndiye alikuwa na makosa.. kuna vehicle inspector mmoja aliniambia nikigonga dereva wa bidaboda nihakikishe namuua then nikapaki polisi... Tanzania bwana....
 
Ha ha ha ha Duh, pole sana mkuu!
 
yaan ni bora usepe tuu kuliko kujifanya msamaria mwema unatoa taarifa polisi, usumbufu utakaopata utajuta kwanza chimbo yko lazima ikalale polisi mpk uchunguz ukamilike hilo sio tatizo pili uwe na kosa au usiwe na kosa lazima utatozwa faini Tatu kama ulikuwa una mishe zako za msingi we Fanya tuu sahau ile gari yko iliyopo kituoni maana mpak uibabadue ni shughuli pevu so kama hujaonekana usiku njia bora ni kukimbia tuu kuepuka usumbufu
 
Kama yakikutokea, hata kama ni mchana peupe. Kama ukifanikiwa kutoka salama hapo mahali, kimbia hadi tairi zichomoke. Tanzania hii si rafiki kwa mtu mwenye gari. Siwachukii mapolisi ila nadhani kila polisi mmoja mzuri, mbele yake wapo wakubwa 4 wenye roho mbaya. Hawakuachiiiii.
Ukigonga bodaboda, hata kama kajigonga mwenyewe, kimbia nasema Kimbia. Wanapokuja hapo hawana simile na wewe. Watakuchomea kwenye gari lako. Polisi wakija wanawaogopa hao boda boda hivyo watakaa upande wao wakuone ukiunguzwa.
Kamanda IGP Sirro, kama ni jipu lililoiva trafiki polisi ndio uanze nao ndipo uingie cid. Nimetoka nje ya mada lakini nasema, ukigonga mtu usiku, wala usirudi kwenda kuangalia kulikoni. Wewe kimbia, Tz haina urafiki na mwenye gari.
 
Kimbia faster toka nduki we kimbia.sio swala la uoga.bora kulogwa kuliko kukosa Uhuru jela.hit and run
 
Back
Top Bottom