Umeme wa Jua kubadili sura ya maendeleo Sekindari za Msalala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wa Jua kubadili sura ya maendeleo Sekindari za Msalala

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Apr 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Shija Felician,Kahama

  UMEME wa mionzi ya jua[ Solar] unaoendelea kufungwa kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige katika baadhi ya Shule za Sekondari za Kata wilayani Kahama umeelezwa kuchangia mabadiliko makubwa kitaaluma kwa wanafunzi wake wa shule hizo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kata za Ngaya,Bulige na Kinaga ambako mradi huo umeanza kutekelezwa walisema kuwa wanafunzi katika Sekondari za Kata za vijijini vyake sasa wanasoma masomo ya ziada nyakati za usiku kwa kutumia mwanga wa umeme huo.

  Walidai kuwa pamoja na mazingira magumu walioyonayo wanafunzi hao katika shule hizo za kata lakini tangu mradi huo uanze kutekelezwa kumejitokeza mabadiliko makubwa kwenye taaluma hali ambayo imeleta matumaini ya kufanya vizuri katika mitihani yao.

  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ngaya, Kafuru Songora alidai kuwa tangu kufungwa kwa umeme huo shuleni kwake wanafunzi wake hutoka madarasani saa tisa mchanana kurejea tena saa kumi na mbili jioni kujisomea hadi saa nne usiku hali ambayo imebadilisha hali ya taaluma iliyokuwa mbovu kabla ya umeme huo.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngaya, Stephen Manyanda alisema kuwa Serikali ya Kijiji hicho inafanya mkakati wa kuimarisha ulinzi katika eneo la shule hiyo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaosoma nyakati za usiku wanatoka salama.

  Mbunge wa Jimbo la Msalala ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige alisema kuwa ataendelea kufanya mikakati ya kuweka umeme kwa kila shule pindi atakapopata wafadhili na kwamba tayari amefanya hivyo katika Shule za Sekondari za Ngaya,Bulige na Kinaga.

  Umeme wa Jua kubadili sura ya maendeleo Sekindari za Msalala
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Angalau kuna viongozi bado maendeleo ya nchi yetu yako katika mioyo yao....a small thing makes a huge difference hawajui tu au wanajua ila wanapuuza
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Ni kweli uyasemayo kuna baadhi ya viongozi wana mioyo ya kibinadamu na kuna viongozi wengine wana mioyo ya kinyama kazi yao ni ufisadi kula haki za walala hoi Mwenyeezi Mungu atatupa viongozi wenye kuwaonea Wananchi wake huruma inshallah sio muda mrefu kuanzia sasa.
   
Loading...