Umeme wa Kubabaisha na Zabuni Binafsi ni Hatari kwa Taifa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wa Kubabaisha na Zabuni Binafsi ni Hatari kwa Taifa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chevchsic, Mar 3, 2011.

 1. C

  Chevchsic Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Umeme wa Kubabaisha na Zabuni Binafsi ni Hatari kwa Taifa.


  Ndugu watanzania naanza kwa kuuliza hivi viongozi waadilifu waliotangulia kama Mwalimu Nyerere wangeanza biashara katika Ikulu ya kuwapatia watu binafsi zabuni za kifisadi za kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya Taifa tungefika wapi? Mnajua kuna hatari kubwa sana ya kuwapatia watu wachache binafsi zabuni za kujilimbikizia mali kupitia uzalishaji umeme? Tanzania kama nchi peke yake inajitosheleza kwa vyanzo vya umeme hata kama mvua hazipo kwa sababu Tanzania ina mito na gesi ya Songosongo ya kutosha ambayo inaweza kutumika kuzalisha umeme. Hakuna sababu ya kuwapa watu binafsi zabuni. Umeme uzalishwe na Taifa lenyewe kupitia wataalamu wa serikali na si kuwapa watu binafsi zabuni ya kuzalisha umeme kwani kufanya hivyo ni kuwapa wachache fursa ya kujilimbikizia mali kitu ambacho kinawaponza viongozi kama Gaddafi na ndio maana sasa wanaondolewa madarakani.

  Nauliza tena mlishawahi kusikia nchi gani ambapo watu wachache binafsi wanapewa zabuni ya kuzalisha umeme huku serikali ikijiweka kando? Watu binafsi wana uwezo gani kushinda taifa zima la Tanzania? Watanzania kwa ujumla wana umaskini gani kushindwa kuzalisha umeme wenyewe hadi waletewe watu wachache binafsi wawachume na kuwafilisi kupitia kuzalisha umeme. Hivi Raisi kushirikiana na Tanesco ameshindwa kutenga fungu la serikali kwa ajili ya kununua jenereta zitazotumia gesi ya Songo Songo.

  Kuna habari kwamba katika mto Kagera kuna sehemu ambapo maji yanazunguka katika bonde na hata Raisi Kagame wa Rwanda aliwahi kusema ikiwa Tanzania wangemruhusu basi angefunga mitambo katika mto huo ambao ungezalisha umeme wa kutosha kwa nchi yake na umeme mwingine angewapa Tanzania bure?

  Swali langu ni hili ikiwa Raisi Kagame anafikiria kuwapatia watanzania umeme bure, kwanini viongozi wa Tanzania wanasingizia kila siku gharama zimepanda na kwanini wanakuwa wepesi kukimbilia kuzalisha umeme wa gharama kubwa wa mafuta usiokuwa na faida kwa watumiaji watanzania? Kama Nyerere aliweza kufunga mitambo ya kuzalisha umeme wa maji peke yake je maraisi waliofuatia baada ya Nyerere wanashindwaje kuanzisha vyanzo vipya vya umeme wa maji? Na kwanini wanakimbilia kubinafsisha? Je wana mpango wowote wa kubinafsisha mabwawa na mito ya kuzalisha umeme kwa watu wachache binafsi hapo baadaye? Kuna haja ya kubinafsisha kila kitu hata kama nchi yenyewe inajiweza na inajitosheleza? Kwanini raisi Jakaya Kikwete anapenda mitambo ya kukodi? Anajua hasara ya kukodi kodi jinsi ilivyo? Kwanini asiiwezesha TANESCO ikaachana na masuala ya kukodi? Kukodi ni kunufaisha watu wachache tu na kulitia Taifa hasara kwa sababu serikali yenyewe itapoteza mapato kwa kuwaachia watu wachache wenye mitambo ya ubabaishaji. Sidhani watu wachache wana uwezo wa kupata mitambo mizuri kushinda Taifa la Tanzania. Nchi ya Tanzania ni kubwa kwanini tuiweke mikononi mwa watu wachache kwa kuwapa fursa ya kuzalisha umeme, nishati ambayo ni uti wa mgongo wa Taifa hili?

  Na kwanini Raisi alishindwa kutatua tatizo la umeme haraka kiasi kwamba wananchi waliendelea kukaa gizani kwa zaidi ya mwaka mmoja? Ni hasara kiasi gani wananchi waliipata mwaka ule 2005 kwa kukosa umeme mwaka mzima?
   
Loading...