Umeme wa TANESCO umekuwa kero katika wilaya ya Masasi

BVR 2015

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
229
413
Sisi wananchi wa wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara kuanzia jana umeme umekuwa unakatika kila baada ya dakika 10 na kuleta madhara makubwa kwa sisi wananchi ambao tunautumia kwani tunaunguliwa na vifaa ambavyo vinatumia umeme.

Pia majokofu yanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na kero ya kata kata ya umeme,wizara husika ya nishati na madini tunaiomba iiangazie hii wilaya kuanzia kwa viongozi husika wa TANESCO kwani wmeshindwa kutatua hii kero.
 
Mikoa ya kusini imeterekezwa sana..hususani kuingia kwenye gridi ya taifa...naamini wahusika watayachukua haya na kuyafanyia kazi haraka..mana hii imekua kero ya muda mrefu sasa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hiyo mikoa inashangaza sana. Kiufupi ishatelekezwa na serikali.

Nauli ya kutoka Dar to Lindi na Dar to Mtwara inafanana. Unalipa nauli sawa.

Upo NAMATUNU?
 
Sasa zi bora hapo kwani lindi mtwara nauli ni buku tatu,
Lindi nachingwea nauli ni buku 8 mpka ten, lindi masasi nauli ni buku 5 newala pia Liwald ila nauli ni ile ile 23 elfu kwenda dar
 
Masasi tunaishi Kama tuko miaka 60,Nina mwaka mmoja tatizo Hilo bado lipo na halina ufumbuzi
 
Sisi wananchi wa wilaya ya masasi,mkoani Mtwara kuanzia jana umeme umekuwa unakatika kila baada ya dakika 10 na kuleta madhara makubwa kwa sisi wananchi ambao tunautumia kwani tunaunguliwa na vifaa ambavyo t
Vinatumia umeme ,pia majokofu yanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na kero ya kata kata ya umeme,wizara husika ya nishati na madini tunaiomba iiangazie hii wilaya kuanzia kwa viongozi husika wa tanesko kwani wmeshindwa kutatua hii kero.

Siyo huko tu, hata huku nilipo wanakata sana, maji vile vile kuna kipindi walikua wanakata sana, sasa kidogo afazali.ila umeme ndio balaa, tangu magufuri afe hawa tanesco wanakata mno. Aise wanakera munoo.
 
Back
Top Bottom