Umeme wakatisha uhondo wa Mechi ya Man, Chelsea

think BIG

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
236
38
Na Mwandishi Wetu

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limesema kukatika kwa umeme katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar juzi usiku kumesababishwa na njia ya umeme kati ya Morogoro na Ubungo kuzidiwa na mzigo.

Kufuatia katizo hilo, shirika hilo limewaomba radhi wateja wake wote wakiwemo wapenzi wa soka walioshindwa kutazama mechi kati ya Manchester United na Chelsea. Mechi hiyo ilichezwa jijini Moscow nchini Urusi juzi.

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco , Dk. Idris Rashid, aliyoitoa jana jijini ilisema, hitilafu hiyo ilikata umeme katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Mashabiki wa timu hizo waliokuwa wakifuatilia mechi hiyo kwenye runinga wakiwa majumbani au kwenye baa, walilazimika kukimbilia matangazo ya redio baada ya umeme kukatika ghafla.

Furaha na shangwe zao ziligeuka hasira baada ya umeme kukatika saa 4:30 usiku wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo iliyoanza saa 3:45 usiku na kuziacha Dar es Salaam na Unguja zikiwa gizani.

Dk. Rashid alifafanua kuwa kwa upande wa Zanzibar njia inayopeleka umeme visiwani ilipata hitilafu kufuatia vikombe kupasuka baada ya kuzidiwa na mzigo mkubwa wa umeme.

"Kwa ujumla hitilafu ilisababisha umeme kukatika maeneo ya kati ya Morogoro na Ubungo, Chalinze na Hale," alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Umeme huo ulirejea jana alfajiri kwa upande wa Dar es Salaam na kwamba Zanzibar tatizo limeendelea kutokana na hitilafu zilizoko kwenye mitambo ilioko Ras Fumba visiwani hapo, kwa mujibu wa taarifa ya Tanesco. Kifaa kibovu kilichosababisha tatizo kati ya Dar es Salaam na Morogoro kiliondolewa jana saa 5:30 asubuhi baada ya kugundua eneo lenye hitilafu.

Wakizungumzia usumbufu huo mashabiki wa soka wa Kimara, Gongo la Mboto, Tegeta, Boko na Pugu, walisema kitendo hicho cha kukatika kwa umeme, kiliwakosesha uhonda mkubwa.

"Ni mechi tuliyoitarajia, tulijiandaa kwenye maeneo ya burudani tuliongeza vinywaji na huduma matokeo yake tumepata hasara baada ya kadhia hiyo," alisema Bw. Athuman Hengo mkazi wa Pugu.

Mkazi wa Tegeta, Bw. Wallace Wambura, alisema tukio hilo ni bahati mbaya na ni hitilafu za kawaida za umeme.

SOURCE: Nipashe
 
hahaha! Huyu Mkazi wa Tegeta hivi hajui kwamba suala la hitilafu halitakiwi kabisa katika vichwa vya watanzania sasa hivi, Eti HITILAFU! Sasa hivi hatuna shida ya Mabwawa kupungua maji, yaani kwa ujumla wake hatuna sababu, Richmond a.k.a ZUGAZUGA CAMP haipo tena sasa Tanesco hawana sababu kabisa. Au ndio walifikiria hatutaona Ushindi wa Man Utd?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom