Mr Pixel3a
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 5,054
- 7,262
Mahakama ziko wazi usieneze propaganda ili wrote tuaminiAnaandika malisa GJ
Fikiria unanunua umeme wa 45K, serikali inalamba 11K kupitia makato mbalimbali, na wewe unaambulia umeme wa 34K tu. Fikiria wewe ni mtumishi, umekatwa PAYE, umekatwa HESLB, umekatwa NSSF. Zote hizo unaichangia serikali. Halafu kile kidogo unachobakiza ukienda kujaza mafuta serikali inakula karibu TZS 700 kwa lita. Ukinunua umeme ndo kama hivi.
Ukinunua sukari, chumvi, mafuta, kote huko wanakulamba kodi zenye kuumiza. Bado hujamtumia pesa mama yako mgonjwa kijijjni ukutane na bwana tozo.
Sasa badala ya kuwaza namna ya kutatua changamoto kama hizi zinazomuumiza mwananchi, tunawaza uchaguzi wa 2025 na maumbile ya wagombea. What the hell with maumbile? Awe mwanamke au mwanaume it doesnt matter, muhimu tunataka kiongozi anayeweza kushughulikia matatizo yetu.
Kama mtu hawezi kushughulika na matatizo ya watu wake, uanaume au uanamke wake unatusaidia nini?
View attachment 1940340