Umeme wakatika Mwananyamala Hospital, Vilio vyatanda wodini!

Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
830
184
Vilio vyatanda kwenye wodi ya wazazi kutoka kwa watoto wachanga na maneno ya kashfa kwenye wodi nyingine zenye watu wazima hapa hospitalini kwa viongozi na serikali ya Kikwete baada ya nishati ya umeme kuondoka hapa majira ya saa 18:22.Wapo watakao poteza maisha kutokana na kukosekana kwa umeme usiku wa leo,japo wapo wanaoona ni haki yao kuwa kwenye mgao kwani wameshazoea.Naomba kujua serikali hii itaweza kutuambia vifo na hasara ya mali iliyosababishwa na kukosekana kwa nishati tangia mgao huu umeanza?Source mimi mwenyewe Mwananyamala.
 
Moderator ukweli utabaki pale pale kuwa Viongozi wenye dhamana ndio wanaolifikisha hili Taifa Tajiri hapa lilipo leo.
 
Mbona hilo sio la kushangaza kwa nchi hii.
Siku chache zilizopita umeme ulikatika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ajabu umeme haukatiki migodini ingawa ndipo panapotumia megawatt nyingi kuliko hospitalini.
 
Waziri wa giza anafanya kazi yake ya kuwaua wa tz na kuwatoa kafara kwa manufaa ya ccm!but what goes around comes around!time will tell!
 
Lowassa Kigeugeu,Adamu Malima Kigeugeu,Ngeleja Kigeugeu,Kikwete kigeugeu,Mukama kigeugeu,Jairo Kigeugeu Ccm kigeugeu,na Cuf kigeugeu.Ipo siku hatutacheza tena tutakuwa tunapiga wao wacheze.FREEDOM IS COMING TOMORROW.
 
kazi kweli haya matukio yawe record kwa kamera CCM wasije kana maovu yao siku watu tukianza kuwa shitaki na serikali yao kwa kuua watu
 
Mbona hilo sio la kushangaza kwa nchi hii.<br />
Siku chache zilizopita umeme ulikatika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.<br />
Ajabu umeme haukatiki migodini ingawa ndipo panapotumia megawatt nyingi kuliko hospitalini.
<br />
<br />
Niko nyamongo north mara gold mine!nashangaa mgodin umeme upo lakini centre na mahosipitali umeme haupo kwa wiki km mbili hivi tangia nimefika!nashangaa hii serikali ya kikwete!MUNGU AWEKE MKONO WAKE!
 
Nimesogea Regent Hosp generator linanguruma,jamaa yangu aliyepo Mwananyamala Hosp anasema watu wawili wamefariki kwa kukosa huduma ya oxygen kwani Dr alifuata taa amerudi amekuta nesi anawafunika Shuka uuuuuuuuuuuuwwwwwiiiii Kikwete Mungu yupo ajaenda likizo
 
CCM imeweka rehani maisha ya watanzania. Tunaishi hatuna uhakika wa kufika kesho. Huduma za afya duni ndugu zetu wengi wamekufa kwa kukosa huduma. Miundombinu duni roho za ndugu zetu zapotea kila kukicha kwa ajali. Maisha magumu vitu bei ghali watoto wanakufa kwa utapiamlo. Elimu duni, umaskini unaongezeka kila kukicha. Kinachouma ni kwamba nchi hii ni tajiri sana, ndege meli zinaingia na kutoka zikiwa zimebeba rasilimali za matrilion ya fedha toka Tz huku watanzania walio wengi wakifa kwa maradhi, njaa na umaskini. Kiujumla inasikitisha sana.
 
swala la wagonjwa kufa kwa kukosekana kwa umeme hospitali ni sharti liwekwe kwenye media watu wasome na kusikia!
 
Tunayaona na kuayasikia haya alafu Watanzania wanaoishi katika nchi zenye kuwajali watu wao, wanafungua matawi ya CCM kushabikia hali iliyopo Tanzania. Nazidi kuwalaumu watanzania kutoona kuwa CCM imetufikisha pabaya, lakini nawalaumu zaidi Wartanzania wanaoishi Ulaya, Marekani, Japan na kwingine wanaoanzisha matawi ya CCM na kuendelea kuwasaliti ndugu zao walio nyumbani.
 
kikwete tulishaambiwa ni bomu tukajifanya hatusikii.sasa ndo tukome
 
Vilio vyatanda kwenye wodi ya wazazi kutoka kwa watoto wachanga na maneno ya kashfa kwenye wodi nyingine zenye watu wazima hapa hospitalini kwa viongozi na serikali ya Kikwete baada ya nishati ya umeme kuondoka hapa majira ya saa 18:22.Wapo watakao poteza maisha kutokana na kukosekana kwa umeme usiku wa leo,japo wapo wanaoona ni haki yao kuwa kwenye mgao kwani wameshazoea.Naomba kujua serikali hii itaweza kutuambia vifo na hasara ya mali iliyosababishwa na kukosekana kwa nishati tangia mgao huu umeanza?Source mimi mwenyewe Mwananyamala.
Mbona tumeambiwa majuzi tu kuwa sasa mgawo ni history?
 
mh Mbowe alitoa onyo wkt wa kampeni kuwa,
kuichagua serikali ya CCM ni janga la kitaifa,
alikuwa sahihi hakukosea.
 
Back
Top Bottom